VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Thursday, March 5, 2015

Diwani Chadema, aapa kulala mlangoni pa mwekezaji. hadi wafanyakazi walipwe!


             Na Bryceson Mathias, Mtibwa Mvomero.
   
DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, ameapa atalala mlangoni pa Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa, akishirikiana na wafanyakazi, hadi watakapolipwa mishahara yao ya miezi miwili wanayodai.

Akizungumza na Wafanyakazi nje ya lango la Kiwanda baada ya kumpigia simu kumlalamikia jinsi Mwekezaji alivyobadilisha maafikiano waliyoafikiana Jumatano Machi 4, mwaka huu kwaba kesho atawalipa mishahara yao, Mwakambaya ammeapa atalala mlangoni hadi walipwe.

Mwakambaya alisema, kama kuna aibu iliyokithiri inayolipata Taifa hili huku baadhi ya wawekezaji wakifanya mchana kweupe bila aibu, basi ni kudhulumu haki za wanyonge na kujinufaisha, kama wanavyofanyiwa wakulima Wadogo wa Miwa na wafanyakazi wa Mtibwa.

“Sasa tumechoshwa na Migogoro ya kila siku anayoibua Mwekzaji huyu kila kukicha, hivyo tunaandaa Unga na Dagaa za kutosha, ili viweze kuwatosheleza wafanyakazi waliopo hapa kukidai haki zao, jambo ambalo enzi za Mwalimu Nyerere ilikuwa ni ndoto kuona haya..

“Hatupendi kufanya hivyo lakini hii aibu ya Serikali kuwakumbatia Wawekezaji uchwara wasio na fedha au Mitaji ya kuwalipa Wafanyakazi na Wakulima wadogo na kuwanyonya, ambapo kimsingi hali hii inalifedhehesha sana Taifa letu, sieleai kwa nini Watawala hawalioni”.alisema Mwakambaya.

Alisema, anasikitishwa na Wawekezaji wa Kiwanda hicho ambao ni Vigogo wakubwa wa Chama cha apinduzi (CCM), kuendelea kuwanyonya Wafanyakazi na Wakulima wadogo wa Miwa katika Kata yake bila huruma, kama Kupe anavyonyonya Damu ya Ng’ombe huku hamlishi.

Uongozi wa Chama cha wafanyakazi mashambani na kilimo Tanzania (TPAWU) Tawi la Mtibwa, umekiri kuwa na Kikao na Meneja Mkuu Hamad Yahaya, Jumatno, Machi 4, na kuafikiana kwamba, Wafanyakazi wangelipwa siku ya pili Misharhaa wanayodai, lakini wameshangazwa akisema, Kiwanda hakina fedha..

Viongozi waaandamizi wa Kiwanda hicho walikuwa wameingia mafichoni, huku Meneja wa Kiwanda Yahaya Hamad, alikuwa ametimkia Morogoro Mjini asubuhi, baada ya kuwaahidi Wafanyakazi kuwa angewalipa haki zao leo, lakini akabadili kauli kuwa Kiwanda hakina fedha

No comments: