VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Thursday, July 28, 2016

Al-Shabab Washambulia Mtambo wa Mawasiliano Kenya



Washukiwa wa kundi la Al-Shabaab mapema leo Alhamisi wameshambulia na kulipua mtambo wa mawasiliano ulioko katika mji wa Fino, Lafey katika kaunti ndogo ya Mandera nchini Kenya.

Afisa mkuu wa Polisi huko Lafey, Bosita Omukolongolo, amesema kuwa kisa hicho kilitokea saa nane usiku.

Afisa huyo wa Polisi anasema kuwa walikabiliana vikali na wanamgambo hao, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa upande wa polisi waliokuwa wakiulinda mlingoti huo wenye vifaa vya kupeperusha mawasiliano.

Kundi la Al- Shaabab, ambalo lina makao yake nchini Somalia, limehusika na mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na mauaji nchini Kenya na mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki na upembe wa Afrika.
VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Saturday, June 11, 2016

Mwanza: Kijana Awafungia ndugu zake Ndani na Kuchoma Moto Nyumba




Nyumba moja iliyopo mtaa wa Kiseke wilayani Ilemela mkoani Mwanza imeteketea kwa moto leo asubuhi na kuunguza vitu vingi huku wakazi wa nyumba hiyo wakinusurika. 

Taarifa zinaarifu kuwa,  nyumba hiyo imewaka moto baada ya mmoja wa watoto wa familia hiyo kuamka asubuhi na kumwaga mafuta ya taa katika moja ya chumba cha nyumba hiyo na kisha kuwasha moto.

Imeelezwa kuwa,  kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili amekuwa akiwatishia kwa muda mrefu kuwachoma moto lakini wamekuwa wakimpuuza kutokana na matatizo yake ya akili.

Baada ya kumwaga mafuta  na kuwasha moto,  kijana huyo alitoweka na kuwafungia ndugu wengine ndani ambapo majirani walifanikiwa kuwahi kuwaokoa.VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Friday, June 10, 2016

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi Ataka Mabasi ya Mwendokasi Kwa Ajili ya wanafunzi Udart

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ameishauri Kampuni inayoendesha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart) kuongeza mabasi ya wanafunzi na mengine ya wazi juu ya watalii wanaoitembelea nchini ili waweze kuangalia mandhari ya jijini Dar es Salaam. 
Rais Mwinyi alitoa ushauri huo jana alipotembelea mradi huo akiwa na mkewe, Sitti Mwinyi na kupokewa na Kaimu Mtendaji mkuu wake, Ronald Lwakatale, Mtendaji wa kampuni inayoendesha mradi huo, David Mgwassa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi. 
Mwinyi alikata tiketi katika Kituo cha Morocco na kupanda gari kwenda Kariakoo, Gerezani kisha Kivukoni. 
Alipofika katika kituo hicho alikutana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtendani na kuzungumza nao kwa kifupi kisha kuwaeleza ushauri huo alioutoa kwa Udart. 
“Nimekuja kupata maarifa na kuona mabasi yetu mapya yanavyofanya kazi kuhudumia wana Dar es Salaam. 
"Wakati nipo kwenye basi nimeteta na viongozi nikiwashauri kama kuna uwezekanao wa kuwa na basi moja au mawili ya wazi ambayo unaweza kupanda juu ili kuona mazingira ya jiji vizuri,” alisema Mwinyi, 
Alisema magari hayo ya wazi yatawasaidia watalii kulitazama jiji vizuri, lakini pia wanafunzi kujionea mandhari yake na kujifunza.
Mtendaji wa Udart, David Mgwassa alisema elimu imeanza kuwaingia wananchi kwani usumbufu na ajali hakuna na kwamba wiki ijayo matumizi ya kadi yataanza baada ya hatua za awali kukamilika na kubakia vitu vichache.
VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Saturday, May 14, 2016

Mamia mkoani Mbeya wajitokeza kumzika Kinyambe


        Mamia ya watu wamejitokeza Ijumaa hii mkoani Mbeya 
  kwa ajili ya mazishi ya mchekeshaji maarufu nchini Tanzania kutoka katika Kundi la Vituko Show, Mohammed Abdallah ‘Kinyambe’ aliyefariki dunia Jumatano iliyopita akiwa katika hospitali ya Mbeya.
????????????????????????????????????
Mmoja kati ya wasanii wanaounda Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania, Mkono Mkonole, kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika:
Kila nafsi itaonja umahuti kwa heri kinyambe kila mwanadamu huu ndio mwisho wake pumzika kwa amani
Mkonole aliiambia Bongo5 Alhamisi hii, kuwa Kinyambe alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni mpaka anapatwa na umahuti akiwa nyumbani kwao Mbeya.
Mazishi yake yamehudhuriwa na wananchi, wadau wa filamu pamoja na wasanii wenzake wa filamu ambao walisafikiri kutoka Dar es salaam.


VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Monday, May 2, 2016

Prof. Lipumba Apongeza Mipango ya Rais Magufuli



Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya uchumi nchini Profesa Ibrahimu Lipumba amesema anaunga mkono mpango wa serikali wa miaka mitano huku akisema ni vema serikali ihakikishe inawekeza zaidi katika nishati ya umeme ili kufikia lengo la kuwa nchi ya viwanda.

Wakati tayari mpango wa serikali ukiwa umekwishawasilishwa kwa miaka mitano ijayo, ambapo umeanisha namna utakavyofanikisha asilimia 40 ya ajira ifikapo mwaka 2020 zikitokana na viwanda, huku miongoni mwa miradi mikubwa uinayotarajiwa kutekelezwa ya viwanda ni ujenzi wa kiwanda cha chuma.

Aidha Mchumi huyo pia amesema adhima ya serikali ya kujenga nchi ya viwanda itafanikia ikiwa itawekeza katika nishati ya umeme wa uhakika, licha ya miradi mikubwa kama ya Power Afrika na MCC kusitishwa huku akiishauri serikali kufanyia kazi maazimio ya bunge kuhusu sakata la Tegeta esrow.

Mahojiano hayo maalum yamefanyika Dar es Salaam, muda mfupi baada ya Prof Lipumba kupokea ujumbe maalum wa wawafuasi wa chama cha CUF kutoka mjini bagamoyo waliokuwa lengo la msihi kurejea kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama cha CUF.

VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......