VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Tuesday, December 30, 2014

NYALANDU ATANGAZA KUGOMBEA URAIS 2015



Pg 3.

Na Kulwa Karedia, Singida

MBIO za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimechukua sura mpya baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kutangaza rasmi nia ya kugombea urais mwaka 2015.

Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wapigakura wake kwenye uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Ilongero, Wilaya ya Singida Vijijini jana, Waziri Nyalandu alisema muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika.


“Muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika, nitachukua hatua ya kuelekea Dodoma kuchukua fomu muda ukifika, maelfu ya watu watanisindikiza, wanawake, vijana kutoka mikoa mbalimbali.


“Naita zama mpya, siku ambayo ndoto yangu itakamilika, Mungu atanyanyua vyombo na kushangaza wakubwa. Najua tulikuwa wadogo kama Nazareti, lakini Ilongero imekuwa na mchango mkubwa ambao utakuwa si faida kwa wana Singida tu, bali taifa zima la Tanzania,” alisema Waziri Nyalandu.


Alisema kila mtu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais ndani ya CCM, lazima kazi zake zipimwe kwa moto.


“Wale wote waliotangaza nia ndani ya chama chetu, kazi zao lazima zipimwe kwa moto na zianikwe hadharani ili mwisho wa siku CCM yenyewe itazipima,” alisema.


Alisema pindi Rais Jakaya Kikwete atakapohitimisha utawala wake, lazima atakabidhi kijiti kwa kizazi kipya.


“Nina uhakika mheshimiwa Rais Kikwete akiondoka madarakani, lazima akabidhi kijiti kwa kizazi chenye fikra… zama za kusimama na kuchukua vijiti zimefika.


“Mwaka 2015, sisi ndani ya CCM tunatarajia utakuwa mwaka wa mabadiliko na fikra mpya.


“Tuna wajibu wa kubadili fikra zetu, watu wasimamie Tanzania kuchukua hatua, licha ya ukweli kwamba CCM tuna utaratibu na itikadi zetu, tumeondoa zuio kwa vijana wasiwe waoga… tumejipanga kuwashangaza wengi,” alisema Waziri Nyalandu.


WAPINZANI
Alisema muda wa kuwashangaza wengi unaanzia kwa vyama vya upinzani, vikiwamo Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).



“Katika safari ya miaka 15, Mungu ametusaidia kusonga mbele, safari moja huanzisha nyingine, nawaomba tusonge tena kwa hatua nyingine, mlianzisha safari yangu ya kisiasa, nilikuwa kama mzabibu uliotoa matunda, mkaniita ‘Mwanyengu’, maana yake mtoto wa tai la kuishangaza dunia. 


Safari hii imekuwa ya milima na mabonde lakini kwa pamoja tumeweza, Mungu ameona, Kikwete ameona sawasawa,” alisema.

VIONGOZI WAZEE
Alisema viongozi wastaafu waliotawala taifa hili wanapaswa kupewa heshima zote.


“Tunatambua mchango wa wazee wetu walioutoa, wana haki ya kuheshimiwa, lakini zamu ya vijana imefika. 


Vijana tunataka taifa litakaloleta siku njema, ni wajibu wetu tuwatunze ndiyo maana kupitia kwao maisha yetu yamebadilika,” alisema.

Alisema bado anawapenda mno wananchi wa jimbo lake, lakini safari waliyoianza mwaka 2000, lazima waikamilishe.


“Nalipenda jimbo langu, wapiga kura wangu, lakini tuungane kukamilisha safari hii tuliyoianza miaka 15 iliyopita,” alisema Waziri Nyalandu.


ATOA MAMILIONI
Baada ya kuwasili katika Kijiji cha Ilongero, Nyalandu alikwenda moja kwa moja katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ilongero ambako alishiriki misa na kuchangia Sh milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.


Katika misa hiyo, alipewa nafasi ya kuzungumza na kusema eneo hilo ni la ushindi kwake.


Pia alitembelea Kanisa la FPTC-Tanzania ambako nako alitoa msaada wa Sh milioni 10 na kiasi kama hicho alitoa kwenye msikiti.


Katika mkutano huo, Nyalandu aliambatana na mke wake Faraja Kota, watoto wake Christopher na Serafine na wazazi wake.

Monday, December 29, 2014

Ivo Mapunda agoma kukaa golini Simba



 

Ivo ametoa kauli hiyo baada ya mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba ilifungwa bao 1-0 yeye akiwa langoni. KIPA Ivo Mapunda ametangaza rasmi kwamba anaondoka Simba na amemtaka kocha wake, Patrick Phiri, asimpange tena katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara kwani amechoka kutuhumiwa kuwa anaihujumu timu.
Ivo ametoa kauli hiyo baada ya mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba ilifungwa bao 1-0 yeye akiwa langoni. Mashabiki wamemlalamikia kuwa alifungwa bao hilo kizembe.
Ivo aliliambia Mwanaspoti kuwa hataki tena kukaa langoni katika mechi za Simba za ligi na nyinginezo kwani imani ya mashabiki kwake imepotea kwani hata akifungwa katika mazingira ya kawaida haeleweki.
“Nafanya kazi katika mazingira magumu mno, sina raha wala amani ndani ya timu, kila mechi nikidaka lazima nilaumiwe sasa kuna haja gani ya kuendelea kusimama langoni? Nitazungumza na kocha asinipange tena kudaka mechi zilizobaki, nataka nikae benchi,” alisema Ivo.
Hii ina maana Simba itapaswa kumtumia kipa chipukizi Manyika Peter katika mechi dhidi ya Mgambo JKT Jumapili wiki hii jijini Tanga.
KIPA Ivo Mapunda ametangaza rasmi kwamba anaondoka Simba na amemtaka kocha wake, Patrick Phiri, asimpange tena katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara kwani amechoka kutuhumiwa kuwa anaihujumu timu.
Ivo ametoa kauli hiyo baada ya mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba ilifungwa bao 1-0 yeye akiwa langoni. Mashabiki wamemlalamikia kuwa alifungwa bao hilo kizembe.
Ivo aliliambia Mwanaspoti kuwa hataki tena kukaa langoni katika mechi za Simba za ligi na nyinginezo kwani imani ya mashabiki kwake imepotea kwani hata akifungwa katika mazingira ya kawaida haeleweki.
“Nafanya kazi katika mazingira magumu mno, sina raha wala amani ndani ya timu, kila mechi nikidaka lazima nilaumiwe sasa kuna haja gani ya kuendelea kusimama langoni? Nitazungumza na kocha asinipange tena kudaka mechi zilizobaki, nataka nikae benchi,” alisema Ivo.
Hii ina maana Simba itapaswa kumtumia kipa chipukizi Manyika Peter katika mechi dhidi ya Mgambo JKT Jumapili wiki hii jijini Tanga.


