Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya uchumi nchini
Profesa Ibrahimu Lipumba amesema anaunga mkono mpango wa serikali wa
miaka mitano huku akisema ni vema serikali ihakikishe inawekeza zaidi
katika nishati ya umeme ili kufikia lengo la kuwa nchi ya viwanda.
Wakati tayari mpango wa serikali ukiwa umekwishawasilishwa kwa miaka
mitano ijayo, ambapo umeanisha namna utakavyofanikisha asilimia 40 ya
ajira ifikapo mwaka 2020 zikitokana na viwanda, huku miongoni mwa miradi
mikubwa uinayotarajiwa kutekelezwa ya viwanda ni ujenzi wa kiwanda cha
chuma.
Aidha Mchumi huyo pia amesema adhima ya serikali ya kujenga nchi ya
viwanda itafanikia ikiwa itawekeza katika nishati ya umeme wa uhakika,
licha ya miradi mikubwa kama ya Power Afrika na MCC kusitishwa huku
akiishauri serikali kufanyia kazi maazimio ya bunge kuhusu sakata la
Tegeta esrow.
Mahojiano hayo maalum yamefanyika Dar es Salaam, muda mfupi baada ya
Prof Lipumba kupokea ujumbe maalum wa wawafuasi wa chama cha CUF kutoka
mjini bagamoyo waliokuwa lengo la msihi kurejea kwenye nafasi yake ya
uenyekiti wa chama cha CUF.
VITUS MTAFYA
..... ILEJE NI NYUMBANI ......