VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Tuesday, August 18, 2015

CCM Yatangaza Kamati ya Kampeni za Uchaguzi Yenye Watu 32 Chini ya Abdulrahman Kinana


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).
 
Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 
 
Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-

1.    Ndugu Abdulrahman Kinana        -    Mwenyekiti
2.    Ndugu Rajab Luhwavi     -    Makamu Mwenyekiti – Bara
3.    Ndugu Vuai Ali Vuai      -     Makamu Mwenyekiti - Z’bar
4.    Ndugu Sofia Simba
5.    Ndugu Mohamed Seif Khatib
6.    Ndugu Asha-Rose Migiro
7.    Ndugu Samwel Sitta
8.    Ndugu Nape Nnauye
9.    Ndugu Mwigulu Nchemba
10.    Ndugu Harrison Mwakyembe
11.    Ndugu January Makamba
12.    Ndugu Amina Makillagi
13.    Ndugu Christopher Ole Sendeka
14.    Ndugu Stephen Wasira
15.    Ndugu Abdallah Bulembo
16.    Ndugu Hadija Aboud
17.    Ndugu Mohamed Aboud
18.    Ndugu Lazaro Nyalandu
19.    Ndugu Issa Haji Ussi
20.    Ndugu Waride Bakari Jabu
21.    Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
22.    Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
23.    Ndugu Maua Daftari
24.    Ndugu Stephen Masele
25.    Ndugu Pindi Chana
26.    Ndugu Shaka Shaka
27.    Ndugu Makongoro Nyerere
28.    Ndugu Bernard Membe
29.    Ndugu Sadifa Juma Khamis
30.    Ndugu Antony Diallo
31.    Ndugu Livingston Lusinde
32 .    Ndugu Ummy Mwalimu

Imetolewa na:-

Sunday, August 16, 2015

Miaka 130 Jela Kwa Kosa la Kumuambukiza Mtoto wa Miaka 9 Ukimwi

 

Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 130 jela kwa kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 ukimwi.
Katika kikao hicho Mahakama kuu ya Kenya mjini Kisumu imempata na hatia bwana John Okewo mwenye umri wa miaka 25 na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye jina lake limebanwa.

Hakimu mwandamizi Aswani Opande alimpata na hatia bwana Okewo kwa kumabaka mtoto huyo na akamhukumu kifungo cha miaka 100 jela.
Katika shtaka la pili hakimu huyo mkuu wa eneo la Tamu lililoko Muhoroni alimhukumu mstakiwa kifungo cha miaka mingine 30 kwa kumuambukiza msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 ugonjwa wa Ukimwi.

Hakimu alimpata na hatia bwana Okewo kutokana na kukiri makosa yake mwenyewe.
Upande wa mashtaka unasema kuwa bwana Okewo alimpa mtoto huyo pipi na biskuti mnamo tarehe 27 mwezi Machi kabla ya kumdanganya hadi akaingia chumbani mwake.
Yamkini Okewo aliwaambia wachunguzi kuwa alimdhulumu mtoto huyo mara kadha.

Mtoto huyo alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi biskuti na ''kumlalia''
Mtoto huyo alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi na ''kumlalia''
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 anaendelea na matibabu maalum ya wanawake baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.

Alipopewa fursa ajitetee, mshtakiwa aliomba asamehewe kwani ni ''shetani aliyemdanganya'' kutenda maovu hayo.

Hata hivyo Hakimu akakataa kabisa kumuonea huruma na akamhukumu kifungo cha miaka 130 jela ili iwe funzo kwake na kwa wengine wenye mawazo potofu kama yake.
Alipewa siku 14 kukata rufaa.
mwezi Machi kabla ya kumdanganya hadi akaingia chumbani mwake.
Yamkini Okewo aliwaambia wachunguzi kuwa alimdhulumu mtoto huyo mara kadha.

Mtoto huyo alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi biskuti na ''kumlalia''
Mtoto huyo alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi na ''kumlalia''
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 anaendelea na matibabu maalum ya wanawake baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.

Alipopewa fursa ajitetee, mshtakiwa aliomba asamehewe kwani ni ''shetani aliyemdanganya'' kutenda maovu hayo.

Hata hivyo Hakimu akakataa kabisa kumuonea huruma na akamhukumu kifungo cha miaka 130 jela ili iwe funzo kwake na kwa wengine wenye mawazo potofu kama yake.
Alipewa siku 14 kukata rufaa.

