Muda wa mwisho wa kufikia mwafaka
katika mazungumzo kati ya Iran na nchi sita tajiri zaidi duniani kuhusu
mpoango wake wa nuklia umeongezwa hadi Juni mwaka ujao.
Hii ni baada ya mazunguzo yanayoendelea mjini Vienna kukosa kufioka mwafaka uliotarajiwa.
Waziri
wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond kusema wamepiga hatua za
kuridhisha ingawa ni vigumu kufika mwafaka katika muda uliotarajiwa.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa China Wang Yi amasema kuwa anaamini mwishowe muafaka utapatikana.
Lakini taarifa kwenye mtandao wake ilisema kwa idadi kubwa ya masuala kadha ya kitaalamu yanatakiwa kuzungumziwa kwa undani.
Wapatanishi
wanasema kuwa kuna pengo kuhusu masuala ya kuiondolea vikwazo Iran ili
nayo iweze kuachana na mipango ya urutubishaji madini ya Uranium.
Kubwa
kwa yote hayo ni kwamba muda unayoyoma kwa viongozi wa dunia kufikia
mwafaka na Iran kuondoa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran
kuhusiana na mradi wake wa Nuklia.
Huku kukiwa na tofauti kati ya
mataifa, inaonekana mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna duru za
kidiplomasia zinasema kuwa yataakhirishwa hadi Disemba.
Iran
inashauriana na nchi nyingine sita zenye ushawishi zaidi dunaini ambazo
zilikuwa zimejipatia hadi mwishoni mwa leo kuwa na mwafaka.
Serikali ya Iran inasema kuwa inataka nishati ya nuklia kwa matumizi ya kawi ya atomiki wala sio kutengeza silaha za nuklia.
Marekani,
Urusi, China na Ufaransa, pamoja na Ujerumani, zinajaribu kufikia
mwafaka wa pamoja kuhusiana na mkataba uliofikiwa mjini Geneva mwaka
jana.
Mazungumzo ya ngazi ya juu yanaendelea kati ya waziri wa
mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, waziri wa mambo ya nje wa Marekani
John Kerry na mawaziri wa mataifa mengine matano.
Katika miezi
michache iliyopita, mazungumzo yamepunguza wasiwasi kuhusu vita vipya
mashariki ya kati na mawaziri watakuwa na wasiwasi kuondoka Vienna bila
ya kupata mwafaka.
No comments:
Post a Comment