VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Saturday, March 7, 2015

Waganga 32 wakamatwa Tanzania

Polisi nchini Tanzania wamewakamata waganga 32 wa kienyeji kazkazini magharibi mwa jimbo la Geita katika juhudi za kukabiliana na mauaji ya Albino.
Siku ya Alhamisi ,watu wanne walihukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanamke albino mwaka wa 2008 katika jimbo hilo.
Serikali iliwapiga marufuku waganga wa kienyeji mwezi Januari kama mojawapo ya kampeni ya kusitisha mauaji hayo.

Waganga wa kienyeji wanaamini viungo vya mwili wa Albino vina nguvu maalum za kuleta mafanikio na bahati.
Tanzania imeshuhudia mauaji ya albino 75 tangu mwaka 2000 kutokana na sababu hizo.
Afisa mkuu wa polisi katika jimbo la Geita Joseph Konyo ameiambia BBC kwamba waganga hao wa kienyeji walikamatwa na vifaa tofauti ikiwemo dawa za kienyeji na mafuta kutoka maeneo yasiojulikana.

Thursday, March 5, 2015

Diwani Chadema, aapa kulala mlangoni pa mwekezaji. hadi wafanyakazi walipwe!


             Na Bryceson Mathias, Mtibwa Mvomero.
   
DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, ameapa atalala mlangoni pa Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa, akishirikiana na wafanyakazi, hadi watakapolipwa mishahara yao ya miezi miwili wanayodai.

Akizungumza na Wafanyakazi nje ya lango la Kiwanda baada ya kumpigia simu kumlalamikia jinsi Mwekezaji alivyobadilisha maafikiano waliyoafikiana Jumatano Machi 4, mwaka huu kwaba kesho atawalipa mishahara yao, Mwakambaya ammeapa atalala mlangoni hadi walipwe.

Mwakambaya alisema, kama kuna aibu iliyokithiri inayolipata Taifa hili huku baadhi ya wawekezaji wakifanya mchana kweupe bila aibu, basi ni kudhulumu haki za wanyonge na kujinufaisha, kama wanavyofanyiwa wakulima Wadogo wa Miwa na wafanyakazi wa Mtibwa.

“Sasa tumechoshwa na Migogoro ya kila siku anayoibua Mwekzaji huyu kila kukicha, hivyo tunaandaa Unga na Dagaa za kutosha, ili viweze kuwatosheleza wafanyakazi waliopo hapa kukidai haki zao, jambo ambalo enzi za Mwalimu Nyerere ilikuwa ni ndoto kuona haya..

“Hatupendi kufanya hivyo lakini hii aibu ya Serikali kuwakumbatia Wawekezaji uchwara wasio na fedha au Mitaji ya kuwalipa Wafanyakazi na Wakulima wadogo na kuwanyonya, ambapo kimsingi hali hii inalifedhehesha sana Taifa letu, sieleai kwa nini Watawala hawalioni”.alisema Mwakambaya.

Alisema, anasikitishwa na Wawekezaji wa Kiwanda hicho ambao ni Vigogo wakubwa wa Chama cha apinduzi (CCM), kuendelea kuwanyonya Wafanyakazi na Wakulima wadogo wa Miwa katika Kata yake bila huruma, kama Kupe anavyonyonya Damu ya Ng’ombe huku hamlishi.

Uongozi wa Chama cha wafanyakazi mashambani na kilimo Tanzania (TPAWU) Tawi la Mtibwa, umekiri kuwa na Kikao na Meneja Mkuu Hamad Yahaya, Jumatno, Machi 4, na kuafikiana kwamba, Wafanyakazi wangelipwa siku ya pili Misharhaa wanayodai, lakini wameshangazwa akisema, Kiwanda hakina fedha..

Viongozi waaandamizi wa Kiwanda hicho walikuwa wameingia mafichoni, huku Meneja wa Kiwanda Yahaya Hamad, alikuwa ametimkia Morogoro Mjini asubuhi, baada ya kuwaahidi Wafanyakazi kuwa angewalipa haki zao leo, lakini akabadili kauli kuwa Kiwanda hakina fedha

Wednesday, March 4, 2015

MKUU WA MKOA WA MBEYA KANDORO AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA MBEYA

 Wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya Wapya iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya jijini hapa.
 Pichani ni wakuu wa Wilaya  za Mkoa wa mbeya

 Kiongozi wa dini ya kiislam akisomna dua katika hafla hiyo

 Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Zainabu Mbussi akiapa mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya 
 Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Ahmad Nammohe 
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Thea Ntara
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa akizungumza kwa niaba ya wenzake 
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa 
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini.

