MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere ameng'atuka rasmi jana katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa idara ya habari
maelezo jijini Dar es Salaam, Leticia alisema kuwa katika suala la
kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza
kwenda huko.
Alisema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila
ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika
masuala ya siasa.
“Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa CHADEMA na kuacha
kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa
nasema narudi nyumbani kutumikia” amesema Leticia.
Leticia alisema kwenda CHADEMA alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi
kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na
atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na
kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.
Alisema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi
(CCM) hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi.
No comments:
Post a Comment