Kampuni
ya Belly Armor, ambayo ilikua ya kwanza kutengeza bidhaa zinazohitajika
na wanawake wajawazito, kutokana na kitambaa maalum kinacholinda mwili
kutokana na athari za madini ya chuma mwilini, imeanzisha biasharta
nyingioenkwa manufaa ya wanaume.
Kampuni hii imeanza kutengeza
nguo za ndani za wanaume ambao zinawalinda kutokana na athari ya madini
ya chuma yanayoweza kupunguza nguvu za kiume na kuathiri uzalishaji wa
mbegu za kiume hali ambayo inaweza kusababisha mwanaume kukosa
kuzalisha.Unaweza kujiuliza je biashara ya kutengeza vitambaa hivyo inanawiri? Jibu? Ndio tena sana.
Mnamo mwaka 2011, shirika la afya duniani lilitaja madini hayo hatari ikiwemo miale inayotokana na simu za mkononi kama yenye uwezo wa kusababisha saratani ya ubongo mbali na athari nyinginezo hatari kwa mwili kiafya.
Kwa mfano, watumjai wa Iphone, je mlijua kama mnapaswa kuzibeba simu zenu umbali wa milimita 10 kutoka kwa mwili wako kuhakikisha kuwa madini hayo hayaathiri mwili?
Licha ya kwamba utafiti mpya unahitajika kuthibitisha hili....ni wazi kwamba madini fulani yanayotumika kutengeza simu yanaweza kusababisha aina ya saratani za mwilini.
Na ndio maana kampuni ya Belly Armor ikaja na wazo la kuwatengezea wanaume nguo za ndani zinazoweza kuwakinga kutokana na athari hizo.
Pia utafiti ambao umefanywa unaonyesha kua baadhi ya miale inayotokana na vifaa kama vile simu za mkononi, Tabiti au Ipad, inaweza kusababisha mwili wa wanaume kupungukiwa na nguvu za kutengeza mbegu za kime au hata mwili kuishiwa na nguvu za kiume.
No comments:
Post a Comment