WATU wawili wameuawa katika matukio tofauti, akiwemo kijana mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi yake.
Kijana huyo alikutwa
amenyongwa na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutundikwa juu ya mti
kwa kutumia suruali aliyokuwa amevaa katika kijiji cha Ibadakuli,
Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Shinyanga, Longinus Tibishubwamu alisema tukio hilo
limetokea Januari 27, mwaka huu. Alisema mwili ulikutwa na jeraha kwenye
mguu wa kulia na uchunguzi wa daktari unaonesha kuwa kijana huyo
aliumia kabla ya kunyongwa shingo na chanzo cha mauaji hayo
hakijajulikana.
Wakati huo huo,
Kamanda Tibishubwamu alisema mwanamke asiyefahamika jina wala makazi
yake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30 ameuawa kisha
mwili wake kuwekwa chini ya daraja dogo lililopo katika kitongoji cha
Jihingu kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga.
Aliongeza kuwa mwili
wa marehemu umekutwa ukiwa na majeraha kichwani, usoni na ubavuni na
kwamba Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi juu ya mauaji hayo ili
kuwabaini na kuwakamata wahusika.
No comments:
Post a Comment