Monday, March 2, 2015

MPYAA MSANII WA BONGO MOVIE MWANADADA CHUCHU AZIRAI NDANI YA JENEZA WAKATI WA KUSHUTI MOVIE

HII ni kali ya mwaka! Staa wa sinema za Bongo, Chuchu Hans amejikuta akizirai ndani ya jeneza wakati akiigiza sini ya kifo kwenye filamu, Amani limeinyaka.
Staa wa sinema za Bongo, Chuchu Hans akiwa kwenye jeneza.
Chuchu alikumbwa na hali hiyo hivi karibuni akiwa ‘lokesheni’ ya kuigizia filamu hiyo maeneo ya Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam ambapo sanjari na yeye, msanii mwingine aliyecheza nafasi ya mwanakwaya naye alipoteza fahamu wakati kipande hicho kikirekodiwa.
TATIZO UHALISIA, WASIWASI
Chanzo kimoja kutoka ndani ya kundi la wasanii waliokuwa wakiigiza filamu kinasema kuwa, Chuchu alikumbwa na hali hiyo kutokana na wasiwasi na ujasiri wa kuuvaa uhusika.
“Awali, Chuchu alionesha wasiwasi wa kuigiza kipande hicho cha kumwonesha yeye yumo ndani ya jeneza akiwa amefariki dunia kwa ugonjwa kama wa kichaa kilichotokana na msongo wa mawazo baada ya kubakwa.
“Mbaya zaidi, mwongozaji naye alisema ni lazima akiwa amelala ndani ya jeneza awekewe pamba za kuziba matundu ya pua kama maiti wanavyowekewa,” kilisema chanzo.
...Waombolezaji wakilia kwa uchungu.
ILIKUWA WAKATI AKIAGWA
Chanzo kikazidi kudai kwamba, taharuki yote hiyo ilitokea pale, ‘mwili’ wa Chuchu ukiagwa kwenye Kanisa la Sabato, Mbezi, Dar ambapo waombolezaji walipokuwa wakipita, binti yake, Farha (9) aliangua kilio kilichomfanya Chuchu ajikute akikata pumzi ghafla!
AMALIZA SINI, ASHINDWA KUAMKA
Ikaelezwa kwamba, ilikuwa wakati kipande hicho kimeisha huku binti yake akiendelea kulia kwa kumwona mama yake ndani ya jeneza, Chuchu hakuamka ili kuendelea na vipande vingine hali iliyowafanya watu wazima kumkagua na kugundua alizirai.
“Watu walianza kupagawa, wengine walijua ameshapoteza maisha. Lakini Mungu mkubwa Chuchu akazinduka na kumkuta mwanaye bado akilia kwa nguvu. Ilibidi wasanii wengine waingilie kati kumtuliza,” kilisema chanzo.
Waombolezaji wakiwa na simanzi.
MWINGINE AITIWA MCHUNGAJI
Wakati Chuchu ‘akifufuka’, yule msanii aliyeigiza nafasi ya mwanakwaya yeye alikuwa bado chini amelala chali akiwa hajitambui kwa kile kilichokuwa kikiendelea.“Yule mwenzake ilibidi aitwe mchungaji wa kanisa hilo ambaye alikuwa jirani kwa ajili ya kumwombea japo mchungaji wa filamu hiyo alikuwa ni msanii Jimy Mafufu,” kilisema chanzo.
MASWALI ENEO LA TUKIO
Baadhi ya wasanii walianza kujiuliza nini kilisababisha hali ile kwani ilionekana kama kuna roho chafu aliyetaka kufanya mauaji ya makusudi.
“Wengine waliuliza kama kuna mtu ana vitu kama hirizi au chanjo ya mambo ya kishirikina, ikaonekana hakuna. Lakini maswali yalikuwa mengi sana,” kilisema chanzo.

Jeneza likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
CHUCHU AONGEA NA AMANI
Baada ya kuinasa taarifa hiyo, Amani lilimsaka Chuchu kwa njia ya simu yake ya mkononi na kumuuliza ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Huyu hapa:  “Yaani siwezi kueleza juu ya ile filamu maana ilikuwa ni hatari tupu na sijui hata mama yangu akiiona itakuaje kwa kweli.
“Lakini kwenye ile sini yangu ndiyo ilikuwa ikihitaji hivyo, nilale kama maiti kweli na huwezi amini lilichimbwa hadi kaburi la ukweli. Mimi nilizimia si chini ya  mara moja. Pumzi yangu ilikata hasa nilipomsikia mwanangu akilia.”
CHUCHU ANAWEZA ASIWE SAWA KISAIKOLOJIA
Kwa mujibu wa maswali ya kisaikolojia kwa wasanii wa maigizo, baada ya msanii kuigiza filamu inayohusu ukatili wowote, kumwaga damu, mapenzi ya kupitiliza, kifo au jambo lolote ambalo ni chungu kwa ubinadamu ni lazima aombewe na viongozi wa dini ili kuifukuza roho hiyo ya kuigizia.
Wanasaikolojia wanasema kuwa, msanii akiigiza nafasi kama hizo na kujiacha hivihihivi kuna hatari baada ya muda kuambukizwa na uigizaji huo ikawa ndiyo maisha yake ya kila siku. Ndiyo maana baadhi ya wasanii wa filamu duniani kote wanaishi maisha ya sawasawa na wanavyocheza filamu. 

AJINYONGA BAADA YA KUSALITIWA NA BOYFRIEND WAKE

Nitukio la kusikitisha lililotokea Nchini Nigeria baada ya msichana mmoja kuamua kuchukua maamuzi ya kujinyoga baada ya kuasilitiwa na  mpenzi wake
 
Taarifa kutoka kwa ndugu zake wa karibu ni kwamba mwili ma marehemu ulipatikana nyuma ya jumba baada ya siku chache majina yao marehemu na mpenzi wake yameifadhiwa

                                                POSTED BY VITUS MTAFYA