VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Tuesday, September 29, 2015

Ajali ya Basi la Ngorika yaua askari wa JWTZ Na Kujeruhi wengine 33



Watu wawili wamefariki dunia akiwemo askari wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na wengine 33 kujeruhiwa baada ya basi mali ya kampuni ya Ngorika kuigonga kwa mbele Toyota Costa eneo la Misugusugu mjini Kibaha .

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 1.30 asubuhi leo wakati basi hilo likitokea Dar esalaam kwenda Arusha ambapo ilipofika eneo hilo dereva alihama upande wake wa njia kuyapita magari mengine yaliyokua mbele yake bila tahadhali hivyo kwenda kugongana uso kwa uso na costa iliyokua ikitokea Miono Bagamoyo kwenda Dar esalaam.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jafari Mohamed amethibitisha tukio hilo na kutaja waliokufa ni Rutta Saimon mwalimu wa shule ya msingi Mwambao Bagamoyo na Peter Maro askari wa JWTZ na kwamba anasadikiwa kuwa ni wa Kikosi cha Jeshi la Nyumbu Kibaha na wote walikua abiria katika Costa hiyo.

Kamanda Jafari amesema kati ya majeruhi hao 33, wanne hali zao ni mbaya kutokana na kuvunjika sehemu mbalimbali za mwili.

"Majeruhi wote wa ajali hiyo walipelekwa Tumbi na walitibiwa na wengi wao wameruhusiwa kuendelea na safari yao lakini hao wanne ndiyo wamelazimika kulazwa hapo kwa matibabu zaidi kutokana na hali zao kuwa mbaya maana wamevunjika sehemu mbalimbali za mwili, na pia miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini humo kusubiri ndugu"amesema Kamanda Jafari.

Monday, September 21, 2015

MAKAMU WA RAIS MOHAMED GHARIB BILAL AHUDHURIA KUWEKWA WAKFU ASKOFU KENEN PANJA MJINI TUKUYU




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani humo leo Sept 20,2015 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule  wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Pannja zilizofanyika katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.
  
 
Wasanii wa kwaya ya Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo kuu la kusini wakitoa burudani wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Kenen Salim Panja iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya. 
 
 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na kumpongeza Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Panja wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule wa Kanisa hilo Mchungaji Kenan Salim  Panja iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mkoani Tukuyu Mkoani Mbeya.
 
 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Kenen Salim Panja baada ya kumalizika kwa Misa na Ibada maalum ya kuwekwa wakfu Askofu huyo iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu Mkoani Mbeya.

Wednesday, September 16, 2015

Kati ya Magufuli na Lowassa, ni Nani atatufaa Kwa siasa za Nje?


“Msifanye mabadiliko kwa pupa kama watu wa Libya. Walimuondoa madarakani rais Saddam, hapana rais Gaddafi maana Saddam alikuwa rais wa Kuwait!!”.

Sikuamini masikio yangu kwamba haya ni maneno yaliyotoka kinywani mwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli.

Alikuwa akiongea na wananchi wa Tanga katika mkutano wa kampeni akiwahadharisha Watanzania wasivichague vyama vya upinzani, kwa lengo la kufanya mabadiliko kwa sababu kufanya hivyo ni kuchagua bora mabadiliko wakati mabadiliko bora yatapatikana.

Nia yangu siyo kumfedhehesha mgombea huyu anayesifika kwa uadilifu na uchapakazi, lakini hivi kuna asiyejua kuwa Saddam Hussein hakuwa rais wa Kuwait bali Iraq? Kila mtu anajua hivyo, nashangaa tu kwamba mgombea wangu wa urais ama kweli hajui hili au hayuko makini katika masuala ya kimataifa.

Ninachokusudia ni kujaribu kuwahadharisha Watanzania kwamba zama hizi rais wa nchi haongozi ndani ya mipaka ya nchi hiyo pekee, bali anakuwa kiungo muhimu kati ya nchi yake na jamii ya kimataifa katika ulimwengu huu ambao sasa ni kama kijiji.

