Rais Magufuli alikuwa mjini Singida alikokuwa amekwenda kushiriki maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Hiyo
ni mara ya pili kwa askari kufariki wakiwa kwenye msafara wa Dk
Magufuli baada ya aliyekuwa akiongoza msafara wake wakati wa kampeni
kugongana na dereva bodaboda katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari
huyo alikuwa kwenye pikipiki maalumu iliyokuwa ikiongoza msafara wakati
Dk Magufuli akitoka katika Hospitali ya Lugalo kuaga mwili wa aliyekuwa
mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka alisema ajali hiyo
ilitokea saa 9.40 alasiri, katika Kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi
mkoani humo baada ya moja ya matairi ya gari hilo kupasuka na dereva
kushindwa kulimudu.
Aliwataja waliofariki kuwa ni Mkaguzi Mwajelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerard.
Waliojeruhiwa ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Singida (RCO), Peter Majira (50
na PC Charles Simon (34) ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
Gari
hilo lililopata ajali ni lile lililokuwa limetangulia ili kufagia
barabara kabla ya msafara wa Rais, likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani cha mkoa huo.
Sedoyeka alisema miili ya askari hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa huo.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Kitundu Jacks alisema hali
za majeruhi waliofikishwa kwenye hospitali hiyo zinaendelea vizuri.
“Mrope
ndiye aliyeletwa akiwa kwenye hali mbaya, alikuwa amevunjika mbavu na
mkono na akafa mara tu baada ya kufikishwa hospitalini hapa. Majeruhi
wengine wamepata michubuko na wanaendelea vizuri,” alisema.
No comments:
Post a Comment