VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Saturday, August 8, 2015

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA KUHITIMISHA SIKU YA NANE NANE JIJINI MBEYA


 Hawa ni watu ambao wameweza kufika katika viwanja vya John Mwakangale kwa ajili ya kujionea mambo mbalimbali Nanenane
 Baadhi ya wanafunzi walionekana wakiwa kaika viwanja hivyo kwa ajili ya kujifunza mbalimbali yahusuyo Kilimo, ufugaji na Mengine mengiiiii....
 Wafanya Biashara nao hawakuwa mbali, kuumia fursa kupitia msimu wa nane nane.
 Uuzaji wa Mitumba ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa katika viwanja vya nane nane 
 Wengine hao wanaondoka

Thursday, July 30, 2015

PICHA: Lowassa Achukua Fomu ya Urais CHADEMA


Edward Lowassa akionesha fomu ya kuwania urais aliyokabidhiwa leo Makao makuu ya Chadema,D ar.
CLJ5hSGWoAACCU3
Umati wa watu waliojitokeza kumpokea Lowassa wakati akichukua fomu ya urais kupitia Chadema.
CLJ8fhkW8AA6IKB
…Akisaini katika kitabu cha wageni.
CLJ9y4iWEAAZWy7
Mnadhimu Mkuu kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu akitoa yake machache.CLJ52JsWwAA--Yc
Lowassa akiwasiri kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Dar leo.
CLKRw2sWcAAzeL9
Baada ya kuchukua fomu.
mbowe na lowassa
Mwenyekiti wa Chadema (kushoto) Mhe. Freeman Mbowe Mhe. Edward Lowassa (katikati) wakati wa zoezi la kuchukua fomu lililofanyika leo Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar .
LOWASA (1)
LOWASA (2)
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika meza kuu ya Chadema.
 **
WAZIRI MKUU wa zamani, Mhe. Edward Lowassa hivi punde amechukua fomu ya kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Lowassa amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 
Lowassa alijiunga rasmi na Chadema juzi akitokea CCM baada ya kuondolewa kwenye mchakato wa kuwa mgombea urais wa chama hicho akidai kuwa jina lake liliondolewa kwa mizengwe.

Wednesday, July 29, 2015

CCM Wamjibu LOWASSA........Wasema Kuhama kwake Hakuna madhara na kwamba Watapata ushindi wa kishindo

 Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Dar, Juma Simba Gaddafi  jana  aliongoza  mkutano  wa  CCM  na  waandishi  wa  habari  uliofanyika  Peacock Hotel Dar, na  haya  ndo  mambo  aliyoyasema;
 
"CCM inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama chenye busara tumeona tuwashukuru

"Tume ya Uchaguzi tunawaomba wawe makini kuongeza Mashine na Watendaji ili watu wapate nafasi kujiandikisha na watumie fursa yao Kupiga Kura… CCM tuna uhakika tutashinda.

"Kingine tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura… 
 
"Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi nzuri… 

 "Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya mengi yanayokubalika."

Akiongelea  sakata  la  Lowassa  kuhamia  CHADEMA, Gaddaf  alisema;
 
"Yeye aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM, kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka.

"Mtu akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe… 
 
"Kama Lowassa angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara."

Akiongelea  kuhusu Uteuzi wa Mgombea wa Urais CCM Dodoma, Gaddaf  alisema;

"Mkutano Dodoma tuliumaliza, lakini tumekwenda kwenye NEC Wajumbe wako 360, walipiga kura majina matano na Wagombea wote wa Halmashauri Kuu akiwepo Rais, Waziri Mkuu na Lowassa walikuwepo… kama asingekuwepo hayo yangesemwa, lakini alishiriki na alipiga Kura"

Tuesday, July 28, 2015

Mbunge Mwingine wa CHADEMA Arudisha Kadi na kujiunga na CCM



MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere ameng'atuka rasmi jana katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam, Leticia alisema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.

Alisema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.
 
“Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa CHADEMA na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi nyumbani kutumikia” amesema Leticia.

Leticia alisema kwenda CHADEMA alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.

Alisema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi.

Monday, July 27, 2015

Lowassa Akaribishwa Rasmi UKAWA......Hapa kuna picha na kilichojiri Leo Katika mkutano wa UKAWA na Waandishi wa habari


“Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje”. Hii ni moja ya kauli  ambayo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliziongea Arusha May 30 2015 alipotangaza nia ya Kugombea Urais kupitia CCM.
 
CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40 ambao walitangaza nia na kuchukua fomu za Kugombea Urais 2015 lakini baadae Chama hicho kikampitisha Dk. John Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo, baada ya hapo kukawa na  taarifa nyingi sana kuhusu ishu ya Edward Lowassa na UKAWA.
 
Viongozi wa Umoja wa UKAWA wamekutana Dar  leo  na mmoja wa Viongozi hao, James Mbatia amesema wamekubaliana kumkaribisha Mbunge Edward Lowassa ndani ya UKAWA na wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana nae.

Mbatia  ameongeza kuwa Lowassa ni mchapa kazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa kiutendaji katika majukumu anayokabidhiwa.
 
Alipoulizwa kuwa Lowassa atakuwa mgombea Urais Mbatia amesema kila chama kina utaratibu wake  hivyo mchakato ukishakamilika  atatangazwa mgombea urais wa UKAWA mmoja  mwanzoni mwa mwezi agosti.




Wednesday, July 22, 2015

Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo


Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema watu  zaidi  ya 10  wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo , huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.
 
Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma.Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu.

Monday, July 20, 2015

Majambazi Walioua Polisi na Raia Kituo cha Polisi Stakishari Wakamatwa



MAJAMBAZI waliovamia Kituo cha Stakishari jijini Dar es Salaam watatu wauwawa na wawili watiwa mbaroni wakati wakitupiana risasi katika eneo la Tuangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 
Tukio hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, na majambazi wa tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao  inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.
 
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika eneo la Tuangoma ndipo majambazi wakapita na pikipiki mbili walipowasimamisha askari majambazi hao walikaidi amri nakisha kuanza kurusha risasi na polisi wakajibu na majambazi watatu kuuwawa.
 
Majambazi waliouawa ni Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala,Yassin alitambulika kwa jina moja mkazi wa Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina moja mkazi wa Mandimkongo ,Mkuranga.
 
Kamanda Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15),Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, Omary Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.
 
Kova amesema baada ya kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki  15 walizopora katika kituo cha Stakishari ambazo walikuwa wamehifadhi chini ya ardhi na kuweka kinyesi juu.
 
Amesema katika Shimo walilohifadhi walikuta bunduki aina ya  Norinko ambayo wanatafuta ilipoibiwa pamoja na kukuta fedha taslimu Sh.Milioni 170 za kitanzania.
 
Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kwa kuwa halipi.
 
Amesema fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibwa wapi,na pikipiki mbili aina ya boxer nazo wanazishiklia na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanataarifa nao.
 
“Hatutafumbia macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au askari” amesema Kamishina Kova.
 
Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea  julai 12 majira ya saa nne.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari, Tazara,leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Stakishari ,Tazara,jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi katika kituo stakishari,Tazara leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na majambazi waliovyamia kituoa stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar es Salaam.
 Fedha za watuhumiwa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakiki zikiwa katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi habari na wananchi leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha picha za majambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi katika hafla ya kutuoa taarifa za kukamatwa kwa askari wa waliovamia kituo cha stakishari leo jijini Dar es salaam 
Pikipiki zilizokuwa zikitumiwa na majambazi waliovyamia Kituo cha Stakishari zikiwa mbele ya Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao leo jijini Dar es Salaam.