VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Wednesday, December 3, 2014

Picha 19 za jinsi Diamond Platnumz alivyopokelewa Dar es salaam, mpaka Polisi ndani ya msafara.




d17Baadhi ya mastaa wa Afrika walioona mapokezi ya Diamond Dar es salaam wamependa sana upendo wa Watanzania kujitokeza kumpokea Platnumz baada ya kushinda tuzo tatu za Channel O 2014 zilizotolewa Johannesburg South Africa.
Kwenye msafara wa Diamond Platnumz kulikua na Polisi pia ambao kazi yao ilikua ni kuhakikisha usalama unakuwepo ambapo sehemu nyingine Diamond alilazimika kushuka na kutembea kupiga picha na watu wake.
d16
d15
d12
d11
d10
d5
d2
d1
d3
d6

d8
d4
d9
d13
d14
d18
d19Ni ahadi yangu kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza

Tuesday, December 2, 2014

Katuni wa Zenj leo na Ujumbe Wakee huuooooooo.............

Angalia video mpya ya Fleva "Gollibe"

Tazama video mpya ya  Mr Fleva "Gollible" ambayo ndani kamuweka msichana anaesemekana kuwa ni girfriend wake pamoja na muigizaji kubwa Nollywood Pete Edochie 

Navy Kenzo na Quick Rocka watoa video siku moja

Wiki iliyopita Quick Rocka (mmilikiwa Switch Records) aliachia audio ya wimbo wake mpya "Bishoo" kupitia XXL, wakati Navykenzo nao waliachia siku hiyohiyo kupitia kipindi cha Lo Tena.
Quick alikuja kudhihirish akuwepo kwa kutokuelewana kati yake na Nahreal (mmoja wa Navykenzo) baada ya kuondoka studioni kwake bila kuaga) na hata kufikia kudaiana kazi walizowahi kufanya pamoja mwingine Nahreal akitaka kugawana mauzo ya wimbo wa Quick alioutengeneza "Sukido"  huku Quick akimzuia kutumia chorus ya wimbo wake huu mpya kwa madai aliandika yeye

Al Shabaab wakiri kuwaua 36 KenyaKundi la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya. Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia. Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu. Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya. Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.

 Wapiganaji wa Al Shabaab

Kundi la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia.
Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.
Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.














Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo.
Mkuu wa Polisi hilo amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa Kenya.
Basi walimokuwa wakisafiria wakenya wengine waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera wiki iliyopita
Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio hilo limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine wanne wamejeruhiwa.
Washambuliaji hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio hilo.
Wiki iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.
Kenya imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab. Mbali na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji mikubwa nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na mashambulio ya kigaidi.






Monday, December 1, 2014

Taarifa rasmi kutoka Ikulu kuhusu mabadiliko kwenye nafasi ya Mdhibiti na Mkkaguzi Mkuu wa Serikali, CAG


Kituo cha ITV kimeripoti kuhusu taarifa ya uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Tanzania, hapa nimekuwekea taarifa rasmi kutoka kwenye Website ya Ikulu Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.
Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.
Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.
Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 – 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.
Katika kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Desemba,2014

Sunday, November 30, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI LEO DESEMBA 1, 2014


KAULI MBIU: Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU, Vifo vitokanavyo na ukimwi na ubaguzi na unyanyapaa inawezekana

Je, Wewe unatumia njia gani kujikinga na maambukizi ya ukimwi?

Chanjo ya EBOLA yatoa matumaini

Watafiti wa masuala ya afya nchini MAREKANI, wamesema, majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa EBOLA yaliyofanyika nchini humo, yanaonekana kuwa ya mafanikio.

Chanjo hiyo imetengenezwa ili kuchochoea kinga ya mwili wa binadamu ili itengeneze kinga dhidi ya virusi vya EBOLA. Watafiti hao wanasema chanjo hiyo imeonyesha mafaniko, kwa vile watu waliokubali kufanyiwa majaribio, miili yao imeweza kutengeneza kinga dhidi ya EBOLA katika kipindi cha wiki nne.

Utafiti huo unaonyesha kuwa watu waliofanyiwa majaribio ya chanjo dhidi ya EBOLA, hawakupata athari hasi za chanjo hiyo. Taasi inayoshughulika na chanjo hiyo, inatarajiwa kufanya majaribio zaidi kuhusiana na chanjo hiyo mwezi ujao.

Kajaribio ya awali ya chanjo hiyo yanatarajiwa kufanyika nchini LIBERIA, ambako watu wengi wameathiriwa na EBOLA.