Moja ya mafanikio ya rais wa nchi yeyote ile duniani ni jinsi gani anazicheza karata zake kwenye medani ya kimataifa. Siasa za kimataifa siku hizi ni mchezo hatari, kiasi kwamba kama rais hazijui vizuri siasa za kimataifa kuna hatari ya kushindwa kutekeleza ilani na sera za chama chake awapo madarakani, kwa sababu ya misuguano na wale waitwao washirika wa maendeleo ambao ni nchi zilizoendelea.

Ukubwa wa hatari hii unazidi pale nchi yetu inapoingia katika uchumi wa mafuta na gesi asilia. Rasilimali mbili hizi zimeyaingiza mataifa yenye rasilimali hizo katika machafuko.

Kwa mujibu wa andiko, Oil and Diamonds as causes of civil war in sub-Saharan Africa, rasilimali ya mafuta na gesi zinaweza kuitia nchi katika machafuko. Lakini hilo hutegemea wingi wa rasilimali hiyo, sera na mikataba ya nchi husika kwa mataifa na mashirika wahitaji wa rasilimali hiyo kwa lugha rahisi wawekezaji.

Jingine ni uwezo wa kidiplomasia ya uchumi wa viongozi wa nchi yenye rasilimali kumudu hila, njama, migandamizo na vishawishi vya wawekezaji hao. Kwa maneno mengine, uwezo wa rais aliye madarakani katika kuongoza diplomasia na mataifa ya nje.

Mbali na rasilimali, uwezo wa rais katika diplomasia na mataifa ya nje ni mtaji muhimu katika kuvutia wawekezaji katika kile kijulikanacho kama mitaji ya moja kwa moja kutoka nje au ‘foreign direct investment (FDI)’, misaada mbalimbali kwa nchi na hata haiba ya nchi kimataifa.

Kwa kweli Rais wa Tanzania anayemaliza muda wake ameipaisha Tanzania katika medani ya kimataifa, ingawa mwishoni mwa utawala wake mataifa na wadau wa maendeleo walifikia kuzuia misaada yao kupinga kashfa mbalimbali, ikiwamo kashfa ya Tegeta Escrow iliyolitikisa Taifa.

Hatari iliyoko mkipata rais asiyejua changamoto zinazolikabili taifa katika siasa za kimataifa ni kuchukua maamuzi yanayoweza kuliingiza taifa katika hasara na hata katika migogoro ya ndani na nje.

John Perkins anaandika katika kitabu chake “The confession of an economic hitman” kwamba mashirika ya kimataifa hususan yale ya uchimbaji mafuta na gesi, huyaingiza mataifa katika lindi la madeni, umaskini na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hapo ndipo unapoonekana umuhimu wa kuwapima wagombea wetu ili kuona ni nani anafaa kwa siasa za nje?
 
 Mwandishi wa makala katika gazeti mmoja litokalo kila siku hapa nchini, alimsifia Dk John Magufuli kwamba katika kipindi chake cha miaka 20 ya utumishi serikalini, amesafiri kwenda nje ya nchi mara nne !

Hii inaonyesha kuwa si mtu mbadhirifu kwani uchache wa safari za nje unathibitisha kuwa yeye siyo mwenye kufanya matumizi ya ovyo ovyo. Japo hili ni jambo zuri kwa upande mmoja, kwa upande wa kukuza uelewa wake katika medani za kimataifa, si jambo la kujivunia. Ziara za nje hupanua uelewa wa mtu katika diplomasia ya kimataifa.

Magufuli Vs Lowassa

Kupitia hotuba zake za kampeni mtu anaweza kupata wasiwasi juu ya uwezo wa Dk Magufuli kuhusu siasa za nje. Ule mfano wake maarufu wa kulinganisha mabadiliko ya Tanzania na yale yaliyotokea Libya umetoa picha hasi kwamba hajui vyema siasa za kimataifa.

Ukichanganya na kauli yake “mimi sifanyagi (sifanyi) siasa na kwa bahati mbaya naweza kuwa si mwanasiasa mzuri,” unapata shaka kama kweli atamudu siasa za kimataifa zilizojaa ulaghai, hila na mizengwe dhidi ya nchi changa. Ili kuwa rais zama hizi, inabidi uzijue vizuri siyo siasa za ndani bali hata zile za kimataifa.

