VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Sunday, November 30, 2014

Chanjo ya EBOLA yatoa matumaini

Watafiti wa masuala ya afya nchini MAREKANI, wamesema, majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa EBOLA yaliyofanyika nchini humo, yanaonekana kuwa ya mafanikio.

Chanjo hiyo imetengenezwa ili kuchochoea kinga ya mwili wa binadamu ili itengeneze kinga dhidi ya virusi vya EBOLA. Watafiti hao wanasema chanjo hiyo imeonyesha mafaniko, kwa vile watu waliokubali kufanyiwa majaribio, miili yao imeweza kutengeneza kinga dhidi ya EBOLA katika kipindi cha wiki nne.

Utafiti huo unaonyesha kuwa watu waliofanyiwa majaribio ya chanjo dhidi ya EBOLA, hawakupata athari hasi za chanjo hiyo. Taasi inayoshughulika na chanjo hiyo, inatarajiwa kufanya majaribio zaidi kuhusiana na chanjo hiyo mwezi ujao.

Kajaribio ya awali ya chanjo hiyo yanatarajiwa kufanyika nchini LIBERIA, ambako watu wengi wameathiriwa na EBOLA.

No comments: