Shirika
la umeme nchni-Tanesco-limesema hakuna mgao wa umeme na kilichojitokeza
kufuatia kukatika kwa umeme mara kwa mara kuanzia machi 15 ni uchakavu
wa miundombinu ya umeme ikiwemo kuanguka kwa nguzo za umeme hususani
katika maeneo ya makazi ya watu yasiyopimwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari, baada ya baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es
Salaam na vitongoji vyake kukosa umeme kwa wakati tofauti kuanzania
machi 15 hadi 18 mwaka huu, meneja wa kanda wa Tanesco, mhandishi
Mahenge Mugaya amesema changamoto kubwa inayoikabili Tanesco ni uchakavu
wa nguzo na nyaya za kusafirisha umeme ambapo katika baadhi ya maeneo
yasiyopimwa kumekuwa na tatizo la magari kugonga nguzo na umeme hali
inayosababisha mitambo ya shirika hilo kukata umeme ili kuzuia madhara
kwa jamii.
Aidha
amesema shirika la umeme nchni limetenga bajeti ya shilingi bilioni 10
katika mpango wa miaka mitatu wa kuimarisha umeme katika jiji la Dar es
Salaam, mpango utakaowezesha kuondoa nguzo mbovu, miti iliyokatika njia
za umeme na kuimarisha vituo vidogo vya kusambaza umeme na kusisitiza
shirika hilo limeshafanya tathimini ya nguzo mbaovu zote katika njia za
umeme na kuandaa mpango kazi ili kuwa na mfumo mzuri wa usambazaji
umeme.
No comments:
Post a Comment