Hili la kutokujua au kujichanganya kuhusu Saddam alikuwa rais wa nchi gani linaweza kuonekana jambo dogo, lakini kwa watu makini haiwezekani kwa mtu msomi wa kiwango cha uzamili tena aliyekuwa katika uongozi wa nchi kama waziri kwa muda mrefu, awe hajui Saddam alikuwa rais wa nchi gani. Ni dalili kwamba kuna upungufu mkubwa kwenye uelewa wa mambo ya kimataifa kwa mgombea wetu huyu.

Lowassa kwa upande wake hatujamsikia akizungumzia lolote kuhusu masuala ya kimataifa, licha ya kuwa amewahi kuwa Waziri Mkuu na waziri wa kawaida kwa miaka mingi.

Nafasi hiyo bila shaka ilimpa uzoefu fulani katika medani ya kimataifa, kwa kuwa Waziri Mkuu ni msaidizi wa karibu wa rais kwenye mambo yote likiwamo la ushirikiano wa kimataifa. Aidha, Lowassa amesafiri mara nyingi nje ya nchi jambo linalompa fursa ya uelewa mpana kuhusu masuala ya nchi za nje.

Katika kampeni zake, tumemsikia akisema “sitosubiri misaada kutoka nje”. Hii ni kauli nzito kwa kuwa nchi hizi changa kama Tanzania haziwezi kabisa kuepuka misaada kutoka nje, ingawa pia hazitakiwi kuwa tegemezi kwani zina rasilimali nyingi.

Kuwa kwake Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), bila shaka kulimwezesha kukutana na wanadiplomasia wengi wa kimataifa wakiwamo mabalozi, mawaziri wakuu, makamu wa marais na hata marais waliowahi kuhudhuria mikutano ya kimataifa katika ukumbi huo.

Tukumbuke kwamba, mchakato wa Ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, utakuwa unaingia katika kipindi nyeti cha ushuru wa pamoja wa forodha na mamabo mengine ambapo masilahi ya nchi yetu itabidi yalindwe ipasavyo.

Ni wazi marais wa nchi jirani wanasubiri kwa hamu ni nani ataibuka Rais wa Tanzania, nchi ambayo ‘kistratejia’ imekaa vizuri kuliko nchi zote za Afrika Mashariki, lakini isiyokuwa na mikakati mizuri ya kufaidika na uwepo wake kijiografia.

Mataifa na mashirika ya nje kama vile Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na mengineyo yatakuwa yanafuatilia kwa karibu uchaguzi wa Tanzania. Kwa hiyo wakati tukishangilia kauli za wagombea kuhusu jinsi watakavyoendesha siasa za ndani ya nchi, tusisahau kuna siasa za kimataifa ambazo zinaweza kukwamisha hata mipango yetu ya maendeleo, iwapo rais atakayechaguliwa hatokuwa na uzoefu au uelewa wa kutosha. 
 

Tuesday, September 15, 2015

LOWASSA: Nitaanzisha Benki ya Mama Lishe na Bodaboda ili Kufuta Umasikini


MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA, Edward Lowassa, ameahidi kuanzisha benki maalumu ya  kusaidia mamalishe, waendesha pikipiki za bodaboda,  wajasiriamali wadogo ili waweze kupata mikopo na kukuza vipato vyao.
 
Bw. Lowassa aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Stendi Mjini Kahama, mkoani Shinyangana kuongeza kuwa, akiingia Ikulu ataifanya wilaya hiyo kuwa mkoa. 
 
Alisema wachimbaji wadogo wa dhahabu mkoani humo wamekuwa wakinyanyaswa na kunyang'anywa maeneo ya uchimbaji; hivyo akiwa Rais, wazawa watapewa fursa kubwa ya kuchimba dhahabu pamoja na kupewa maeneo ya kufanyia kazi hiyo. 
 
"Nimechoka na umaskini, nitahakikisha naboresha mazingira ya kilimo na kuanzisha soko huria ili wakulima wanapolima mazao yao wayauze popote ikiwemo nje ya nchi bila ushuru.
 