Friday, August 14, 2015

TUKIO LA KUSIKITISHA : RUNGWE AUAWA KINYAMA NA KUTUPWA KADO YA BARABARA




Tukio hilo limetokea wilayani rungwe mkoani Mbeya kata ya Katumba. Marehemu anasadikika kuwa ni mkazi wa Wilayani Ileje Mkoani Mbeya.
Pia inasemekana kuwa marehemu ametupwa sehemu hiyo usiku wa kuamkia leo na watu wasiosemekana  kwa kutumia Usafiri wa bodaboda.
                                     Picha zaidi.











Thursday, August 13, 2015

Dk Slaa aikana twitter inayomzushia mazito


Wakati kukiwa na taarifa zinazosambaa mtandaoni zikimuhusisha Dk Willibrod Slaa na akaunti ambayo imekuwa ikitoa msimamo wake wa kujitenga na shughuli za siasa pamoja na Ukawa, katibu huyo mkuu wa Chadema amekanusha taarifa hizo akisema hajawahi kuwa na akaunti ya twitter.
 
Dk Slaa, aliyekuwa anatajwa kuwa mgombea urais wa Chadema, hajaonekana hadharani katika matukio makubwa ya kichama tangu Chadema na Ukawa walipomkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kumteua kuwa mgombea urais anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja huo.

Mara ya mwisho kuonekana kwenye shughuli za chama hicho ni katika kikao cha Kamati Kuu wakati Lowassa alikaribishwa kufanya majadiliano na kujibu hoja za wajumbe.

Lakini baada ya hapo Dk Slaa hakuonekana wakati wa kutambulishwa kwa Lowassa kwa waandishi wa habari, tukio la kuchukua na kurudisha fomu za urais ndani ya chama na tukio la juzi la kuchukua fomu za urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wakati hayo yakiendelea, kuna akaunti ya twitter yenye jina la “Dr Willibrord Slaa” ambayo imekuwa ikitoa kauli mfululizo zikiwa na ujumbe mbalimbali unaoendana na mazingira aliyomo sasa mwanasiasa huyo.

 Agosti 10, kulitumwa ujumbe zaidi mara 10, mmojawapo ukijaribu kuwaaminisha watu kuwa hiyo ni akaunti halisi ya Dk Slaa.

“Ndugu zangu Watanzania, hii ni akaunti yangu rasmi, bila shaka yoyote na naomba ninachoandika hapa kifikishwe kwa Watanzania popote walipo,” unasema ujumbe huo.

Taarifa nyingine zilizotumwa kwenye akaunti hiyo ya twitter ni pamoja na ile iliyoeleza kuwa   Dk Slaa ameomba ulinzi kutoka nchi na mashirika ya kimataifa na atazungumza kupitia runinga na redio pindi atakapopata ulinzi.

Akizungumzia sakata  hili jana, Dk Slaa alisema hajawahi kutuma taarifa yoyote kwenye mitandao ya kijamii.

“Sijawahi ku-operate (kuendesha) kitu chochote kwenye akaunti ya twitter, sina akaunti kama hiyo,” alisema Dk Slaa.

Mbali na kukanusha kumiliki na kuendesha akaunti hiyo, Dk Slaa alirudia kauli yake ya wiki iliyopita kuwa atatoa msimamo wake muda muafaka utakapofika, baada ya kuulizwa swali kuhusu hatma yake ndani ya Chadema na kisiasa kwa ujumla.

“Subira yavuta heri, sasa ili uipate hiyo heri unatakiwa kuvumilia. Kwa hiyo wakati ukifika nitazungumza tu na Watanzania,” alisema.

Alipoulizwa ni wapi alipo kwa sasa, alisema yupo Dar es Salaam anapumzika, lakini akasisitiza kuwa ipo siku ataweka wazi mustakabali wake kisiasa.

Dk Slaa alisema yeye na mke wake Josephine Mushumbusi wanatarajia kusafiri kwenda nje ya nchi katika siku chache zijazo, ingawa hakuweka wazi nchi anayotarajia kuitembelea, lakini akasema atarejea baada ya wiki moja.

Tuesday, August 11, 2015

Magufuli Aahidi Ushindi wa Tsunami CCM......Asema Wapinzani Wataishia Kupiga Kelele Tu, Mwigulu Nchemba Naye Apigilia Msumari wa 'Moto'



MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, amewahakikishia wana-CCM na Watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa Tsunami na si wa kishindo wala kimbunga.

Dk Magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani Mtwara juzi alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa CCM ni lazima na upo pale pale.

Alisema ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama na kwamba watu hao wameiacha CCM ikiwa safi na salama zaidi. 
 
Alisema watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ambapo chama kiliwakata na kukimbilia vyama vingine vya upinzani.