Sunday, December 28, 2014

Feri ya abiria 460 yashika moto Ugiriki

Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na karibu abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki kwenda Italia.
Abiria waliokuwa kwneye ferry hiyo walipiga simu kwa vituo vya runinga nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na upepo unatatiza shughuli za uokoaji.
Maafisa wa ulinzi wa pwani nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman Atlantic ilikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati walipotuma ujumbe .
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari.

Ndege ya AirAsia yapotea na abiria 160

Shirika la ndege la AirAsia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.
Zadi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.
Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

Thursday, December 25, 2014

SUPERSTAR WA BONGO MOVIE AFUMANIWA NA MKE WA MTU NA HIKI NDICHO ALICHOFANYIWA




Wakati wengine wakisheherekea sikukuu ya Christmass duniani kote ikiwa ni kumbukumbu kwa wakristo wote kuzaliwa kwa Mwokozi wao "YESU" Wengine siku hiyo wanaifanya kuwa siku ya starehe na kufanya mambo kinyume na maana ya siku yenyewe. Msanii wa filamu za bongo maarufu kwa jina la Pancho Mwamba, anadaiwa kufanyiwa mbaya baada ya fumanizi siku ya Xmass. Msanii huyo inasemekana amefumaniwa na mke ambaye si wake siku ya Christmass maeneo ya Kinondoni jijini hapa.


Patcho Mwamba Lukusa ni muimbaji, Mtunzi, Composer, Music 
Arranger, Mchezaji, Mchekeshaji na ni muigizaji wa 
cinema. Patcho amejitokeza kucheza vizuri katika tasmia nzima ya 
sinema huku ajijizolea umaarufu kama mwanamuziki huyu toka 
kundi la FM Academia wana Ngwasuma ameweza kujizolea sifa kem kem toka kwa mashabiki wa Dollywood

Tuesday, December 23, 2014

Sakata la Escrow

Nchini Tanzania mtikisiko wa matokeo ya kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow umeendelea baada ya Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yake. Maswi anakuwa kiongozi wa tatu wa ngazi ya juu kukumbwa na upepo huo akitanguliwa na Mwanasheria mkuu wa serikali ambaye alijiuzulu mwenyewe na Waziri wa Ardhi aliyetimuliwa kazi hadharani na Rais Jakaya Kikwete. Licha ya kuondoka kwa viongozi hao bado baadhi ya wananchi na vyama vya upinzani wameendelea kulalamika kuwa juhudi za kutekeleza maazimio ya Bunge ni ndogo. Kuhusiana na hilo Baruan Muhuza wa BBC alizungumza na Neville Meena, katibu wa Jukwaa la wahariri Tanzania.

Sunday, December 21, 2014

UJENZI WA MABWENI SHULE ZA PEMBEZONI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WANAFUNZI MIJINI



Jamii imetakiwa kuendelea  kuunga mkono juhudi za Serikali za ujenzi wa mabweni katika shule  za Sekondari  zilizoko pembezoni mwa miji hasa maeneo ya vijijini ili kukabiliana na tatizo la msongamano wa wanafunzi mijini linalosababishwa na baadhi ya wanafunzi kushindwa kujaza nafasi wanazopangiwa   maeneo ya pembezoni mwa miji kutokana na umbali.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni jijini Dar es salaam na Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando wakati akizungumza na viongozi wa Elimu wa mkoa na walimu wakuu wa Shule za Sekondari za mkoa wa Dar es salaam wakati wa kikao cha Kamati ya Uchaguzi wa wanafunzi wa watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015.
Alisema  mwaka huu  mkoa wa Dar es salaam umekuwa na kiwango cha juu cha ufaulu  kitaifa kwa kuwa na wanafunzi wanaokidhi vigezo vya kuendelea na masomo ya sekondari kwa kiwango cha asilimia 78 ukifuatiwa na mkoa wa Kilimanjaro ambao umepata asilimia 69.
Alifafanua kuwa kati ya wanafunzi 60,709 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu , wanafunzi 59,577 ambao ni sawa na asilimia 98.14  waliofanya mtihani huo, wavulana wakiwa 28,419 na wasichana 31,158.
Bi. Mmbando alibainisha kuwa  kati ya hao watahiniwa 1,132  sawa na asilimia 1.86 katika mkoa wa Dar es salaam hawawakuweza kufanya mtihani huo kutokana sababu mbalimbali zikiwemo utoro, vifo, ugonjwa na sababu nyinginezo.
Akizungumzia  kuhusu ufaulu wa wanafunzi hao kimkoa alisema wanafunzi 46,434 sawa na asilimia 78 walifaulu mtihani huo na kuufanya mkoa wa Dar es salaam kuongoza kwa kuwa na ufaulu wa juu kitaifa wavulana 22,389 na wasichana 24,086.
Alibainisha kuwa wanafunzi 36,610 walichaguliwa katika chaguo la kwanza kujiunga na shule mbalimbali za Sekondari za ndani na nje ya mkoa wa Dar es salaam na kufafanua kuwa wanafunzi 9824 waliobaki sawa na asilimia 21 ambao nao wamefaulu watachaguliwa katika chaguo la pili kufuatia baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa katika chaguo la kwanza kujiunga na shule zisizokuwa za serikali na nafasi zao kubaki wazi.
Katika kufanikisha zoezi hilo Bi. Mmbando alieleza kuwa mkoa tayari umeunda timu tatu zitakazofuatilia idadi ya wanafunzi watakaoshindwa kufika katika shule walizopangiwa  kuanzia Januari 14, 2015 katika halimashauri za Temeke, Ilala na Kinondoni ili nafasi zao zijazwe na wanafunzi wengine.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Raymond Mapunda akitoa tathmini ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika nchi nzima mwezi Septemba mwaka huu alisema mkoa wake ulifanya vizuri kutokana na juhudi za walimu pamoja na wanafunzi kuuelewa vizuri mfumo wa ufanyaji mitihani uliotumika wa Optical Mark Reader (OMR).
Alisema kuwa wanafunzi wa shule 506 za jiji la Dar es salaam walifanya mtihani walitumia mfumo huo kwa ufanisi mwanafunzi 1 alifutiwa matokeo yake kwa sababu za udanganyifu, 2 walipata alama 0  huku  wavulana 10 na wasichana 10 kutoka wilaya ya Ilala na Kinondoni waliibuka washindi wa nafasi 10 bora kitaifa.