"Sijawahi kuona Serikali legelege kama ya CCM, naomba mnipe kura nyingi niweze kuwa rais, Serikali ambayo nitaiunda itakuwa rafiki wa watu maskini, mamalishe, waendesha pikipiki za bodaboda na wachimbaji wadogo ili nichochee maendeleo," alisema. 
 
Awali aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoani humo ambaye alihamia CHADEMA, Hamisi Mgeja, alisema Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kutekeleza ahadi zake katika mkoa huo.
 
Alisema aliahidi kupeleka umeme wa uhakika mjini Kahama, kujenga Kiwanda cha Nyama, Uwanja wa Ndege, kuongeza mtandao wa maji ahadi hizo hadi leo hajazitekeleza.
 
Naye mgombea ubunge Jimbo la Kahama kwa tiketi ya CHADEMA,Bw. James Lembeli, alimkabidhi Bw. Lowassa mfano wa ufunguo akimtaka autumie kufungua makufuli yote katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25, mwaka huu.

Tuesday, September 1, 2015

LIVE Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea


1.Napenda  kumshukuru  mwenyezi  mungu  kwa  kutujalia  uzima.

2. Nimeamua  kujitokeza  leo  hii  ili  kukomesha  upotoshaji  na  kuuweka  wazi  ukweli.


3.Sina  tabia  ya  kuyumbishwa  na  ninasimamia  ninachokiamini.

4.Sina  ugomvi  na  kiongozi  yeyote  maana  siasa  sio  uadui.

5. Siasa  inapoongozwa  kwa  misingi  ya  upotoshaji, matokeo  yake  ni  vurugu.

6. Naweka  wazi  kuwa  mimi  sikuwa  likizo  na  hakuna  mtu  yoyote  aliyenipa  likizo.

7.Kilichotokea  ni  kuwa  niliamua  kuachana  na  siasa  tangu  tarehe  28.7.2015  saa  sita  usiku  baada  ya  kutoridhishwa  na  kilichokuwa  kinaendelea  ndani  ya  chama  changu.

8.Ni  kweli  nilishiriki  kumleta  Lowassa  CHADEMA  Lakini  nilikuwa  na  misimamo  yangu  ambayo  ilitufanya  tusielewane. 

9. Baada  ya  Lowassa  kukatwa  pale  Dodoma, Gwajima  ambaye  ni  mshenga  wa  Lowassa  alinipigia  simu  kutaka  kujua  ninii  cha  kufanya.

10. Nilimpigia   Mwenyekiti    Mbowe  kumjulisha  na  tukakubaliana  kupanga  muda  wa  kuwasikiliza.

11. Kabla  ya  kuanza  kuwasikiliza, msimamo  wangu  ulikuwa  ni  kumtaka  Lowassa  kwanza  atangaze  kuhama  chama, aweke  wazi  ni  chama  gani  anaenda  na  ajisafishe  juu  ya  tuhuma  zake

12.Tangu  akatwe  jina, Lowassa  hakutangaza  kujitoa  CCM  na  wala  hakujisafisha  na  tuhuma  zake, kitu  kilichonifanya  nitofautiane  naye.

13. Niliwauliza  wanachadema  wenzangu  kuwa  Lowassa  anakuja  kama  Mtaji  au  Mzigo?

14. Swala  sio  urais  kama  watu  wanavyozusha, mimi  nilikuwa  nataka  mgombea  mwenye  uwezo  na  sifa  ambaye  ataweza  kuitoa  CCM.  Sikuwa  na  tamaa  ya  urais  kama  watu  wanavyosema 

15. Tangu  Gwajima  atupe  taarifa  za  ujio  wa  Lowassa, Swali  langu  la  Lowassa  kuwa  Mtaji  au  mzigo  halikuwahi  kujibiwa.

