Serikali
ya Kenya imeamuru uchunguzi kufanywa baada ya majina ya wafanyakazi
hewa 12,000 kupatikana kwenye orodha yake ya mishahara.
Majina
hayo, yaligunduliwa baada ya maafisa wakuu kuanza kuwasajili wafanyakazi
wa serikali kwa njia ya kielektroniki kuanzia mwezi Septemba.Tume ya kupambana na rushwa nchini humo pamoja na kitengo cha kupambana na wizi kwenye benki zimetakiwa kuanzisha uchunguzi.
Kenya inashikilia nafasi ya 136 kati ya nchi 177 kwenye orodha ya shirika la kimataifa ya Transparency International ya mataifa fisadi zaidi duniani.
Ripoti ya awali iligundua kuwa serikali hupoteza takriban dola milioni moja kila mwezi kwa malipo ya mishara ya wafanyakazi ghushi, pamoja na nyenzo nyinginezo fisadi
Serikali inashuku kuwa wafanyakazi wa zamani wanaendelea kupokea mishahara hata baada ya kustaafu.
Rais Kenyatta ameamuru uchunguzi kufanywa mara moja
Wachunguzi katika idara ya ujasusi imeamrishwa kufanya uchunguzi kuhusiana na madai hayo.
Zaidi ya majina 12,500 ya wafanyakazi wa umma, waliokosa kufika kwa usajili wa kielektroniki, waliondolewa kwenye orodha ya mishahara mwanzoni mwa Novemba,kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation ambalo limenukuu waziri wa mipango na ugatuzi Ann Waiguru.Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kupambana na rushwa katika sekta ya umma baada ya kuchukua mamlaka mwaka jana.
No comments:
Post a Comment