WEKA MAONI YAKO HAPA

Friday, December 19, 2014

A.Y Atoboa Siri ya Kupiga Collabo na Wasanii wa Kimataifa




Baada ya kupiga Collabo na Miss Trinity katika studio za B-Hits, weekend hii Ambwene Yesaya a.k.a A.Y amefichua siri ya kupiga Collabo na Wasanii mbalimbali wa kimataifa wanaoshuka bongo kila kukicha. A.Y ameyasema hayo baada ya kuulizwa na swali 255 kwamba ni mbinu gani anayoitumia katika kumshawishi mtu kama Sean Kingston, P-Square, Miss Trinity, K-Naan na wengineo.

Ambwene akajibu kuwa siri yake ya mafanikio hayo ni kujitangaza sana kupitia vyombo mbalimbali vya habari kadri inavyowezekana, so anapokuja msanii kutoka nje Tayari wanakua wameshafanya utafiti wa kujua ni msanii gani mkali au anayejulikana nchini Tanzania.

Ambwene pia amezungumzia Collabo yake na Sean Kingston ambayo walishindwa kuifanya hapa bongo na meneja wa Kingston akamshauri Ambwene kuwa ili aweze kujitangaza zaidi ni bora aende kurekodi nchini marekani kwani atapata fursa ya kukutana na wataarishaji wa muziki wa kimataifa lakini pia kazi atakayofanya na Kingston itakua yenye ubora.

A.Y yuko mbioni kwenda katika mji wa Miami nchini marekani kurekodi ngoma na mtu mzima Sean Kingston.

Lakini pia kesho A.Y anaelekea jijini Kampala kupiga Video ya ngoma aliyorekodi na Miss Trinity.

Monday, December 15, 2014

Nywele za mwanamke zashika moto wakati akizima mshumaa siku ya birthday yake


 
Hii imetokea huko Marekani! Mwanamke mmoja Shelley Meyer amejikuta sherehe yake ya siku ya kuzaliwa ikigeuka kilio baada ya nywele zake kuteketea kwa moto wakati akizima mishumaa kwenye keki yake.

 

 

 

Mwanamziki mkongwe Shem Kaengaa afariki dunia


Marehemu Shem Ibrahim Karenga enzi za uhai wake.
Chumba cha habari cha Globu ya jamii,imepata taarifa za kuaminika kutoka kwenye chanzo cha karibu kuhusiana na Msiba wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,

 

 

 

Shilole aachia ngoma yake mpya kwenye Leo Tena iitwayo Malele


Msanii wa Bongo Fleva,Shilole akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena,Husna Abdul wakati akiachia ngoma yake mpya iitwayo Malele.

Iggy Azalea Ajibu Tuhuma Kwamba Alizaliwa Mwanaume Na Aliitwa Cody.



Rappa wa Iggy Azalea ametumia kurasa yake ya Twitter kujibu tuhuma kuwa alizaliwa mwanaume n jina lake lilikuwa Cody. Ijumaa jioni Iggy aliweka hizi post nakufanya watu wacheke na wengine wakijiuliza hii interview aliyofanyiwa mpaka kukiri mambo haya ilitokea lini.

 

Kourtney Kardashian ajifungua mtoo wa kiume


Baada ya zile picha za Kourtney Kardashian kupiga huku akiachia tumbo lake lilokuwa na kiumbe ndani yake sasa amejifungua mtoto wa kiume ambaye baba wa mtoto anajulikana kama Scott Disick na hii ni kwa mujibu wa mtandao mkubwa wa burandi wa

Sunday, December 14, 2014

Watu kadhaa wanashikiliwa mateka Sydney

 mgahawa wa Lindt ambao tukio la utekaji limefanyika
Watu kadhaa wanashikiliwa mateka na mtu mmoja au zaidi wenye silaja katika mgahawa wa Lindt mjini Sydney, Australia.
Mamia ya Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira eneo lilipotokea tukio hilo.
Takriban watu watatu wameonekana ndani ya mgahawa wakiwa wamenyanyua mikono juu wakiwa wameiegesha kwenye dirisha wakiwa wameshika bendera nyeusi ikiwa na maandishi ya kiarabu.
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbot amesema tuki hilo linahuzunisha sana.
Abbot amesema haijajulikana nani alihusika na tukio hilo hata hivyo anahisi huenda ni njama za kisiasa na kuwa tayarikamati ya usalama ya taifa imepewa taarifa.
Kamishna wa Polisi wa South Wales Andrew Scipione amesema tukio hilo halichukuliwi kuwa la kigaidi lakini imethibitishwa kuwa kuna mtu mwenye silaha anayewashikilia mateka watu kadhaa.
Mashahidi wa tukio hilo wamesema walimuona mtu akiwa na begi na silaha akiingia kwenye mgahawa, polisi wamefunga eneo hilo, barabara na kuwaondoa watu katika eneo hilo.