16. Nilitaka  kujua  ni  mtaji  gani  lowassa  atakuja  nao  na  ni  viongozi  gan  atakuja  nao.

17. Nilijibiwa  kuwa  anakuja  na  wabunge  50  wa  CCM, wenyeviti  22  wa  mikoa  na  wenyeviti  80  wa  wilaya.

18.Baada  ya  ahadi  hiyo, nilitaka  sasa  nipewe  majina  ya  hawa  watu  lakini  mpaka  tarehe  25  july  sikupewa  hayo  majina 

19. Wenzangu  waliniambia  kuwa  tarehe  27  niitishe  kikao  cha  dharura  ila  niligoma  kwa  sababu  nilikuwa  sijapewa  haya  majina 

20. Ndani  ya  kikao  hicho,  tulianza  kwa  mabishano  makali  kati  yangu  na  Mbowe, Lissu  na  Gwajima, viongozi  wenzangu  ni  shahidi  na  mungu  anajua. Msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule  kujua  mchango  wa  Lowassa 

21. Kikao  kile  kikavunjika, baadae  tukaingia  kamati  kuu  lakini  bado  msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule. Baadae  nikaandika  barua  ya  kujiuzulu.

22.Profesa  Safari  aliichana  ile  barua. 

23.Cha  kusikitisha  ni  kuwa  Kesho  yake  picha  zikaanza  kusambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  na  lowassa  japo  viongozi  wangu  walizikana  zile  picha.  Kibaya  ni  kuwa  viongozi  waliuficha  ukweli 

24.  Kesho  yake  niliandika  tena  barua  rasmi  ya  kujiuzulu. 

25. Baada  ya  pale  zikaanza  propaganda  za  uongo  zikimuhusisha  hadi  mke  wangu  eti  kanizuia.

26. Naomba  watanzania  wajue  kuwa  mke  wangu  hakuwahi  kunizuia  kwa  lolote, lkn  hata  angefanya  hivyo  sio  mbaya  maana  hata  yeye  ni  mwanaharakati  mwenye  uchungu  na  nchi  hii. 

27. Mke  wangu  aliwahi  hadi  kuumia  wakati  akipigania  ukombozi  wa  nchi  hii.....Lakini  sio  mbaya, familia  yangu  imezoea  propaganda. 

28. Kikubwa  katika  harakati  ni  credibility  ambayo  lazima  uilinde  na  mimi  sitaki  jina  langu  liharibiwe  na  ni  haki  yangu.

29. Maslah  mapana  ya  taifa  ndiyo  yaliyotufikisha  hapa  na  sio  maslahi  binafsi. 

30.Lowassa  na  wapambe  wake  ni  waongo  maana  hakuna  hata  kipengele  kimoja  walichokitekeleza.

31. Tulitaka  hao  wabunge  50  waje  kwanza  kabla  ya  mchakato  wa  uteuzi  ccm

32. Napinga  kuchukua  makapi  ya  CCM  na  kuyaita  MTAJI.

33.Mtu  kama  Sumaye  ni  FISADI  na  nilikuwa  siongei  naye 

34. Sumaye  aliwahi  kusema  CCM  wakimchagua  Lowassa  atahama  chama. Leo  Lowassa  kawaje  msafi?? 

35. Tulitaka  Mtaji  toka  kwa  Lowassa  na  sio  MAKAPI 

36. Wenyeviti  walioletwa  na  Lowassa  ni  MIZIGO  na  namjua  vizuri. Akithubutu  kunijibu  ntamwaga  UOZO  wake  wote 

37.Nani  asiyejua  Guninita  pia  ni  mzigo??

38:  Nawataka  viongozi  wangu  wanijibu  ni  mtaji  upi  walioupata  toka  kwa  Lowassa.

39. Mimi  ni  Padri  Mstaafu, sipendi  siasa  za  uongo. 

39. Ukisema  unataka  kuiondoa  CCM  ni  lazima  ujikumbushe  misingi  ya  CHADEMA  ambayo  ilikuwa  ni  uadilifu. Leo  chadema  hii  ina  Uadilifu  gani?? 

40.  Namshangaa  sana  Lowassa  eti  kusimama  mbele  ya  watu  akijinasibu  kuwa  ni  msafi.....kwamba  mwenye  ushahidi  aende  Mahakamani. Ni  dhambi  kupotosha  watu.

