VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Tuesday, November 11, 2014

BURIANI KWA RAIS MICHAEL SATA ZAMBIA

   
  Mazishi ya kitaifa yanafanyika nchini Zambia kumuaga hayati Rais wa nchi hiyo Michael Sata aliyefariki hospitalini mjini London Uingereza mwezi jana.
Sata alikuwa na umri wa miaka 77.
Katika wiki chache zilizopita, wanachi wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye mwili wake ulikuwa 
 umelazwa katika majengo ya bunge

 Mwili wa hayati Rais Michael Sata utazikwa leo mjini Lusaka Zambia


  Mazishi ya kitaifa yanafanyika nchini Zambia kumuaga hayati Rais wa nchi hiyo Michael Sata aliyefariki hospitalini mjini London Uingereza mwezi jana.
Sata alikuwa na umri wa miaka 77.
Katika wiki chache zilizopita, wanachi wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye mwili wake ulikuwa umelazwa katika majengo ya bunge.


Monday, November 10, 2014

MAPIGANO MAPYA YAZUKA SUDAN KUSINI

Vita vimekuwa vikiendeleea nchini Sudan kwa miezi 11 sasa huku maelfu wakiachwa bila makao


Mapigano mapya yamezuka katika majimbo matatu nchini Sudani kusini , siku chache baada ya pande mbili hasimu kukubaliana kumaliza mzozo ambao umekuwepo kwa miezi 11.

   Wiki iliyopita, Raisi wa Salva Kiir na Kiongozi wa waasi Riek Machar walikubaliana kumaliza mapigano kufuatia mazungumzo ya siku mbili nchini Ethiopia.

Serikali na Waasi wamekuwa wakinyoosheana kidole kuwa wamekuwa wakitekeleza mashambulizi katika jimbo la Upper Nile,Unity na Jonglei.

Msemaji wa Waasi Brigedia Jenerali Lul Ruai Koang ameishutumu Serikali kwa kuanzisha mashambulizi dhidi yao hasa katika maeneo yenye mafuta katika jimbo la Unity.

Lakini msemaji wa Jeshi Philip Aguer amesema vikosi vya waasi ndivyo vilivyoanzisha mapigano, kisha wao haraka wakajibu mashambulizi.

Mazungumzo yanayoratibiwa na jumuia ya IGAD,ambayo imetoa muda wa siku 15 kwa pande zote mbili kufikia makubaliano kumaliza mzozo.IGAD imetishia kuweka vikwazo ikiwemo marufuku ya kusafiri na usafirishaji wa silaha,ikiwa makubaliano hayatafikiwa kwa kipindi kilichotolewa.

Maelfu ya Watu wameuawa kwenye mapigano ya Sudani kusini na wengine milioni 1.8 wamekimbia mapigano tangu yalipoanza nchini humo katikati ya mwezi Desemba mwaka jana.


Saturday, November 8, 2014

TODAY




Bilionea Dangote azidi kung’ara.
     Mtandao wa Forbes umetoa list mpya ya matajiri hamsini kutoka Afrika list ambayo inaongozwa na tajiri wa Nigeria ambae ni Mfanya biashara maarufu na Rais wa kampuni ya Dangote Aliko Dangote, aliyekuwa akishikilia nafasi ya arobaini na tatu na kupanda...
Read More »




Stori 5 Hot Magazeti ya leo Tanzania November8, 2014

   MWANANCHI Wafanyakazi wapya katika hospitali ya taifa ya Muhimbili MNH wamelalamikia kutolipwa mishahara kwa miezi minne sasa huku uongozi ukishindwa kuwapa majibu ya ufumbuzi wa tatizo hilo. Wafanyakazi hao zaidi ya5o waliajiriwa na Hospitali hiyo tangu mwezi wa nane mwaka...
Read More »






Picha 15 za Usiku wa Damian Soul na watu wake ziko hapa….



