VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Friday, June 26, 2015

Ajinyonga Baada ya Kubainika Ana Virus Vya UKIMWI



MKAZI mmoja wa Mtaa Myegeya katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Mathias Ngimba (41), amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga  kwa kutumia kipande cha nguo kwa kile kilichodaiwa baada ya kupimwa afya yake alibainika kuwa ana maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi  (VVU).
 
Akizungumza jana Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela,  alisema tukio hilo limetokea Juni 20, mwaka huu saa 4 asubuhi katika nyumba ambayo aliwekwa na kaka yake marehemu aitwaye Festo Ngimba.
 
Kamanda alisema marehemu Mathias Ngimba, inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kichwa pamoja na tumbo la kuhara ndipo alipochukua maamuzi ya kwenda katika Zahanati ya jeshi iliyopo Chaburuma  na kupimwa afya yake ili kubaini tatizo linalomsumbua.
 
“Marehemu alipofika zahanati alipimwa na kubainika maradhi yanayomsumbua aligundulika kuwa ameshapata maambukizi ya VVU ndipo akarejea nyumbani alipokuwa akiishi na kuamua kuchukua maamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kipande cha nguo.
 
“… alijingonga huku akiwa ameacha ujumbe uliosomeka kuwa ameamua kujitoa duniani kwa hiyari yake mwenyewe ili asiisumbue Serikali pamoja na ndugu zake,” alisema Kamanda Msikhela.
 
Kutokana na tukio hilo Kamanda  huyo wa polisi amewataka wananchi kuachana na tabia ya kujihukumu kwa kujitoa uhai kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Wednesday, June 24, 2015

Serikali Yavifuta Vyuo Vitatu na Kuvishusha Hadhi Vyuo 16


KATIKA jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dk Adolf Rutayuga alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya vyuo husika kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na NACTE.
 
Kwa kutumia Sheria ya Bunge Sura Na. 129 na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujitetea na kufanya marekebisho yaliyobainishwa,” alieleza.
 
Kaimu Katibu Mtendaji huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya Taasisi na Vyuo vya Ufundi NACTE aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi vilivyopewa maelekezo ya kufanya marekebisho vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yabainishwa.
 
Hata hivyo alisema hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake.
 
“Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa kwa makosa yafuatayo, moja kumalizika kwa muda wa Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); pili kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; tatu kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukuliwa hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na nne taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbali mbali,” alifafanua.
 
Vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na Dar es Salaam College of Clinical Medicine cha jijini Dar es Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali na Institute for Information Technology cha jijini Dar es Salaam pia chenye namba za usajili REG/EOS/014.
 
Taasisi/vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kushindwa kutimiza masharti ni pamoja na Sura Technologies – Dar es Salaam, Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam, Techno Brain - Dar es Salaam, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya, Mbozi School of Nursing – Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi.
 
Vingine ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC – Songea, CATC – Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga, COTC – Musoma, Dental Therapists Training Centre – Tanga, Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.

Mh: Gwamaka mbughi kutangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Ileje Kupitia chama cha CHADEMA Tarehe 22/06/2015








 mkutano waKutangaza nia ya kuwania Ubunge jimbo la Ileje 2015; Mahalia:Isongole Trh:22/6/2015. ............................. SI DHAMBI KUZALIWA MASIKINI LAKINI PENGINE NI DHAMBI KUBWA SANA KUFARIKI MASIKINI KWASABA BU TU YA AMA KUTOSHIRIKI MAAMUZI YA KUPATA VIONGOZI WAZURI AU KUFANYA MAAMUZI YASIYO SAHIHI. Alisema  Mbunge Mtarajiwa kupitia chama cha CHADEMA.
maelezo mafupi kuhusu Ahadi zake kwa wananchi wa Ileje