Aliwataka wana-CCM wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya kampeni za kisayansi. 
 
Aidha, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema ni kazi rahisi kumnadi Dk Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.

Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema walioshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi, lakini wataumbuka mapema.

Akizungumza na mamia ya wana-CCM waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mgombea na kumdhamini, Dk Magufuli aliwataka makada hao na Wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa Watanzania walio wengi bado wanakipenda Chama.

Ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa Tsunami, watapiga kelele sana, watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa CCM ni lazima. Ni lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani,” alisema. 
 
Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, CCM ina kundi moja tu la ushindi.

“Hako ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao safi.
 
 “Lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM.

"Hata ukiangalia tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wapo waliotoka wako akina Kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao,” alisema.

Alisema iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu, asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atimize matarajio yao.
 
 Dk Magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.

Aliwataka wana-CCM wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda Chama.
 
 Dk Magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya CCM, alisema alikuwa mbunge katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.

Alisema anaifahamu vizuri Mtwara, Tanzania, CCM na kero za Watanzania anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya utendaji kwa maendeleo ya taifa.
 
 “Nilichaguliwa na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale walionichagua waliwakishia Watanzania wote. Niwahakikishie kuwa mwaka huu, tutashinda zaidi,” alisema.
Aliwataka wana-CCM katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si maneno matamu bila vitendo.

“Chama nakifahamu, shida za wana-CCM nazifahamu, matarajio yao nayafahamu, shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo,” alisema.

Sunday, August 9, 2015

BENKI YA POSTA TANZANIA, YASAIDIA SHULE ZA MSINGI WILAYANI ILEJE MKOANI MBEYA‏


  

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mmbene, (wapili kushoto), akipeana mikono na Meneja msaidizi wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, tawi la Tunduma, Teddy Msanzi, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolewa kama msaada na benki hiyo, kusaidia shule mbili za msingi wilayani Ileje, mkoa wa Mbeya, hivi karibuni


Benki ya Posta Tanzania (TPB) kupitia tawi lake la Tunduma, imetoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi Milioni Tatu kwa shule mbili za Msingi zilizopo Wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Akikabidhi madawati hayo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene kwenye hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Wilayani humo hivi karibuni, Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Tunduma Teddy Msanzi alisema kuwa,  Benki yake iliguswa sana na suala la uhaba wa madawati kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo na kuona ni muhimu kusaidia.
“Benki ya Posta inatambua umuhimu wa elimu bora kwa ajili ya kujenga kizazi bora cha baadae. Ni vigumu kutoa elimu bora katika mazingira magumu ya wanafunzi kukaa chini madarasani.Ni vema wanafunzi wetu wakawekewa mazingira mazuri ya kupata elimu, ikiwemo madawati. Hivyo basi sisi Benki ya Posta tunatoa madawati haya 100 ili kupunguza tatizo hili.” Alifafanua Teddy.
Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya elimu wilaya Ileje, Wilaya hiyo ina jumla ya wanafunzi 28,488 wa shule za Msingi , lakini idadi ya madawatii ni 10,028, na kufanya idadi ya madawati yanayohitajika kuwa 4,116.
Akitoa shukrani zake kwa niaba ya shule za Wilaya ya Ileje, Mhe. Janeth Mbene aliishukuru Benki ya Posta kwa msaada huo ambao alisema ni mkombozi kwa wanafunzi waliokuwa wakikaa chini kwa muda mrefu. Alitumia fursa hiyo pia kuziomba taasisi nyingine ziguswe na tatizo lao na ziweze kuwasaidia ili waweze kuondokana na changamoto hiyo.


 Naibu Waziri Mmbene, akiwa na maafisa wa benki hiyo, tawi la Tunduma
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimkabidhi katibu wa CCM Wilaya ya Ileje Hamida Mbogo madawati ya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi wilayani ileje ambayo yametolewa na benki Posta Tawi la Tunduma.

Saturday, August 8, 2015

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA KUHITIMISHA SIKU YA NANE NANE JIJINI MBEYA


 Hawa ni watu ambao wameweza kufika katika viwanja vya John Mwakangale kwa ajili ya kujionea mambo mbalimbali Nanenane
 Baadhi ya wanafunzi walionekana wakiwa kaika viwanja hivyo kwa ajili ya kujifunza mbalimbali yahusuyo Kilimo, ufugaji na Mengine mengiiiii....
 Wafanya Biashara nao hawakuwa mbali, kuumia fursa kupitia msimu wa nane nane.
 Uuzaji wa Mitumba ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa katika viwanja vya nane nane 
 Wengine hao wanaondoka