VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Wednesday, June 10, 2015

Lowassa Apata Wakati Mgumu Mkoani Mara Ambako ni Nyumbani kwa Wassira........ Maelfu ya Wananchi Wazuia Msafara Wake Wakitaka Wamuone



Waziri mkuu wa zamani Mh.Edward Lowasa aliyeko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini amepata wakati  mgumu alipowasili mkoani Mara baada ya makundi ya wananchi wakiwemo vijana,wanawake na watoto   kumfuata kila alikokwenda wakitaka wapewe nafasi ya kumueleza kero zao jambo lililosababisha  zoezi la kumdhamini kuwa gumu licha ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 
Heka heka za wananchi kutaka kuzuia msafara wa Mh.Lowasa zilianza mapema asubuhi wakati  anawasili kwenye uwanja wa ndege wa musoma ambapo vijana walizuia msafara wake kutoka kwenye  uwanja huo wakitaka wapewe nafasi ya kuonana naye.

Baada ya waratibu wa msafara huo kufanya kazi ya ziada ya kufanikiwa kutatua changamoto hiyo Mh.Lowasa aliekea katika wilaya ya Bunda na licha ya kusimamishwa na wananchi njiani hali  ilikuwa ngumu zaidi katika ofisi ya CCM wilaya ya  hiyo kutokana na watu kujitokeza kwa wingi.

Hata hivyo pamoja na maelfu ya wananchi hao wanaounga mkono safari ya matumaiani kuwa na shauku ya kumueleza Mh.Lowasa shida zao alishindwa kuwasikiliza  kutokana na kubanwa na kanuni   na aliwaomba kuwa watulivu na kuendelea kuiombea kheri safari ya matumaini.

Mh.Lowasa akiwa katika mkoa wa Mara  amepata idadi kubwa ya wadhaamini pia amefika  nyumbani kwa hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere na kupewa  baraka,  kisha kuweka shada la maua kwenye kaburi na pia  ametembelea wilaya ya Tarime na Musoma.

Mh.Lowassa ambaye ameshatembelea mikoa ya Mwanza Geita,Zanzibar na Pemba anaendelea na ziara yake ya kutafuta wadhamini katika mkoa wa Simiyu.  
 Maelfu  ya  Wananchi  wakiwa  wameuzuia  Msafara  wa  Lowassa  wakishinikiza  kumuona, hali  iliyowalazimu Polisi  na waratibu  wa  msafara  ya  kutumia  njia  mbadala  kutatua  changamoto  hiyo
Mh. Lowassa  alipotembelea  Kaburi  la  Baba  wa  Taifa, Hayati Mwl. J.K. Nyerere

Monday, June 8, 2015

Polisi Iringa yakamata DVD za Mafunzo ya kigaidi



Jeshi la polisi mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo ya kijeshi yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al shaabab cha nchini Somalia zilizokuwa zikitumika na watoto wa mitaani wanaodaiwa kuwa walikuwa wakichukua mafunzo kwakutumia DVD hizo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari akieleza kuwa mikanda hiyo iliyokuwa ikitumiwa na vijana hao wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16 inaonesha ukatili na mauaji yanayodaiwa kufanywa na kikundi cha kigaidi cha Al shaabab.Mikanda hiyo walikuwa wakiitazama kwa kutumia kompyuta mpakato yaani laptop.

Aidha kamanda Mungi amesema pamoja na mikanda hiyo ya DVD pia jeshi hilo limekamata watu wawili wanaojihusisha na biashara ya bangi wakiwa na magunia matatu ya bangi katika harakati za kufunga bangi hiyo kwenye vifurushi vidogo tayari kuisambaza kwa wateja wao.

Mungi ameongeza kuwa kamata kamata hiyo iliyofanywa na jeshi hilo mkoa wa Iringa pia imekamata nguzo 35 za umeme za shirika la umeme nchini TANESCO, nyaya za kusambaza umeme na vifaa vingine zikiwa zimehifadhiwa kwa watu binafsi wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za kiupelelezi.

MWANZA: Meya Matata ajiengua Chadema, Arejea CCM



HATIMAYE Meya wa Halmashauri ya Ilemela jijini Mwanza, Henry Matata, amejiengua ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uamuzi aliufanya juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Minazi Mitatu Kata ya Kitangiri Manispaa ya Ilemela ambako alikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu na kupewa ya CCM.

Akizungumza baada ya kurudisha kadi ya Chadema, Matata alisema kabla ya kujiunga na upinzani alikuwa ndani ya chama hicho tangu utotoni  lakini baada ya CCM kumfanyia mizengwe kwa kuweka jina lake nafasi ya nne katika kura za maoni kwenye uchaguzi wa  mwaka 2010, aliamua alikimbilia Chadema.
 
Alisema alipokimbilia Chadema alipokelewa kwa shangwe kwa sababu alikuwa anakubalika kwa wananchi na kumpa nafasi ya kuwania udiwani na kushinda Kata ya Kitangiri.

Alisema  baada ya kuanza kutekeleza majukumu ya udiwani  ndani ya upinzani alijikita kutekeleza ilani ya CCM ndipo alipoanza kuchukiwa.

“Mimi damu yangu ilikuwa CCM ingawa nilikuwa Chadema, baada ya kushinda udiwani nikaanza kupigania nafasi ya umeya kwa bahati nzuri nikapata.

“Sasa ukishakuwa meya lazima utekeleze ilani ya CCM kwa sababu ndiyo chama tawala… wenzangu wakaanza kunichukia na kuniundia zengwe kama ilivyokuwa awali CCM.

 “Ikafika wakati nikavuliwa uanachama nikabaki diwani wa mahakama- lakini sikupoteza chochote kwa sababu  stahili zangu zote nilipata,” alisema.

Tuesday, June 2, 2015

Pigo jingine: Mbunge Eugene afariki Dunia, bunge lahairishwa


Mbunge wa jimbo la Ukonga Dar es Salaam kupitia tiketi ya (CCM) Eugen Mwaiposa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini nyumbani kwake Dodoma.

Kwa mujibu wa Naibu Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai ambaye amelitangazia bunge leo majira ya saa 7 mchana, marehemu Mwaiposa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu.

Ndugai amesema kuwa kwa sasa msiba upo nyumbani kwake eneo la Chadulu Dodoma ambapo pia familia yake inasubiria hapo kwa ajili ya kuaga mwili wake shughuli ambayo itafanyika kesho (Jumatano).

Bunge limeahirishwa hadi keshokutwa saa 3 Asubuhi.

Mungu ametoa Mungu ametwaa jina lake lihimidiwe. R.I.P ‪

Saturday, May 30, 2015

MATUKIO MBALIMBALI YA MKUTANO WA CHADEMA ULIOFANYIKA KATA YA MTULA WILAYANI ILEJE MKOANI MBEYA

LENGO KUU LA MKUTANO HUO NI KUHAMASISHA BVR
katibu vijana chadema mkoani mbeya akiwa katika meza kuu iliyo andaliwa na wanchi na viongozi wa chadema kata ya mtula kijiji cha lubanda wakitafakali moja baada ya jingine


 kikundi cha ngoma za kindali kikitumbwiza .

PICHA ZAIDI 
^

































Shukran za dhati kwa mr Gwamaka Mbugh