 Ndugu zangu Wakazi wa Ileje kwa itikadi zenu nyote, Nimeisoma na kuilewa vema ibara ya 67 ib ara ndogo ya (1-13) ya katiba ya JMT 1997, ambayo pamoja na mambo mengine inaeleza SIFA,
     HAKI NA WAJIBU WA MBUNGE.Na kwa tafsiri ya jumla (yangu)ya Ibara hii inaonesha ushiriki wa Wananchi katika kumtathimini na kumpa majukumu mtu yeyote miongoni mwao kuwa Mbunge au mwakilishi kwa kuzingatia sifa tajwa. Ndugu zangu, binafsi nimejitathimini na kuja kuwashirikisha jambo na kuhitaji Baraka zenu kuwa ninao uwezo wa kuwa MBUNGE WA JIMBO LA ILEJE kwa kutimizi vema Majukumu tajwa, na hivyo natangaza kwenu rasimi kuwa nimetia nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ileje kwa ticket ya CHADEMA, na kwamba kwa kuheshimu taratibu na kila aina ya matokeo yatakayo tokea Mara baada ya kura ya maoni kufanyika ndani ya Chama changu nitaunga mkono kwa namna nitakayo weza mabadiliko wanayohitaji Wanachi wa Ileje kwa muda mrefu sasa.

Natambua majukumu ya nafasi ninayo omba ikiwa ntapitishwa na chama changu ni pamoja.
1.Kutunga sheria
2.Kuwakilisha Wanachi
3.Kuisimamia Serikali.
  Katika majukumu hayo, hakuna sehemu inayo onesha kuwa Mbunge ni MFADHIRI ama vinginevyo kama anavyo tafsiliwi kwa RAIA wa kawaida ama kwa kuto fahamu au maksudi. CHADEMA ,tumeonesha uwezo wa kutekeleza majukumu madogo mlio tupa kupitia kwa viongozi wa serikali za mitaa mlio wachagua katika uchaguzi wa 2014 na hivyo tumieni historia hii kutuunga ama kuto tuunga mkono kwa mgombea yeyote atakaye pendekezwa miongoni mwetu Wanachadema /Ukawa kuwania Ubunge katika jimbo hili na Mimi ni miongoni mwao.

Ndugu zangu, Kila mwananchi anawajibika kwa Taifa hili; hapa tulipofika kama Taifa si kwa sababu ya watu waovu na wala rushwa, bali ni kwa sababu ya watu waadilifu na wenye hekima waliokaa pembeni na kuangalia kinachofanywa na watu waovu; Wanatumia muda mwingi kulaani giza badala ya kuwasha taa, na mtambue Kuwa serikali mbovu huchaguliwa na wasio piga kura.
Hivyo nina wasihi kuwa tujitokeze kwa wingi wakati wa kupiga muda utakapo fika ili kupata viongozi wanao tokana na matakwa yetu wenyewe na si vinginivyo. Ambapo bila kufanya hivyo tutakua tunajitakia Umasikini wenyewe.

Na ,tunaomba ifahamike kuwa CHADEMA/UKAWA hatuombi ridhaa ya miaka 50 mlio toa kwa CCM bali tunaomba ridhaa ya miaka 5 tu ambapo kupitia miaka hii mtatumia historia na kutathimini ikiwa tunafaa ama hatufai kuongezwa muda zaidi wa kutekeleza majukumu mlio tupa. Mungu awabariki na awa ongoze kupata kiongozi atakaye iunganisha Ileje,2015 na Asanteni kwa kunisikiliza"

Sunday, June 21, 2015

Mkutano mkuu wa ACT mkoa wa mbeya ktk viwanja vya rwanda nzovwe.

       Mkutano ulihutubiwa na kiongozi wa chama cha Wazalendo ACT  katika viwanja vya Nzovwe mbeya huku Mh Zito Kabwe akiahidi kuwa (Pesa zangu za halali za kiinua mgongo za ubunge zote ntazipereke shule ya walemavu wa ngozi.albino SHINYANGA.) alisema Zitto Kabwe





Saturday, June 20, 2015

MATUKIO KATIKA PICHA : MA ELFU WAMPOKEA LOWASA MBEYA JANA APATA WADHAMIMI 53,156 SHUHUDIA.



Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wakiwa wamemzunguka, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati), wakati alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya jana Juni 19, 2015, kukabidhiwa fomu zitakazomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mbeya wamevunja rekodi udhamini kwa Mh. Lowassa ya mikoa yote aliyopita, amepata wadhamini 53,156 kwa mkoa wa Mbeya pekee.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipunga mkono kwa Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, wakati alipowasili kwenye Ofisi hizo leo Juni 19, 2015, tayari kwa kupokea fomu za WanaCCM 53,156 wanaliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, leo Juni 19, 2015.
Furaha ya Mh. Edward Lowassa kwa wanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, hata haikujificha pale alipata mapokezi makubwa ambayo hata yeye hakuyategemea.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu tisa wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mary Kalinze.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM wa Wilaya ya Mbeya Vijijini, kwenye mji Mdogo wa Mbalizi wakati aliposimama kuwasalimia.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Kijana Mwenye ulemavu, Ernest Mhagama aliekuja kumpokea katika Uwanja wa Ndege Songwe, Jijini Mbeya jana Juni 19, 2015.


 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akitoka nje ya Uwanja wa Ndege wa Songwe na kulakiwa na umati wa WanaCCM wa Mkoa wa Mbeya.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungia wanaCCM wa Mkoa wa Mbeya.
 Shangwe kwa wanaCCM wa Mji wa Mbalizi, Mbeya Vijijini.
 Mh. Lowassa akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini.
 Umati wa wanaCCM wa Mji wa Mbalizi jijini Mbeya.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu tisa wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mary Kalinze.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM wa Wilaya ya Mbeya Vijijini, kwenye mji Mdogo wa Mbalizi wakati aliposimama kuwasalimia.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Mbalizi jijini Mbeya waliojitokeza kumlaki.

Thursday, June 18, 2015

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe AHUKUMIWA Jela Mwaka Mmoja au kulipa faini ya Sh milioni moja.


MAHAKAMA ya wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, imemtia hatiani na kumhukumu Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh milioni moja, kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumshambulia mwangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
 
Akisoma hukumu hiyo iliyohudhuriwa na wabunge wengi wa Chadema, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Denis Mpelembwa, alisema mahakama imemkuta Mbowe na hatia, hivyo kutakiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini kiasi cha Sh milioni moja.
 
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, katika kesi hiyo ya jinai namba 73 ya mwaka 2011, alidaiwa kumshambulia Nassir Yamin, katika Kijiji cha Nshara, kata ya Machame Kaskazini, Wilaya ya Hai, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. 
 
Mpelembwa alisema mahakamani hapo kuwa hukumu iliyotolewa mahakamani hapo imezingatia ushahidi uliotolewa kwa upande wa mlalamikaji Nassir Yamini.
 
Kwa upande wake, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe akizungumza mahakamani hapo, alisema hukumu iliyosomwa mahakamani hapo haijamtendea haki.
 
Alisema kesi yake hiyo haikustahili kuchukua muda mrefu kama mahakama ilivyofanya kwa kuchukua zaidi ya miaka mitano bila kusomewa hukumu.
 
Hata hivyo, Mbowe amelipa kiasi cha fedha Sh milioni moja alichotakiwa kulipa kama hukumu ilivyoeleza, kwa kumtaka kulipa kiasi hicho cha fedha au kwenda jela mwaka mmoja.

Sunday, June 14, 2015

Mafuriko Ya Lowassa Yatua Kigoma......Azoa Wadhamini 11,250

Umati wa WanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma, kuja kumuona Mh. Edward Lowassa (anaeonekana kule mbele) wakati alipofika kuomba udhamini wa wanachama wa CCM, ili aweze kupata ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
 
 Mh. Lowassa alipata udhaminiwa na wanaCCM 11,250 wa Mkoa wa Kigoma, jana Juni 13, 2015.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC), Daniel Nsanzugwanko (kulia) amkabidhi Mtangaza nia, Majina ya wanaCCM  waliomdhani.
Umati wa WanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma, kuja kumuona Mh. Edward Lowassa (anaeonekana kule mbele) wakati alipofika kuomba udhamini wa wanachama wa CCM, ili aweze kupata ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
 
 Mh. Lowassa alipata udhaminiwa na wanaCCM 11,250 wa Mkoa wa Kigoma, jana Juni 13, 2015.
Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM wa Mkoa wa Kigoma.