Vita vimekuwa vikiendeleea nchini Sudan kwa miezi 11 sasa huku maelfu wakiachwa bila makao
Mapigano
mapya yamezuka katika majimbo matatu nchini Sudani kusini , siku chache
baada ya pande mbili hasimu kukubaliana kumaliza mzozo ambao umekuwepo
kwa miezi 11.
Wiki iliyopita, Raisi wa Salva Kiir na Kiongozi wa waasi Riek Machar walikubaliana kumaliza mapigano kufuatia mazungumzo ya siku mbili nchini Ethiopia.
Serikali
na Waasi wamekuwa wakinyoosheana kidole kuwa wamekuwa wakitekeleza
mashambulizi katika jimbo la Upper Nile,Unity na Jonglei.
Msemaji
wa Waasi Brigedia Jenerali Lul Ruai Koang ameishutumu Serikali kwa
kuanzisha mashambulizi dhidi yao hasa katika maeneo yenye mafuta katika
jimbo la Unity.
Lakini msemaji wa Jeshi Philip Aguer amesema vikosi vya waasi ndivyo vilivyoanzisha mapigano, kisha wao haraka wakajibu mashambulizi.
Mazungumzo
yanayoratibiwa na jumuia ya IGAD,ambayo imetoa muda wa siku 15 kwa
pande zote mbili kufikia makubaliano kumaliza mzozo.IGAD imetishia
kuweka vikwazo ikiwemo marufuku ya kusafiri na usafirishaji wa
silaha,ikiwa makubaliano hayatafikiwa kwa kipindi kilichotolewa.
Maelfu
ya Watu wameuawa kwenye mapigano ya Sudani kusini na wengine milioni
1.8 wamekimbia mapigano tangu yalipoanza nchini humo katikati ya mwezi
Desemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment