VIONGOZI
mbalimbali wa dini nchini wameandaa maandamano kwa lengo la kumuona
Rais jakaya kikwete ili kumuomba alifanyie mabadiliko makubwa Jeshi
Polisi.
Mabadiliko
hayo ni pamoja na kubadili mawaziri wote wa mambo ya ndani, mkuu wa
jeshi hilo (IGP) na MA-CP wawili ambao wametajwa kuendesha jeshi
hilo kimtandao kinyume na taratibu za kijeshi.
Maandamano
hayo yamefikiwa na Maaskofu na Mashekhe 160 wa mjini Dodoma jana chini
ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, amani na haki za binadamu ya
Madhehebu ya Dini Nchini Askofu William Mwamalanga.
Mwamalanga
alisema viongozi hao wamepokea taarifa ya kuuwa kwa askari polisi
wanne wa kituo cha stakishari cha jijini Dar es Salaam kwa masitikito.
“Tumepokea
taarifa ya vifo vya askari hawa kwa masikitiko, hali hii haikubaliki
kila mara vituo vimekuwa vikivamiwa na hadi sasa takriban Askari 47
wameuwawa,” alisema Mwamalanga.
Huku
akibubujikwa na machozi ya Uchungu Askofu Mwamalanga amehoji ukimya wa
Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe na IGP Erinest Mangu kwa vifo
vyote ambavyo vimekuwa vikitokea tangu mwaka huu uanze.
“Uvamizi
huu na mauaji ya askari wa chini unatisha na hatuoni hatua yoyote ya
maana iweje wahalifu wawe na nguvu kuliko jeshi hasa kipindi hiki
ambacho dunia inakabiliana na makundi ya wahalifu hatari wakiwemo al
shabab,” alihoji.
Kufuatia
hali hiyo, ASkofu Mwamalanga amemuomba Rais kikwete kuwaongeza
askari wangazi ya chini mishahara kwa kiwango cha Millioni moja
ili walingane na wenzao wa nchi za afrika mashariki na kusini.
Alisema
hatua hiyo itawawezesha askari hao kukabiliana na changamoto za maisha
kama ilivyofanya kwa wafanyakazi Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo
ilisema hiyo itawaondolea tamaa za Rushwa.
“Kwa
Polisi ni zaidi kwani kitendo cha kuuwawa kama tembo porini bila
mshahara mzuri kunawakatisha tamaa na ari ya kufanya kazi,” alisema.
Askofu
Mwamalanga ambaye ni Mwanaharakati Mtafiti wa haki za jamii alisema
idadi kubwa ya Maaskofu na Maashekhe nchini wamelaani Mauaji hayo
yanayoendelea dhidi ya polisi.
“Tayari
zaidi ya askari 47 wameuwawa na wengine wamebaki vilema, silaha lukuki
zimechukuliwa vituoni na kutokomea kusikojulikana, hili lina dhihirisha
kuwa Taifa letu lipo pabaya. Ndiyo maana tunaona ipo haja tena muhimu
kwa rais kwachukilia hatua za haraka wanaosababisha uzembe huo ikiwa ni
pamoja na kulifanyia ukarabati jeshi hili,” alisema.
Aliwakumbusha
watanzania kuliona jeshi hilo kuwa ni chombo chao cha kuwalinda wao
wawe salama dhidi magenge ya uhalifu duniani hivyo wana wajibu kama
raia wema kuhakikisha wanawalinda askari hao kwa hali na mali ikiwa ni
pamoja na kuwapa taarifa muhimu ili kuwakamata wauaji wote pamoja na
silaha zote zilizoporwa.
Aidha
viongozi hao walihoji kuondolewa kwa vizuizi [ berial] barabarani
kulikuwa na maslahi gani kwa usalama wa nchi kwani hivi sasa wahalifu
wametumia nafasi kutoroka kirahisi pale wanakuwa wamefanya uhalifu.
“Tunataka vizuizi hivyo virudishwe mara moja kwa barabara zote nchini,” alisema.
Kwa
upande wake shekhe Athumani Mukambaku ambaye ni Mwenyekiti mwenza
wa Kamati hiyo na mjumbe wa BAKWATA halmashauri ya mkoa wa dar es
Salaam alishauri serikali itunge sera mahususi ya raia wote kuwalinda
polisi baadala ya dhana iliyojengeka kuwa ni polisi pekee ndiyo wenye
wajibu wa kulinda raia, jambo linalojenga chuki pale ambapo polisi
wanaposhindwa kusimamia haki za raia sawasawa.
“Katika
kipindi hiki cha kulelekea uchaguzi mkuu jeshi linapaswa kuimarisha
vituo vyake vyote ikiwa ni pamoja na kufunga kamera maalumu za cctv ili
kuweka rekodi ya watu wote wanaotembelea vituo hivyo pamoja kuvunja
kanda maalumu za kipolisi ambazo hazionesha juhudi ya kupambana na
uhalifu na baadala yake zimeongeza gharama kwa jeshi hilo,” alisema Shekhe Mukambaku.
Alisema
rais anapaswa ateue makamanda wabunifu wanaokwenda na wakati na kwamba
kila mkoa uwe maalumu kwa kuimarisha vitendea kazi vya askari ikiwa ni
pamoja kuwapatia motisha wale walio ngazi ya chini ambao hukesha vituo
kuimarisha ulinzi.
No comments:
Post a Comment