Mahakama ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji wa M23.
Afisa anayedaiwa kupangiwa
njama za kuuawa ni Mamadou Ndala mabaye kwa kiasi kikubwa aliamini
katika vita dhidi ya kundi hilo la wapiganaji na ambaye aliuawa mwezi
januari mwaka huu. Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa nane
ambapo kati ya hao mmoja ndiye Kanali Ndala aliyehukumiwa kifo. Mahakama imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa akitumiwa na waasi wa ADF kutoka Uganda kuandaa maujaji.
No comments:
Post a Comment