Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Msangi.
Akithibitisha
kutokea kwa matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema
katika tukio la kwanza Mwili wa marehemu ulikutwa katika nyumba aliyokuwa
akiishi mnamo tarehe 16.03.2015 majira ya saa 10:00 asubuhi huko katika
kitongoji cha rusungo, kijiji na kata ya chitete, tarafa ya bulambya, wilaya ya
ileje, mkoa wa Mbeya.
Mwili wa
marehemu ulikutwa ukiwa na majeraha sehemu za kichwani ya kukatwa kitu chenye
ncha kali na huku ukiwa umeanza kuharibika. chanzo cha tukio hilo
kinachunguzwa, upelelezi zaidi unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watu
waliohusika katika tukio hili.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed z. Msangi
anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa watu
waliohusika katika tukio hili azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na
hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari kiwira wilayani Rungwe
aliyefahamika kwa jina la Yohana Kaini (17) mkazi wa kijiji cha ibula alifariki
dunia baada ya kugongwa na gari ambalo halikuweza kufahamika namba zake za
usajili wala dereva wake.
Tukio hilo
limetokea mnamo tarehe 16.03.2015 majira ya saa 07:00 asubuhi huko katika
kitongoji cha kikumbe, kijiji cha Ibula, kata ya Kiwira, tarafa ya Ukukwe,
wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya.
Inadaiwa
kuwa, marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake aitwaye Rojas Yusuph (15) mkazi wa
kijiji cha ibula wakiwa wamepakizana kwenye baiskeli wakielekea shule ndipo
waligongwa na gari hilo lililokuwa likitokea tukuyu kuelekea mbeya mjini.
Katika ajali
hiyo Rojas Yusuph alijeruhiwa na amelazwa katika hospitali ya misheni
Igogwe-Tukuyu. chanzo cha ajali ni mwendo kasi. dereva alikimbia mara baada ya
ajali na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
kamanda wa
polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi
anatoa wito madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na
kufuata sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali. aidha anatoa
wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo dereva wa aliyesababisha ajali
hii azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yake.
No comments:
Post a Comment