Friday, December 12, 2014

Chadema kupinga uchaguzi wa mitaa leo


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro, kimepitisha azimio la kwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu, hadi hapo Tamisemi itakapotoa haki ya kurejeshwa kwa wapiga kura 517 na wagombea wake 52 walioenguliwa.

Azimio hilo la Chadema la kupinga uchaguzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, limetolewa wakati zikiwa zimebaki siku nne tu, uchaguzi huo ufanyike nchini kote.

Katibu wa Chama hicho mkoani hapa, Basil Lema, alisema tayari wamemwagiza Mwanasheria wao kuandaa hoja za kisheria kisha kufungua kesi ya kupinga uchaguzi huo leo kutafuta haki ya wananchi na wagombea wa nafasi mbalimbali walioenguliwa, hivyo kuwakosesha kutimiza haki yao ya kikatiba.

“Jumla ya wagombea 52 wa nafasi mbalimbali wanaotokana na Chadema mkoa wa Kilimanjaro, wameenguliwa kwa makusudi kutokana na kasoro zilizopo kwenye fomu ya kuomba uongozi, lakini pia wamo wapiga kura 517 walioenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi kwa madai ya kuwa si wakazi halali na wengine wakitajwa kuwa si raia. Tunaamini wapo wanaoonewa,” alisema Lema.

Katika Kata ya Mawenzi mjini Moshi, wananchi 159 kati ya 162 waliojiandikisha kupiga kura, wameenguliwa baada yakudaiwa kwamba siyo wakazi halali wa eneo hilo. Aidha, kwenye kundi hilo la wanaodaiwa kuwa si wakazi, imo familia ya watu wanne ya Diwani wa Chadema, Hawa Mushi.

Kwa mujibu wa Lema, hali ni mbaya zaidi katika Jimbo la Same Magharibi, kwa kuwa kwenye Kata tatu zenye jumla ya wagombea wake 21 walioomba uongozi wameenguliwa wote na hivyo kutoa mwanya kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupita bila kupingwa.

“Kwenye jimbo hilo hilo, wananchi 180 wa Kijiji cha Marwa, Kata ya Ruvu wameenguliwa baada ya kujiandikisha kwa madai kwamba wao si wakazi wa eneo hilo. Hizi ni rafu ambazo wenzetu CCM wanatuchezea Ukawa ili kuuhadaa umma kwamba Muungano wetu hauna tija kisiasa,” alisisitiza Katibu huyo.

Nguo za ndani zinazowalinda wanaume



Nguo hizi za ndani zinasemekana kuwa na uwezo wa kulinda wanaume kutokana na madini hatari yanayoathiri nguvu za kiume
Kampuni ya Belly Armor, ambayo ilikua ya kwanza kutengeza bidhaa zinazohitajika na wanawake wajawazito, kutokana na kitambaa maalum kinacholinda mwili kutokana na athari za madini ya chuma mwilini, imeanzisha biasharta nyingioenkwa manufaa ya wanaume.
Kampuni hii imeanza kutengeza nguo za ndani za wanaume ambao zinawalinda kutokana na athari ya madini ya chuma yanayoweza kupunguza nguvu za kiume na kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume hali ambayo inaweza kusababisha mwanaume kukosa kuzalisha.
Unaweza kujiuliza je biashara ya kutengeza vitambaa hivyo inanawiri? Jibu? Ndio tena sana.
Mbegu za wanaume zinaweza kuthiriwa na madini yanayotumiwa kutengeza simu za mkononi
Mnamo mwaka 2011, shirika la afya duniani lilitaja madini hayo hatari ikiwemo miale inayotokana na simu za mkononi kama yenye uwezo wa kusababisha saratani ya ubongo mbali na athari nyinginezo hatari kwa mwili kiafya.
Kwa mfano, watumjai wa Iphone, je mlijua kama mnapaswa kuzibeba simu zenu umbali wa milimita 10 kutoka kwa mwili wako kuhakikisha kuwa madini hayo hayaathiri mwili?
Licha ya kwamba utafiti mpya unahitajika kuthibitisha hili....ni wazi kwamba madini fulani yanayotumika kutengeza simu yanaweza kusababisha aina ya saratani za mwilini.
Na ndio maana kampuni ya Belly Armor ikaja na wazo la kuwatengezea wanaume nguo za ndani zinazoweza kuwakinga kutokana na athari hizo.
Pia utafiti ambao umefanywa unaonyesha kua baadhi ya miale inayotokana na vifaa kama vile simu za mkononi, Tabiti au Ipad, inaweza kusababisha mwili wa wanaume kupungukiwa na nguvu za kutengeza mbegu za kime au hata mwili kuishiwa na nguvu za kiume.