41. CCM    hawana  ujasiri, ni  waoga  na  ndiyo  maana  wamewalea  watu  kama  akina  Lowassa 

42. Ukitoa  kinyesi  chooni  na  kukipeleka  Chumbani  maana  yake  hata  chumba  chako  ni  CHOO  na  kitakuwa  kinanuka  zaidi  kuliko  choo  cha  kawaida 

43.Mimi  nilikuwepo  wakati  sakata  la  Richmond  likijadiliwa.Mimi  nina  ugomvi  wa  muda  mrefu  na  Lowassa.

44.  Mwaka  2010  mimi  nilimtaka  Lowassa  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.

45. Leo  tena  namtaka  Lowassa   Lowassa  atoke  hadharani  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.  Unaposema  ni  ya  mkubwa, atuambie  mkubwa  gani

46. Ukitaka  kuijua  Richmond  rejea  Ripoti  ya  Mwakyembe. Nampongeza  Mwakyembe  na  Sitta  kujitokeza  hadharan  kuusema  ukweli.

47. Siku  moja  kabla  ya  ripoti  kusomwa, nililetewa  Rushwa  ya  milioni  500  ili  tukaupindishe  ukweli  bungeni  lakini  nilikataa 

48. Ripoti  ya  mwakyembe  iliamua   mambo  mawili,  moja; Lowassa  ajipime  au  bunge  lijadili  na  lichukue  hatua.  Lowassa  kuona  hivyo  akaamua  kukimbilia  kujiuzulu  kukwepa  aibu  ya  kung'olewa  na  bunge 

49:  Lowassa  haaminiki, ni  muongo  na  hastahili  kuwa  Rais  wa  nchi....

50.  Lowassa  ni  FISADI  na  kama  mimi  ni  muongo  ajitokeze  hadharani  akanushe

51. Anasema  Lowassa  ataleta  maji, mbona  jimbo  lake  la  Monduli  halina  Maji???

52.  Mnasema  Lowassa  kaanzisha  shule  za  kata, iv  mjua  msingi  wa  shule  za  kata?  waandishi  rudini  shule  mkajifunze  upya.

53.Nilifanikiwa  kuijenga  Chadema  na  ikawa  tumaini  jipya  la  watanzania.....Vijana  wangu  wa  Chadema, naomba  niwe  mkweli  propaganda  imekivamia  chama.

54.  Inasikitisha  kuona  CHADEMA  inajazwa kwa mabasi  pale  jangwani .....alafu  mnawadanganya  watu  eti  ni   MAFURIKO

55.  CHADEMA  ya  kipindi  changu  ilikuwa  inakemea  Rushwa. Niambien  leo  chadema  watasema  nini  kwenye  majukwaa? 

56. Mnaomtetea  Lowassa  na  nyie  jitokezen  hadharani...mimi  nasema  kwa  sababu  nina  ushahidi  na  sio  lazima  ushahidi  huu  niupeleke  mahakamani.

57. Wenye  uwezo  wa  kumpeleka  Lowassa  Mahakamani  ni  Serikali, na  mwakyembe  alisema  juzi  kuwa  kesi  ya  jinai  haina  kikomo, mtu  anaweza  kushitakiwa  muda  wowote 

58. Sitaki  kuingila  swala  la  Babu  Seya, lakini  waliolawitiwa  ni  watoto  waliokuwa  chini  ya  umri. kwa  nini  haki  yao  ipotee?

59.  Rais  hana  mamlaka  ya  kumtoa  Babu  Seya. Lowassa  asiwadanganye.

60.  Kuhusu  swala  la  Masheikh, Sumaye  ndiye  aliyeamuru  mapolisi  wavamie  misikiti  wakiwa  na  mbwa......Watanzania  msikubali  kudanganywa. hizo  ni  propaganda  za  wasaka  urais 

61. Masikubali  Rais  Muongo  na  mimi  naapa  ntapiga  kelele  kila  kona  kumpinga  Lowassa.

62.Lowassa  alipokuwa  waziri  mkuu, matatizo  yanayotokea  leo  hayakuwepo?  mapigano  ya  wakulima  na  wafugaji  hayakuwepo?

