VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Saturday, January 10, 2015

HOT NEWS: SAJENTI WA POLISI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI NDANI YA KITUO CHA POLISI USIKU WA MANANE


Sajenti Patrick Kondwa(54) anayedaiwa kujiua kwa kujipiga risasi ndani ya kituo cha Polisi Vwawa Mboz
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Kota za Polisi Vwawa nyumbani kwa marehemu Sajent Patrick leo mchana




Habari kamili juu ya tukio zima la kujiua kwa Sajenti Patrick Kongwa zitakujia hapa hapa...Fuatilia

Picha zote kwa Hisani ya Mkwinda Blog

Friday, January 9, 2015

WATOTO CHINI YA MIAKA 5 HUFARIKI NDANI YA SAA 100

 

 
Theluthi ya watoto chini ya miaka 5 hufa ndani ya saa 100 za uhai.
Huduma bora wakati wa kuzaliwa iliwekwa kipaumbele na Tanzania  ili kuokoa mama na vichanga 18,000, ifikapo Desemba 2014. 

Kila siku wanawake 21 na watoto wachanga 136 wa Tanzania wanapoteza maisha kipindi cha kujifungua.

Tuesday, January 6, 2015

KINANA AWASHUKURU WATANZANIA KWA KUICHAGUA CCM KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


  • Mkutano wake waweka historia
  • Atoa salaam za mwaka na kusema Chama kitashughulika na maadili ya viongozi mwaka 2015
  • Asisitiza viongozi kutembelea wananchi na kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa mikutano Tangamano ambapo aliwashukuru wananchi walioichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo Tanga ilichukua nafasi ya pili kwa kupata ushindi wa asilimia 97.
 Wananchi wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyekuja kuwashukuru kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
 Baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa kushukuru wananchi kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa January Makamba,Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Abdalah Kigoda na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mheshimiwa Mboni Mgaza.
 Wananchi wakifuatilia picha za matukio ya mkutano wa kuwashukuru wananchi.


 Mzee Yusuf akiwasalimu wakazi wa Tanga mjini ambapo anatazamiwa kutumbiza jioni ya leo kwenye uwanja wa Mkwakwani ikiwa kama ahadi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyoitoa wakati wa ziara yake ya mkoa wa Tanga mwishoni mwa mwaka 2014.
 Wananchi wakiwa wamefurika uwanjani Tangamano kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa kuwashukuru wananchi hao kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi Desemba 2014.
 Umati wa watu
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akitoa salaam na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa Tangamano, Tanga mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye mkutano wa kuwashukuru wananchi walioichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 2014 nchi nzima ambapo mkoa wa Tanga umekuwa wa pili kwa kushinda kwa asilimia 97.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano ambapo alitoa salaam za mwaka huuambapo alisema CCM mwaka huu itaweka mkazo kwenye maadili ya Viongozi.
 Katibu Mkuu wa CCM akisisitiza jambo wakati wa kuwahutubia wananchi wa Tanga mjini




 Wananchi wakionekana kuhamasika na hotuba ya Kinana.


 Mnenguaji wa Jahazi Modern Taarab akiwapa mikono baadhi ya viongozi wakati wa kutoa bashraf kabla ya kuwatumbuiza wananchi jioni ya leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Mbaraka Saad Mbaraka akitangaza kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara mbale ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Tangamano.
 Hassan Omary Mbaraka aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia CHADEMA mwaka  2010 akitangaza kujiunga na CCM baada ya kumsikiliza kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Tangamano.



 Wananchi wa Tanga mjini wakimpa mkono wa kumuga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kuwashukuru Watanzania kwa kuichagua CCM na kuwashukuru kwa imani yao kwa kutambua chama kinaweza kuongoza.

KAMERA YETU MITAA YA SIDO NA KABWE , VUMBI IMEBAKI HISTORIA.


PICHA NA MBEYA YETU BLOG

U Heard ya leo Jan. 06 iko hapa, inahusu Sitti Mtemvu na Wema Sepetu


wema sepetu 2006
Wema Sepetu alipovalishwa Taji la Miss Tanzania 2006.
Soudy Brown leo katuletea U Heard inayowahusu Wema Sepetu na Sitti Mtemvu ambao waliwahi kuvaa Taji la Miss Tanzania kwa nyakati tofauti.
Soudy amewalinganisha Wema na Sitti kwamba, wakati ambao Wema alishinda Taji hilo kulikuwa na story kwamba ameongopa umri kwa kujiongeza miaka miwili huku Sitti kukiwa na story ya kupunguza umri miaka miwili pia story ya kwamba wote walikuwa wanene.
IMG_6871
Sitti Mtemvu baada ya kuvishwa Taji la Miss Tanzania 2014.
Kuhusiana na Sitti kujivua Taji, Wema amesema kama ingekuwa ni yeye asingevua taji kutokana na mambo ambayo yalikuwa yakizungumzwa mitandaoni baada ya kuvishwa Taji hilo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu

Monday, January 5, 2015

Air Asia:Miili 37 imepatikana mpaka sasa


Shirika la uokoaji nchini Indonesia limesema hivi sasa miili 37 imepatikana kutoka kwenye bahari ya Java ambapo ndege ya Air Asia iliangukia mwishoni mwa juma lililopita.
Helikopta na Meli za kijeshi zimekuwa zikifanya doria katika eneo la bahari hiyo ambapo vitu vinavyoelezwa kuwa mabaki ya ndege vimeonekana.hali ya hewa ya eneo hilo kwa sasa imetengemaa ingawa bado mikondo ya bahari ina nguvu.
Vikosi vya wapiga mbizi wa Indonesia na Urusi vina matumaini ya kupata vifaa vya kurekodia mawasiliano ndani ya ndege, ambavyo vitasaidia kujua sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Surabaya kwenda Singapore.
Air Asia ilikuwa imebeba Watu 162 ilipopata ajali.

Mwili wa marehemu wazikwa na kuku tumboni


Pg 2
Na Kadama Malunde, Shinyanga

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa Benadetha Steven (35), aliyefariki dunia juzi umefanyiwa matambiko ya kimila baada ya kupasuliwa na wembe ukiwa kaburini na kuingiziwa kuku ndani ya tumbo lake ikiwa ni ishara ya kuondoa mkosi.


Tukio hilo lilitokea juzi katika Mtaa wa Mapinduzi wakati waombolezaji wakiwa hatua ya mwisho ya kumzika marehemu.


Lakini ghafla alijitokeza ndugu wa marehemu mwanamke kuwazuia waombolezaji, huku mwenyewe akiingia kaburini na kufungua sanduku na kuanza kuchana tumbo la marehemu aliyekuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na uvimbe tumboni.


Mashuhuda wa tukio hilo, walisema mwanamke huyo ambaye hakutaka kujitambulisha jina kabila la Mkurya, aliupasua mwili wa marehemu kwa kutumia wembe kisha kuchinja kifaranga cha kuku na kuumwagia damu baadaye kufunika jeneza na kuruhusu maziko.


Walisema kabla ya tukio hilo, kulitokea mabishano kati ya waombolezaji na ndugu wakitaka matambiko hayo yafanyike Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga alikokuwa akitibiwa.


“Mgogoro ulianzia nyumbani hata kabla ya kwenda makaburini, wakati mazishi yanaendelea ndipo ndugu mmoja wa marehemu akaingia kaburini akiwa amevaa mipira ya mkononi (glovu), akiwa na wembe na boksi dogo lililokuwa na kifaranga cha kuku na kuzuia waombolezaji wasitupe udongo kaburini.


“Ndugu huyo wa marehemu mwenye jinsia ya kike, aliingia kaburini baada ya mchungaji kumaliza ibada ya mazishi na kuruhusu mwili wa marehemu ufukiwe ndipo akaanza kuuchana kwa wembe, akachinja kuku kisha kummwagia damu na kumwingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu, akafunika jeneza na ndugu wakaendelea na mazishi,” alieleza mmoja wa mashuhuda, Sijali Jumanne.


Jumanne alisema ndugu wa marehemu waliamua kufanya hivyo wakiamini wanaondoa mkosi ili kifo kama hicho kinachotokana na uvimbe tumboni kisitokee tena kwenye ukoo wao.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Mapinduzi, Ayubu Daniel, alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa baada ya tukio alitoa taarifa polisi ambapo ndugu hao wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.


Hata hivyo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ndala, Dickson Venance, alisema marehemu alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu na kwamba siku moja kabla ya mazishi kulikuwa na mgogoro juu ya mazishi ya mwanamke huyo ambaye aliolewa bila kulipiwa mahari.


“Kabla ya mazishi nilisuluhisha mgogoro, ndugu wa marehemu walikuwa wanataka mahari ya Sh milioni moja, kukawa na mvutano, wakakubaliana Sh 100,000, ndugu wa mwanaume wakachangishana wakakubaliana kuzika, sikuwepo wakati wa mazishi lakini nashangaa leo yamekuwa hayo,” alisema.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, amethibitisha tukio hilo na kusema uchunguzi unafanyika.

Chanzo. Gazeti Mtanzania