  Usiku wa Nov 7 Damian Soul amezindua video ya single yake ‘Ni Penzi’ aliomshirikisha rapper kutokea Arusha (87.9CloudsFM) Joh Makini.Uzinduzi huo umefanyika katika ufukwe wa bahari Escape One uliopo Mikocheni Dar es Salaam.Katika uzinduzi huo Damian Soul alitumbuiza live bendi....

Tuesday, November 4, 2014

WASSIRA AITAHADHALISHA CCM UTEUZI WA WAGOMBEA



 Waziri wa nchi ,Ofisi ya Stephan Wassira , amekitaka chama cha ccm kutokufanya makosa  ya kusimamisha wagombea wasiokubalika  katika uchaguzi wa serikari za mitaa . alisema 2010 ccm ilifanya makosa katika  baadhi ya maeneo kwakusimamisha wagombea wasiokubalika  , hatua ambayo ilifanya baadhi ya majimbo hayo kuweza kuchukuliwa na vyama pinzani
      " naomba makosa ya mwaka 2010 yasiljirudie tena  kwa kuwachagua viongozi wasiyo kubalika na wananchi  Hali ambayo inaweza kusababisha kuvipa upenyo vyama pindani"

Monday, November 3, 2014

BUNGE KUWAKA MOTO DODOMA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda.
Stori: Mwandishi Wetu
Bunge la Jamhuri ya Muungano linatarajia kuwaka moto leo litakapoanza vikao vyake ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa.Tayari Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, imesema imepokea Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2014, unaopendekeza kuzifanyia marekebisho sheria 33, ambapo pia utawasilishwa katika vikao vyake.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Ngeleja alisema hivi karibuni jijini Dar kuwa kati ya sheria hizo 33, imo Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Sura Namba 370 inayopendekeza kuongeza wigo wa wanafunzi kupatiwa mikopo ya elimu ya juu.


“Ikumbukwe haya bado ni mapendekezo, lakini moja ya mapendelezo yaliyopo kwenye sheria hii ya mikopo ni pamoja na kuwajumuisha wanafunzi waliomaliza chuo cha sheria wanaokwenda shule ya sheria nao kupatiwa mikopo,” alisema Ngeleja.

Alisema pia muswada huo umejumuisha Sheria ya Mbegu sura namba 308 iliyoongezewa makali kwa kampuni ambazo zinasambaza mbegu kwa wakulima kuhakikisha zinasambaza mbegu zenye viwango vinginevyo adhabu kali iliyoongezwa ya faini ya kuanzia Shilingi milioni 100 hadi 500 itawakabili.


Alisema kwa sasa takriban Watanzania asilimia 75 wanaishi vijijini na wanajishughulisha na kilimo lakini wengi wao wamejikuta wakipata matatizo katika eneo la mbegu kutokana na sheria zilizopo kushindwa kuzibana kampuni zinazozalisha mbegu.
Sheria nyingine zilizopo kwenye muswada huo ni pamoja na Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa mazingira sura namba 272 na Sheria ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi sura namba 179.

Umeipata hii ya Mchungaji kukamatwa na dawa za kulevya za bil.2 Tanzania ?


dawaaa
Jeshi la Polisi kitengo cha Kupambana na Dawa za kulevya limekamata kilo40 za dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani ya shilingi bilioni2.

Tukio hilo lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambapo Polisi walifaniikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na mchungaji ambaye wakati huo alikua katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza.
Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitishia Gazeti la MTANZANIA kuwa  kuwepo kwa tukio hilo akiomba jina la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi.

“Ni kweli tukio la aina hiyo lipo  lakini watu kama hawa siwezi kusema moja kwa moja ni Mchungaji  ndio muhusika hadi nipate vithibitisho vya kutosha ikiwa kuendesha kanisa kwani wengi wao wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biashara hii,”Alisema Nzowa.
Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo ambapo wawili kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya kuweka hadharani ukweli wa mambo.