Wednesday, December 10, 2014

Kilio cha Albino Tanzania

Wanachama wa chama cha maalbino wakitembelea kisiwani ambako wanaishi walemavu wa ngozi
Mtobi Namigambo, ni mvuvi anayeuza samaki, amekaa kwa utulivi nje ya nyumba yake ya matope katika kisiwa cha ukerewa mahali ambapo zamani palikuwa makao ya albino lakini kwa sasa si hivyo. Mtoto wake wa miaka nne May Mosi ameketi kwenye paja lake akionyesha umarufu wake wa hisabati kwa kuhesabau moja hadi kumi kwa ujasiri.
Mara kwa mara Mtobi anamtazama mke wake, Sabina, ambaye ameketi kwa mkeka kando yake akitayarisha chakula cha jioni. Watoto wake wengine wawili wanachezea hapa karibu na pia wamejaliwa na mtoto mchanga amabye yuko chumbani analala.
May alipokuwa na umri wa miezi mitatu, aliponea jaribio la kutekwa nyara.
Albino wanauawa kinyama kwa ajili ya imani potovu
" nilikuwa nimeenda ziwani kuvua samaki. walikuwa pekee yao nyumbani wavamizi walipokuja, mke wangu alitorokea kwa dirisha na kukimbillia usalama akiwa na May, na akawawacha watoto hawa wawili nyumabani ambao hawakuwadhuru kabisa", Mtobi ananiarifu.
"Wavamazi hao walikuwa wakimtaka May," Sabina anaongezea, "mume wangu alikuwa ameenda safari ya uvuvi na wavamizi hao walijua na hio ndio sababu walikujia mtoto wangu, baada ya kutorokea kwa dirisha, bado waliniandama huku nikipiga mayoye ya usaidizi, waliwacha kuniandama wakati tu niliwaamsha majirani"
May ni mojawapo wa Albino sabini wanaoishi katika kisiwa hiki cha Ukerewa ambacho ni masaa matatu tu kutoka mwanza, mji wa pili mkubwa zaidi Tanzania.
Elimu kwa jamii
Mtobi anasema "tunaiomba serikali kufanya juhudu zaidi za kuelimisha jamii hapa, serikali ishawahi kuandaa majadiliano kuhusu Albino na kulikuwa na mabadiliko makuwa, akini si hivyo tena"
Shirika lisilo la kiserekali chini ya mrengo wa 'The Same Sun' linalowashughulikia jamii ya Albino hapa Ukerewa, linasema kuwa kisiwa hiki hakina usalama kando na vile watu wangependa kuamini.
Idadi ya maalbino waliouawa ni kubwa na kuna hofu ya wengine wengi kuuawa kutokana na imani potovu
Mwenye kiti wa chama cha maalbino tawi la Mwanza, (TAS) Alfred Kapole, mzaliwa wa Ukerewe, alilazimika kutorokea mji wa Mwanza akiwa mmoja wa albino wa kwanza kufika kortini baada ya kiognozi mmoja wa kijiji akitaka kumuua kwa ajili ya nywele zake.
Mwaka uliopita boma lake lilivamiwa, kwa bahati nzuri alikuwa ameenda mwanza. Kulikuwa na jairibio lEngine la kumuua mwaka huu.
Kampeni kabambe
Serikali ya Tanzania imeanzisha kampeni ili kuchangisha fedha za kuelimisha jamii.
Kampeni nyingi za uhamasishaji hufanyika mijini kwani ni rahisi kufikia watu,lakini ni vijiji ndivyo vinahitaji msaada zaidi.
Ramadhan Khalfan, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha albino Ukerewa,anasema kuwa wanataka kufikia maeneo ya vijiji na kuzungumza na watu,lakini ni vigumu kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha.''Hatuna uwezo ama njia za kufikia jamii zilizoko vijijini.Aliongezea kusema,''tunategemea pakubwa redio na televisheni,lakini hatuwezi kufika mashinani kwa sababu ya gharama.''
Mnara unaowapa matumaini watanzania Serengema
Sehemu ya Serengema inapatikana kilomita 60 (maili 33.5) kutoka Mwanza.Ili kusisitiza shida hii,umejengwa mnara katika mzunguko katikati ya mji.
Ni sanamu ya chuma kimo cha binadamu,inayoonyesha baba mwenye rangi akimbeba begani mto wake albino huku mama yake mwenye rangi akitundika kofia yenye ukingo mpana kwenye kichwa cha mwana huyo kumkinga kutokana na miale ya jua.Pia kuna majina ya watu 139 ya waathiriwa waliouawa,kuvamiwa ama miili yao kuibiwa kutoka kwenye makaburi.
Serengema ndio sehemu iliyoathirika vibaya zaidi.
Kuna mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi pamoja na chama cha Tanzania Albino katika kuhamasisha na pia kujenga makaazi.
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanaamini kuwa uhamasisho na kuacha imani potovu zinaweza kusimamisha mauaji haya.
Kamanda mkuu wa polisi mjini Mwanza anasema kuna changamoto nyingi sana katika kukabiliana na mauaji ya Albino
Mwakilishi wa chama cha Serengema Mashaka Benedict anasema kuwa watu bado wanaamini kuwa sehemu za mwili wa albino zinaweza kuleta utajiri.''Kama hiyo ndiyo hali,mbona sisi si matajiri?''anauliza.
Anadai kuwa watu mashuhuri wanahusika katika ''biashara ya mauaji'' na ndio maanake watu wachache sana wamekamatwa,kushitakiwa,kupatikana na hatia ama kufungwa.''Itakuwa vipi masikini kutoa dola 10,000 kwa kipande cha mwili?,ni wanabiashara na wanasiasa ndio wanaohusika.''
Hata hivyo polisi wanasema kuwa wanachungunza kila moja ya visa lakini wanakosa ushahidi wa kuthibitisha madai yanayotolewa.Kamanda wa polisi wa Mwanza,Valentino Mlolowa anasema,''Kesi hizi ni ngumu kwa kuwa visa hufanyika mashinani sana katika sehemu ambazo hazina stima kwa mfano,na hiyo inafanya kuwajua wahalifu usiku kuwa vigumu.Tunachunguza kila moja ya kesi na madai,lakini kama uonavyo,si
rahisi.''
Yaweza onekana kama kuwa tumepoteza kila kitu lakini hii haiwazuilii watu wanaoishi na hali ya Uhalbino kama May Mosi,kutokuwa na tumaini kuwa fedha zinazochangishwa kutoka kwenye kampeni iliyoanzishwa na serikali zitasaidia kusikizwa zaidi kwa Albino nchini Tanzania.

Tuesday, December 9, 2014

Daktari feki akamatwa Tanzania

Sekta ya afya nchini Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la madaktari feki ambapo jana Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu, MOI ilimkamata daktari feki aliyefahamika kwa jina la Dismas John Macha mwenye umri wa miaka 35.

Taasisi hiyo ipo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, MNH jijini Dar es Salaam, ambapo daktari huyo anadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kwa madai kwamba angemhudumia mgonjwa wao.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, Mkurugenzi wa MOI, Athumani Kiloloma, alisema mara ya kwanza alikamatwa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS, akijifanya mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika shule ya tiba.
Dk. Kiloloma alisema alipokamatwa mara ya kwanza, walitoa matangazo katika hospitali nzima na kutoa taarifa kwa wananchi, lakini wanashangaa tukio hilo limejirudia tena.

Akizungumzia tukio hilo, mkurugenzi huyo alisema wanakabiliwa na tatizo kubwa la madaktari feki, ambao wamekuwa wakiomba michango mbalimbali ya fedha.

Mtuhumiwa Dismas Macha anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
Awali, Dismas akizungumza na waandishi wa habari, alisema yeye si daktari bali ni mgonjwa wa akili.

Matukio ya madaktari feki yamekuwa yakiripotiwa katika hospitali mbalimbali nchini Tanzania katika siku za karibuni, ambapo inadaiwa madaktari hao kazi kubwa ni kuwatapeli wagonjwa na ndugu wa wagonjwa.

Monday, December 8, 2014

Yaya aliyemtesa mtoto UG aomba msamaha

Jolly Tumuhirwe ameomba mahakama kumsamehe kwa kumtesa mtoto


Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajulia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.
Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la ,mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
Bi Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.
Kesi hio imeakhirishwa hadi Jumatano, wakati ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.
Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mianne au adhabu zote mbili.

Sunday, December 7, 2014

Lwakatare wa Chadema, Ludovick waibwaga Serikali mahakamani


Dar es Salaam. Mahakama ya Rufani imetupilia mbali maombi ya marejeo kuhusu uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam kuwafutia mashtaka ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick Rwezahura.
Hatua hiyo ya mahakama imefanya kiongozi huyo wa Chadema na mwenzake kuibwaga Serikali kwa mara ya pili mahakamani katika mashitaka dhidi yao.
Maombi hayo namba 5 ya mwaka 2014, yalifunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika Mahakama ya Rufani akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufumfutia mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ulisomwa jana na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma kwa niaba ya Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo lililokuwa limepangwa kusikiliza maombi hayo.
Majaji hao ni Nathalia Kimaro (kiongozi wa jopo), William Mandia na Profesa Ibrahimu Juma.
Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa maombi hayo yalikuwa na dosari za kisheria kutokana na DPP kutoambatanisha mwenendo wa uamuzi wa Mahakama Kuu aliokuwa akiupinga.
Dosari hiyo iliibuliwa na Jaji Prosefa Juma katika tarehe ambayo maombi hayo yalikuwa yamepangwa kusikilizwa ambapo alihoji iwapo ni halali kusikiliza maombi hayo bila kuwepo kwa mwenendo huo.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Angaza Mwipopo akisaidiana na Wakili Serikali Mwandamizi, Hashim Ngole, alijibu kuwa wanachopinga ni uamuzi wa mahakama kufuta mashtaka katika kesi ambayo haikuwa mbele yake.
Wakili Angaza alidai kwamba kutokuwepo kwa mwenendo huo hakuathiri na kwamba mahakama ina uwezo wa kuyasikiliza maombi hayo hata bila kuwepo kwa mwenendo huo.
Akijibu hoja hizo, Wakili wa Lwakatare, Peter Kibatala alisema kuwa suala la mwenendo wa uamuzi unaopingwa ni miongoni mwa hoja za pingamizi lake la awali dhidi ya maombi hayo.
Wakili Kibatala alidai kuwa kutokuwepo kwa mwenendo huo ni dosari ambayo ina athari kubwa kiasi kwamba mahakama haitakuwa na uwezo wa kutoa kile kinachoombwa.
Alisisitiza kuwa kutokuwepo kwa kumbukumbu za mwenendo huo ni athari ambayo tiba yake ni mahakama kuyatupilia mbali maombi hayo.
Wakili Mwipopo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 65 ya Kanuni za Mahakama ya Rufani, siyo lazima kuambatanisha mwenendo katika maombi na kwamba nyaraka za msingi kwa mujibu wa kanuni hiyo ni hati ya kiapo, ambavyo wameviambatanisha.
Hata hivyo, kupitia uamuzi wake jana, mahakama ilisema kuwa msimamo wa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 4 (3) cha Sheria ya Mamlaka ya Mahakama ya Rufani ni lazima kuambatanisha mwenendo wa uamuzi unaopingwa, uamuzi na amri ya mahakama katika maombi ya marejeo.
“Kutokana na kasoro hiyo ya kutokuwepo kwa mwenendo wa uamuzi unaopingwa, tunatupilia mbali maombi haya,” ilisema mahakama katika uamuzi wake.
Katika maombi hayo, DPP alikuwa akiiomba Mahakama ya Rufani iitishe majalada ya kesi hiyo na kuchunguza uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu kuwafutia washtakiwa hao mashtaka ya ugaidi na kisha ifute uamuzi huo wa Mahakama Kuu na amri zote ilizozitoa. Pamoja na mambo mengine, DPP alikuwa akidai kuwa haikuwa sahihi Mahakama Kuu kuamua kuwa mashtaka hayo hayakuwa halali, kwani hapakuwa na taarifa zilizowasilishwa dhidi ya washtakiwa, ambazo Mahakama Kuu ingezizingatia katika kuamua uhalali wake.
Kulingana na uamuzi huo, DPP anaweza kufungua tena maombi hayo baada ya kurekebisha kasoro hiyo, lakini baada ya kuomba kibali cha mahakama kufungua marejeo hayo nje ya muda wa kawaida kisheria.
Akizungumzia kesi hiyo, Lwakatare alisema: “Kwanza namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kushinda kesi hii…; kusema kweli ilikuwa kesi ngumu na mbaya, hasa ikizingatiwa kwamba ilikuwa ndiyo kesi ya kwanza ya ugaidi kufunguliwa hapa nchini.”
Lwakatare aliongeza: “Nawashukuru mawakili wangu ambao wamekuwa wakisimamia kesi hii pamoja na makahama pia kwa kutenda haki leo (jana). Kama ungefanyika uamuzi tofauti na huu, basi ningebaki Segerea. Pia, haki hiyo imeweza kutendeka kutokana na misingi ya kesi husika kuwa ya kusuasua. Kesi ilifunguliwa kwa jabza na shinikizo la kisiasa.”
Alieleza kuwa, licha ya shinikizo hilo, haki imeweza kutawala na ameshinda kesi hiyo mbali na misukusuko aliyopitia.
Alisema kwamba anatumaini makahama itaendelea kutoa hati katika kutoa uamuzi wa kesi yake iliyobaki katika Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Naye Wakili Kibatala alisema kuwa kwa hali ilivyo suala hilo limekwisha na kwamba DPP hana mwanya wa kurudi tena na maombi hayo.
Alifafanua kuwa kwa kawaida maombi ya marejeo hufunguliwa katika muda wa siku 60 tangu siku ya kutolewa kwa uamuzi unaopingwa na kwamba, nje ya muda huo mwombaji analazimika kuomba kibali cha Mahakama kufungua maombi nje ya muda na kutoa sababu za kuridhisha.
“Siku 60 tayari zimeshakwisha, hivyo DPP akitaka kurudi tena ni lazima aombe kibali na atoe sababu za kuiridhisha Mahakama. Sababu za kuridhisha ni pamoja na ugonjwa, au kuchelewa kupata nakala ya uamuzi na mwenendo kutoka mahakamani, lakini siyo kwa uzembe,” alisema.
Lwakatare na Ludovick walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, matatu kati yake yakiwa ya ugaidi na moja la kawaida la jinai.
Mashtaka hayo ya ugaidi yalikuwa ni kupanga kumteka aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky na kisha kumdhuru kwa sumu, kushiriki mkutano wa vitendo vya ugaidi (kwa washtakiwa wote) na kuhamasisha vitendo vya ugaidi lililokuwa likimkabili Lwakatare pekee.
Shtaka lingine la jinai lilikuwa ni kula njama ya kutenda makosa, ambalo lilikuwa likiwakabili wote kwa pamoja na bado linaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hata hivyo, Mei 8, mwaka huu Jaji Lawrence Kaduri wa Mahakama Kuu aliwafutia mashtaka ya ugaidi, baada ya mawakili wa Lwakatare kufungua maombi wakipinga uamuzi wa DPP kuwafutia mashtaka katika kesi ya awali na kisha kuwakamata na kuwafungulia mashtaka hayohayo

