Tunisia inakabiliwa na adhabu ya
kufungiwa kushiriki michuano ijayo ya Kombe la mataifa Afrika baada ya
kukaidi kuomba radhi kwa kosa la kushutumu shirikisho la soka Afrika CAF
kujihusisha na vitendo vya udanganyifu.
Tunisia ilitoa madai hayo
baada ya Mchezo wa robo fainali walipokutana na wenyeji Guinea ya
Ikweta, hasa baada ya mwamuzi kutoa Penalti katika dakika za lala salama
za mchezo huo ambapo mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa Tunisia
ilikuwa imefungwa magoli 2-1.Mwamuzi wa mchezo huo naye amefungiwa kwa miezi sita kwa kuchezesha vibaya mchezo huo.
Tunisia ilikua imepewa mpaka siku ya Alhamisi kuomba radhi vinginevyo adhabu ya kufungiwa michuano ya mwaka 2017 ingewakabili.
Baada ya mkutano siku ya Jumatano, Shirikisho la Soka Tunisia ilikataa kuomba radhi huku Msemaji wake akisema kuwa Timu yake haikutendewa haki na Waamuzi wa mchezo.
Caf,iliyowapiga faini Tunisia baada ya Wachezaji kumzonga na kumfanyia vurugu Mwamuzi Rajindraparsad Seechurn baada ya kipyenga cha mwisho, ilitaka mabingwa hao wa mwaka 2004 kuomba radhi baada ya kudai kuwa Shirikisho hilo na maafisa wake wana upendeleo na hawana maadili vinginevyo wapeleke vigezo vya kuthibitisha madai yao.
No comments:
Post a Comment