Kasisi
mmoja raia wa Australia amefichua na kuthibitisha kuwa kuna idadi kubwa
ya wafungwa wenye asili ya Afrika katika magereza ya Hong Kong, wengi
wao wakiwa ni kutoka Tanzania.
Kasisi huyo John Wortherspoon
ambaye kwa sasa anafanya ziara maalum Tanzania, amesema yeye ndiye
ambaye amekuwa akisambaza barua zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa
wanaoshikiliwa kwenye magereza hayo ambapo baadhi yao wametaja majina ya
watu wanaodaiwa kuwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya
waliowatuma kusafirisha dawa hizo. Padre Wotherspoon amefika
kuonana na familia za wafungwa hao pamoja na idara za serikali
zinazohusika na mapambano dhidi ya biashara hiyo hatari ya dawa za
kulevya.
No comments:
Post a Comment