IDRISS SULTAN AIBUKA KIDEDEA SHINDANO LA BIGBROTHER HUKO AFRIKA KUSINI USIKU HUU

unnamedIdriss Sultan Mtanzania aliyetikisa Bigbrother leo ameibuka mshindi wa shindano hilo na kuwabwaga washiriki kutoka mataifa mbalimbali yaliyoshiriki katika shindano hilo akiibuka na kitita cha shilingi milioni 500 za Kitanzania katika shindano hilo lililokuwa likiendelea kwa miezi mitatu nchini Afrika Kusini Idriss ni Mtanzania wa tatu kushinda shindano hilo akitanguliwa na Mwisho Mwampamba na Richard wote wakiwakilisha vizuri taifa la Tanzania katika shindano hilo, Fullshangwe inampa hongera sana Idriss kwa ushindi huo na inamtakia kila mafanikio katika maisha yake.

WAZIRI CHIKAWE ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 22 KKKT JIMBO LA KASKAZINI-MAGHARIBI NACHINGWEA

unnamedWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akifungua zoezi la uchangiaji wa harambee ya kupatikana kwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, anayefuata ni Katibu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini –Mashariki, Jane Mkimbo. Kulia ni Mkuu wa Jimbo hilo, Mchungaji Charles Mtweve. Katika harambee hiyo Shilingi Milioni 22.3 zilipatikana. Picha zote na Felix Mwagara
unnamed1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akifungua zoezi la uchangiaji wa harambee ya kupatikana kwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi. Katika harambee hiyo Shilingi Milioni 22.3 zilipatikana.
unnamed2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akitoa mchango wake wa awali shilingi milioni moja kwa ajili ya uchangiaji wa harambee ya kupatikana kwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, anayefuata ni Katibu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini –Mashariki, Jane Mkimbo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jimbo hilo, Mchungaji Charles Mtweve. Katika harambee hiyo Shilingi Milioni 22.3 zilipatikana.
unnamed3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (watatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo (wanne kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi, Nachingwea na KKKT Dayosisi ya Kusini-Mashariki, Kanisa Katoliki na maofisa wa wilaya hiyo, mara baada ya kumaliza harambee ya kuchangisha milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi. Picha zote na Felix Mwagara

DIAOMOND USIPIME ANOGESHA SHEREHE YA UHURU DMV

Prezida wa Wasafi Diamond Platnumz akiwa pamoja na wacheza showa wake Roma Tonsa na Moses Iyobo wakitoa burudani katika kunogesha sherehe ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika Sheraton Hotel ya Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na mashabiki wake kutoka kila pembe ya Marekani huku mashabiki wengine wakitokea Tanzania, Picha na Vijimabo Blog
Mzuka unazidi kupanda Diamond Platnumz asaula koti lake.
Balozi akimshukuru Diamond kwa kuwezesha kunogesha usiku wa Uhuru wa Tanzania na pia aliwashukuru wadhamini wa sherehe hiyo ya moaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Diamond akizidi kuwapa burudani mashabiki wake
Shabiki akicheza wimbo wa mdogo mdogo
Shabiki akijumuika na Diamond kwenye jukwaa.

