Wakati bado haijafahamika lini mgombea urais kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) atatangazwa rasmi, imefahamika kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba, amekuwa ndiyo kikwazo cha kutopatikana kwa mgombea huyo.
Uchunguzi
uliofanywa na mtandao huu kwa siku nne sasa umebaini kuwa hatua ya
Profesa Lipumba kukwepa vikao vya Ukawa, ni mkakati mahsusi unaolenga
kukwamisha mchakato wa kupatikana mgombea urais wa umoja huo.
Ukawa unaundwa na Cuf, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi na NLD.
Taarifa
kutoka ndani ya vikao vya Ukawa vimeeleza kuwa kikao cha kwanza cha
umoja huo, Profesa Lipumba aliulizwa kwanini anataka kugombea urais na
kujibu kuwa anaamini kuwa yeye ndiye bora kuliko wengine.
Hata
hivyo, alipoulizwa kama amejiandaa vipi kirasilimali iwapo atateuliwa
kuwania nafasi hiyo kupitia Ukawa, hakuwa na majibu ya kujitosheleza na
badala yake ilibainika kuwa Cuf imejiandaa zaidi Zanzibar kuliko
Tanzania Bara.
Taarifa
zaidi zinaeleza kuwa Profesa Lipumba amekuwa aking’ang’ania agombee
urais na hata mkutano wa mwisho wa Ukawa ambao hakuhudhuria, inadaiwa
kwamba ni mkakati wa kushinikiza ateuliwe yeye kugombea nafasi hiyo ya
juu ya uongozi wa nchi.
Katika
vikao vya Ukawa, hoja kubwa imekuwa ni suala la mgombea urais, nafasi
ambayo inawaniwa na Profesa Lipumba ambaye tayari ameshachukua fomu
kupitia chama chake cha Cuf pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.
Willibrod Slaa, anayeungwa mkono na vyama vyote vinne.
Profesa
Lipumba ameshagombea urais mara nne bila mafanikio, wakati Dk. Slaa
aligombea mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili, akiwa ameitikisa CCM
iliyopoteza asilimia takriban 20 ya kura za mwaka 2005.
Mwenyekiti
Mwenza wa Ukawa, James Mbatia, akizungumza na waandishi wa habari Julai
14, mwaka huu, alisema umoja huo utamtangaza mgombea wao wa urais baada
ya siku saba ambazo zinaisha wiki hii.
Alisema
wamekubaliana kutangaza mgombea baada ya siku saba ili kutoa nafasi kwa
viongozi walioshiriki majadaliano hayo kutoa taarifa kwa wanachama wa
vyama vyao juu ya mambo waliokubaliana.
Aidha,
Mbatia alikanusha uvumi kuwa kada wa CCM na Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa, ana mpango wa kujiunga na umoja huo ili apewe nafasi ya
kugombea urais baada ya kukosa nafasi hiyo kupitia chama chake.
Mbatia
pia alikanusha uvumi ulioenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna
mvutano mkubwa ndani ya Ukawa katika suala la mgombea urais ambao
umesababisha Cuf kutaka kujitoa.
“Hakuna
ukweli katika hilo na hata leo (jana), nimeongea na Profesa Lipumba
kumtaarifu hatua tulioyofikia, hivyo hakuna mpasuko wowote,” alisema Mbatia.
Kabla
ya taarifa hiyo ya Mbatia,Ijumaa iliyopita Ukawa walitoa taarifa ya
kwamba wangemtangaza mgombea wake ndani ya saa 24, ahadi ambayo
haikutimizwa.
No comments:
Post a Comment