VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Monday, November 17, 2014

Wito kwa wakazi kujihami dhidi ya Boko:H

Emir Sanusi alikuwa gavana wa benki kuu ya Nigeria kabla ya kuteuliwa kama Emir Kaskazini mwa Nigeria

Emir wa Kaskazini mwa Nigeria, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kiisilmau wenye ushawishi mkubwa, ametoa wito kwa watu nchini humo kuchukua silaha na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa kiisilamu wa Boko Haram.
Emir huyo wa Kano, Muhammad Sanusi, amewaambia wakazi wasisubiri wanajeshi kuwalinda kutokana na magaidi.
Emir huyo ambaye alikuwa gavana wa benki kuu nchini humo kabla ya kuchukua wadhifa wake wa Emir, alitoa matamshi yake ya kutatanisha kwenye mkutano wa maombi.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kauli kama hii sio kawaida kutolewa kwani Emir huyo huyo hazungumzii sana maswala ya kisiasa.
Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mitano sasa
Wapiganaji wa wa Boko Haram wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika sehemu kadhaa za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku wakiteka miji na mijiji ambko wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria kali ya kiisilamu.
Sanusi alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali alipokuwa anafanya kazi yake ya benki, alisema kuwa watu hawapaswi kuogopa wanamgambo hao na kwamba wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.
Mwandishi wa BBC anasema ingawa Emir huyo hakutaka kundi la Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee kwa kiongozi kama huyo kuwataka watu kujihami dhidi ya Boko Haram.
Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria


Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mitano sasa

         

        wapiganaji wa wa Boko Haram wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika sehemu kadhaa za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku wakiteka miji na mijiji ambko wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria kali ya kiisilamu.
Sanusi alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali alipokuwa anafanya kazi yake ya benki, alisema kuwa watu hawapaswi kuogopa wanamgambo hao na kwamba wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.
Mwandishi wa BBC anasema ingawa Emir huyo hakutaka kundi la Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee kwa kiongozi kama huyo kuwataka watu kujihami dhidi ya Boko Haram.
Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

HATARI!! Diamond aamua kuwapa ''makavu live'' team Wema baada ya wao kumdiss. HATARI!! Diamond aamua kuwapa ''makavu live'' team Wema baada ya wao kumdiss.

Baada ya mashabiki wa mwanadada Wema "kumjia juu mwanamuziki Diamond Platnumz" kuhusu tuhuma za yeye kumtumia mwanadada huyu kimwili zaidi bila kumuendeleza, hatimaye raisi huyu wa kundi la WCB ameamua nay eye kufunguka haya mazito juu ya kauli hizo. Kupitia ukurasa wake wa mtandao ule maarufu wa kijamii Diamond ameandika haya..

“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu... kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe...
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng'ombe wake Kwenye Maji safi....ila yeye ng'ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!... leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeeeew!




Msako mkali dhidi ya misikiti Mombasa

Msako mkali dhidi ya misikiti Mombasa

Polisi nchini Kenya wamefanya msako mkali dhidi ya misikiti inayotoa mafunzo ya itikadi kali za kidini mjini Mombasa pwani ya Kenya.

Mtu mmoja ameuawa kwenye msako huo ulioanzishwa Jumapili dhidi ya misikiti inayosemekana kutoa mafunzo ya kuunga mkono harakati za kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia.
 Misikiti ya kwanza kulengwa katika msako huo ni ile ya Masjid Musa na Sakina.

Mkuu wa polisi mjini Mombasa alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa walipata taarifa kwamba kundi hilo limekuwa likipanga kufanya mashambulizi na hiyo ndiyo sababu ya msako huo kuanzishwa.

Sunday, November 16, 2014

Matokeo ya michuano ya dimba la Afrika

Mchezaji wa Ivory Coast Gervinho 


Mabingwa watetezi wa kombe la Afrika Nigeria wameicharaza Congo Brazaville 2-0 siku ya jumamosi ili kuimarisha matumaini yake ya kufuzu katika dimba la Afrika mwaka 2015 huku Afrika kusini na Cameroon zikifuzu katika kinya'nganyiro hicho.
Afrika kusini iliichapa Sudan 2-1 katika mechi yao ya kwanza tangu kuuawa kwa mlinda lango wake Senzo Meyiwa ili kuongoza kundi la Da.
Zambia nayo iliinyamazisha Mozambique 1-0 mjini Moputo kufuzu na katika kundi Fa pamoja na viongozi wa kundi hilo Cape Verde.
Burkina Faso na Gabon pia zilifuzu katika kundi Cha baada ya Kuishinda Lesotho 1-0 mjini Maseru huku Angola ikipata sare ya bila kwa bila dhidi ya wenyeji wake mjini Luanda.
 

Saturday, November 15, 2014

Kura dhidi ya waziri mkuu yapigwa Somali


  • Aliyekuwa rais wa Somali kushoto na waziri mkuu wa sasa nchini Abdiweli Sheikh Ahmed
Aliyekuwa rais wa Somali kushoto na waziri mkuu wa sasa nchini Abdiweli Sheikh Ahmed
Wabunge nchini Somalia wanapiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed.
Shughuli za bunge zimekwama kutokana na tofauti zilizopo kati ya waziri kuu na rais wa Somalia Hassan Sheik Mohamud.
Wadadisi wanasema kuwa hali imedhoofika kutokana na mizozo ya kisiasa.
Marekani inasema kuwa kura hiyo ya kutokuwa na imani haiwakilishi maslahi ya raia.

Wednesday, November 12, 2014

Wanasayansi wajawa na shauku ya kimondo

      Wanasanyansi wa safari za anga za mbali wamejawa na shauku ya kutaka thibitisho kwamba Chombo kilichopelekwa na kutua kwenye kimondo au nyota mkia yaani Comet iliyo umbali wa zaidi ya kilometa nusu bilioni kutoka duniani.
Hapo jana Chombo hicho kiliwezesha kuwekwa kwa historia ya kuwa kifaa cha kwanza kuwahi kutengenezwa na binadamu kutua kwenye kimondo, kazi iliyochukua zaidi ya miaka 10.
Hata hivyo huenda bado kifaa hicho hakijajibanza kwenye kimondo hicho chenye upana wa kilometa mbili , kama ilivyotarajiwa-Data mpya na hasa picha zinasubiriwa kwa hamu kubwa.

Tuesday, November 11, 2014

MSF: MBINU MPYA ZAHITAJIKA KUKABILI EBOLA

Mbinu mpya mbalimbali zinahitajika kwa ajili ya kupambana na virusi vya Ebola nchini Liberia, shirika la madaktari wasio na mipaka, MSF limeeleza.

Zaidi ya Watu 6,000 wameathiriwa na ugonjwa huo nchini Liberia lakini takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya maambulizi mapya imeendelea kupungua.



MSF imesema kuwa imekuwa na uwezo mkubwa wa kuwa na vituo vingi vya kupambana na maradhi hayo kuliko idadi ya wagonjwa.
Mfano kituo kimoja mjini Monrovia kilikua na vitanda 250 lakini kimekua kikitibu wagonjwa 50 pekee, hivyo shirika hilo limeomba kubadilishwa kwa mbinu za mapambano dhidi ya ebola
Liberia ni nchi iliyoathirika zaidi na ugonjwa wa 

Ebola kwa karibu ya nusu ya idadi ya walioathiriwa wa ugonjwa huo Afrika magharibi.
Hivi sasa kiasi cha maambukizi kinaendelea kuwa juu nchini Guinea na Sierra Leone