Thursday, December 4, 2014

KUITWA KWENYE USAILI JESHI LA MAGEREZA TANZANIA BARA




04 Desemba, 2014
KUITWA KWENYE USAILI

Jeshi la Magereza linawatangazia wafuatao kufika kwenye usaili kwa nafasi walizoomba. Usaili huo utafanyika kuanzia tarehe 10/12/2014 mpaka tarehe 17/12/2014 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga Jijini Dar es salaam kuanzia 2:00 asubuhi kwa mujibu wa tarehe za makundi kama yalivyoainishwa. Kwa wale wa kidato cha Nne na Sita waliosailiwa kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wasubiri maelekezo mengineyo. Aidha wale ambao hawakuona majina yao hapa wahesabu kuwa hawakufanikiwa.

Waombaji wanatakiwa kuzingatia  yafuatavyo;-
i.    Kuja na Vyeti halisi (Original Certificates) vya elimu na ujuzi
ii.    Kuja naCheti halisi cha kuzaliwa,
iii.    Hati za matokeo ya mitihani (Result Slip/Statements) hazitakubaliwa isipokuwa kwa wahitimu ambao vyeti vyao halisi havijatolewa na vyuo husika wakiwa na barua Maalum ya kuthibitisha kwamba vyeti halisi havijatolewa,
iv.    Wahusika watajitegemea kwa nauli za kuja na kurudi, chakula na malazi kwa kipindi chote cha usaili
Tangazo hili pia linapatikana kwenye Mbao za Matangazo zilizopo Bwalo Kuu la Magereza, tovuti ya magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz, gazeti la Uhuru la tarehe 05 Desemba 2014 sanjari na blog ya magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com

Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza

J.C.Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
Bofya HAPA kupata orodha ya wanaotakiwa kufika kwenye usaili
 

NAIBU KATIBU MKUU CHADEMA AKIWA ZIARANI MKOANI RUKWA KATIKA MKUTANO WA OPERESHENI DELETE CCM


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Muze, Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa, katika mfululizo wa mikutano ya ziara ya Operesheni Delete CCM, (Jumamosi 29/11/2014.)

KESI YA CHIDI YA BENZ YAPIGWA KALENDA




Mashtaka matatu yanayomkabili chidi benz mojawapo la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya zaidi ya elfu 30, ambayo alikutwa nayo wakati anakaguliwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu julius kambarage nyerere, kesi imesogezwa mbele

Chidi benz jana jioni aliandika kupitia account yake facebook “chiddi Beenz chuma” maneno yafuatayo

Kesho ni judgement yangu na ni mwisho wa kesi yangu pale kwa Hakimu mkazi wa kisutu, najua nimekosea lakini sio sana kuliko makosa yooote, muhimu ni kusamehe na kuondoa hasira na mimi, msipoteze imani na mimi, nimekua Msanii mzuri na bora kwa kipindi chote, nikiwa kazini inafahamika nachokifanya, sijawahi kosea kufanya kazi yangu hayo mengine ni mengine tayari, mnaweza kutokea kwa support na naomba mniombee, nisirudi kule tafadhali

Wednesday, December 3, 2014

IS wafungua kambi za mafunzo Libya

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo Libya
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika.
Wapiganaji wa Kikurd wakiwa katika mafunzo ya kijeshi kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State Septemba 2014 nchini Iraq
Jenerali David Rodriguez amesema kuna mamia ya wapiganaji wa IS wanaopata mafunzo ya kijeshi kwenye kambi zake nchini Libya. Amesema kambi hizo zipo katika hatua za mwanoz kabisa, lakini Marekani imekuwa ikiyafuatilia kwa karibu kuona zinavyoendelezwa.
Libya imekuwa katika mgogoro tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, ambapo makabila mbalimbali, wanamgambo na makundi ya kisiasa, wote wakipigania madaraka.
Makundi mbalimbali ya Kiislam yanawania madaraka mashariki mwa Libya, huku baadhi yakitangaza kuwa na ushirikiano la kundi la Islamic State, IS.
 
Wapiganaji kutoka kikundi cha IS wakipakia mabaki ya kile kinachosemekana kuwa mabaki ya ndege ya Marekani isiyotumia abiria baada ya kukonga katika mnara wa mawasiliano huko Raqqa Septemba 23,2014
Akizungumza mjini Washington Jumatano, Jenerali Rodriguez bado haijafahamika ukaribu uliopo kati ya watu wanaopata mafunzo hayo na kundi la IS.
"Kikubwa ni watu wanaokuja kupata mafunzo na msaada wa vifaa kwa ajili ya kambi za mafunzo kwa sasa," amesema. "kwa sasa mafunzo hayo bado ni ya hatua ya chini sana na tunafuatilia kuona namna hali inavyokwenda."
Watoto wakikimbia kando ya mlima hukumoshi ukisambaa angani kufuatia mapigano katika eneo hilo la mji wa Kobani, wakati majeshi yanayoongozwa na Marekani kushambulia wapiganaji wa Islamic State
Waandishi wa habari wanasema katika kipindi cha mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Gaddafi, wapiganaji wengi waasi waliondoka nchini humo kwenda kujiunga na vikundi vya wapiganaji nchini Syria na baadhi yao wanaaminika kuwa wamerejea nyumbani(Libya).
Serikali iliyochaguliwa imepoteza miji mikuu mitatu ya Libya huku kukiwa na mgogoro wa kisiasa.
Benghazi, mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya, uko mikononi mwa wapiganaji wa Kiislam, na bunge linalotambuliwa kimataifa kwa sasa linaendesha vikao vyake katika mji ulioko pwani ya Tobruk mashariki mwa nchi hiyo.
Marekani imekuwa ikiongoza washirika wa kimataifa kufanya mashambulio ya anga dhidi ya IS nchini Iraq na Syria katika miezi ya karibun