63.  Lowassa  akiwa  waziri  mkuu  alisababisha  migogoro  mizito  sana  kati  ya  monduli  na  karatu.  Rais  wa  aina  hii  wa  nini?

64.  Naomba  nisiongee  mengi  kwa  sababu  ntakosa  ya  kusema  siku  nyingine.....Nawataka  Lowassa  na  Sumaye  wajitokeze  kunijibu.

65. Siku  nyingine  ntakuja  kuongelea  kuhusu  hisa  za  Lowassa  kwenye  makampuni 

66.  Nahitimisha  kwa  kusema  kuwa  Nimestaafu  siasa  na  sina  chama  lakini  nina  nchi, hivyo  ntaendelea  kuwatumikia  watanzania  kwa  jinsi  mungu  alivyonipa  vipawa 


67.  Narudia  tena, Sina  chama  na  sitajiunga  na  chama  chochote. 

Waandishi  wanauliza  Maswali: 
Mwandishi:  Umesema  hujiungi  na  chama  chochote, utawasaidiaje  watanzania?  Rais  gani  unamuunga  mkono?

Mwandishi  Guardian:  Ulisema  Lowassa  atakuwa  assert  kama  atakuja  na  wabunge  na  hao  wenyeviti.  Je  angekuja  kama  assert  ungeyasema  haya  yote?

Mwandishi  binafsi:  Umesema  waliohamia  Chadema  ni  makapi.  Mwaka  1995  Uliihama  CCM,   ukahamia  chadema. Je  na  wewe  ni  KAPI?

Mwandishi-Azam:  Umetangaza  kustaafu  siasa, lakini  bado  unakadi  ya  CCM  na  CHADEMA?  Je  utazirudisha?

Mwandishi  Blog:  Inaonekana  baada  ya  chedema  kukutosa  ndo  maana  unamshambulia  Lowassa, je  ni  kweli?

Majibu:
1. Kadi  ni  mali  zangu  na  siwezi  kuzirudisha. Ya  chadema  nimeilipia  miaka  20,ya  CCM  bado  haijaisha  muda  wake.

2. Kuhusu  urais, mimi  sijagombea  urais  na  sikuchukua  fomu.  sasa  kwa  nini  nikasirike  kisa  wamempa  Lowassa?
Sina  ugomvi  na  Mbowe  na  nakumbuka  alinisaidia  nyumba

3.  Mimi  sio  KAPI....Ili  kuujua  ukweli  unahitaji  kutumia  kigezo. KAPI  ni  yule  aliyekataliwa  na  chama  flani, mimi  sikuwahi  kukataliwa.  Sikuwa  na  uchafu  wowote  wakati  naingia  CCM.

4.  Lowassa  ni  mzigo  tu  hata  kama  angetuletea  hao  watu  wake.....Lowassa  ana  makandokando  mengi. Angetuletea  hao  watu  ndo  tungeamua  tumpokee  au  tusimpokee

5.Mimi  sina  chama  na  sitampigia  kampeni  mtu  yeyote. Mimi  nimefanya  utafiti  kwa Lowassa  pekee, kwamba  taifa  litapata  madhara  gan  Lowassa  akiwa  Rais.....Lowassa  ni  Fisadi.
 
 -Kazi  yangu  leo  ilikuwa  ni  kuwaambia  watanzania  waachanane  na  ushabiki.Ukihamishia  CHOO  chumbani, manake  harufu  itahamia  huko.
 -Chadema  ya  leo  kwa  sasa  imetekwa  na  Lowassa  na  hawawezi  tena  kuongelea  Ufisadi 

Maswali  ya  nyongeza

1.Umesema  waliohamia  chadema  kwa  sasa  ni  sawa  na  mfano  wa  Choo. Je, wewe  ulipohama  hukuwa  choo?  kwa  nini  wewe  uliweza  kukibadili  chama  halafu  akina  Lowassa  washindwe?

Jibu:  Wakati  mimi  nahama  sikuwa  mchafu  kama  hawa  akina  Lowassa  na  Sumaye.