Rais mstaafu wa Awamu ya Pili,
Ali Hassan Mwinyi ameishauri Kampuni inayoendesha Mradi wa Mabasi
Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart) kuongeza mabasi ya wanafunzi na
mengine ya wazi juu ya watalii wanaoitembelea nchini ili waweze
kuangalia mandhari ya jijini Dar es Salaam.
Rais Mwinyi alitoa ushauri huo jana
alipotembelea mradi huo akiwa na mkewe, Sitti Mwinyi na kupokewa na
Kaimu Mtendaji mkuu wake, Ronald Lwakatale, Mtendaji wa kampuni
inayoendesha mradi huo, David Mgwassa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Ally Hapi.
Mwinyi alikata tiketi katika Kituo cha Morocco na kupanda
gari kwenda Kariakoo, Gerezani kisha Kivukoni.
Alipofika katika kituo
hicho alikutana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtendani na kuzungumza
nao kwa kifupi kisha kuwaeleza ushauri huo alioutoa kwa Udart.
“Nimekuja
kupata maarifa na kuona mabasi yetu mapya yanavyofanya kazi kuhudumia
wana Dar es Salaam.
"Wakati nipo kwenye basi nimeteta na viongozi
nikiwashauri kama kuna uwezekanao wa kuwa na basi moja au mawili ya wazi
ambayo unaweza kupanda juu ili kuona mazingira ya jiji vizuri,” alisema
Mwinyi,
Alisema magari hayo ya wazi yatawasaidia watalii kulitazama
jiji vizuri, lakini pia wanafunzi kujionea mandhari yake na kujifunza.
Mtendaji wa Udart, David Mgwassa alisema elimu imeanza kuwaingia
wananchi kwani usumbufu na ajali hakuna na kwamba wiki ijayo matumizi ya
kadi yataanza baada ya hatua za awali kukamilika na kubakia vitu
vichache.
VITUS MTAFYA
..... ILEJE NI NYUMBANI ......