Mtandao wa Forbes umetoa list mpya ya matajiri hamsini kutoka Afrika
list ambayo inaongozwa na tajiri wa Nigeria ambae ni Mfanya biashara
maarufu na Rais wa kampuni ya Dangote Aliko Dangote, aliyekuwa
akishikilia nafasi ya arobaini na tatu na kupanda...
Read More »
Sunday, November 30, 2014
Chanjo ya EBOLA yatoa matumaini
Watafiti wa masuala ya afya nchini MAREKANI, wamesema, majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa EBOLA yaliyofanyika nchini humo, yanaonekana kuwa ya mafanikio.
Chanjo hiyo imetengenezwa ili kuchochoea kinga ya mwili wa binadamu ili itengeneze kinga dhidi ya virusi vya EBOLA. Watafiti hao wanasema chanjo hiyo imeonyesha mafaniko, kwa vile watu waliokubali kufanyiwa majaribio, miili yao imeweza kutengeneza kinga dhidi ya EBOLA katika kipindi cha wiki nne.
Utafiti huo unaonyesha kuwa watu waliofanyiwa majaribio ya chanjo dhidi ya EBOLA, hawakupata athari hasi za chanjo hiyo. Taasi inayoshughulika na chanjo hiyo, inatarajiwa kufanya majaribio zaidi kuhusiana na chanjo hiyo mwezi ujao.
Kajaribio ya awali ya chanjo hiyo yanatarajiwa kufanyika nchini LIBERIA, ambako watu wengi wameathiriwa na EBOLA.
Polisi,waandamanaji wapambana Hong Kong
Polisi na waandamanaji wanaodai demokrasia wamepambana mjini Hong Kong katika eneo linalozunguka makao makuu ya serikali.
Ili kutuliza maandamano hayo Polisi wamelazimika kutumia maji yenye pilipili ambao baadhi yao walikuwa wamejihami kwa silaha.Takribani watu 48 wanashikiliwa na polisi kutokana na maandamano hayo ambayo yamechukua miezi miwili hadi sasa.
Madai ya waandamanaji hao ni kutaka kuwa na uhuru wa kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na Beijing.
Saturday, November 29, 2014
Nigeria:Raia watakiwa kuwa waangalifu
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
amewataka watu wote nchini Nigeria kuwa waangalifu na kushirikiana na
vikosi vya usalama vya nchi hiyo ili kujaribu kuzuia mashambulizi zaidi
yanayotekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mwa nchi.
Hakuna
kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo lililotokea kwenye msikiti
mmoja mkubwa ulio kwenye mji wa Kano ambapo watu kadhaa waliuawa.Hata hivyo shambulizi hilo linaaminika kutekelezwa na Boko Haram ambalo kampeni yake dhidi ya serikali imesababisha vifo vya maelfu ya watu mwaka huu.
Polisi walitibua njama ya shambulizi jingine kwenye mji ulio kaskazini mwa Nigeria wa Maiduguri ambapo mabomu sita yaliharibiwa ndani ya msikiti mmoja na kwenye soko lililo karibu.
Friday, November 28, 2014
Tibaijuka:''Nilipokea pesa za Escrow''
Mjadala kuhusu kashfa ya uchotaji wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya ESCROW ya Benki Kuu ya Tanzania umezidi kuunguruma nchini Tanzania kufuatia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, na ripoti ya serikali kuhusu kashafa hiyo.Mambo yaliyojitokeza katika ripoti ya PAC ni kutaja majina ya viongozi na maafisa wandamizi wa serikali walionufaika na magao huo.
Thursday, November 27, 2014
EMERSON AANZA MAZOEZI
Kiungo mbarazil Emerson de Oliveira a(wa pili kutoka kulia) akiwa
mazoezini leo asubuhi katika uwnaja wa shule ya sekondari Loyola,
wengine ni Kizza, Javu na Coutinho
Baada ya kuwasili jana kutoka nchini Brazil, kiungo mkabaji Emerson de Oliveira Neves Roque leo ameanza mazoezi mepesi asubuhi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola kufuatia kusaifri kwa zaidi ya masaa 11 kutoka jijini Rio de Janeiro.
Emerson ameungana na wachezaji wengine wa Young Africans katika mazoezi ya leo asubuhi ikiwa ni siku yake ya kwanza katika ardhi ya Tanzania na kufanya mazoezi mepesi mepesi chini ya kocha msaidizi Leonardo Neiva kuijiweka fit na kutoa uchovu safari.
Kiungo huyo mwenye umbo lililonyumbulika ambae alikuwa akichezea timu ya Bonsucesso FC iliyopo lii daraja la pili nchini Brazi katika jiji la Rio de Janeiro pia msimu uliopita alikua akicheza soka la kulipwa katika nchi ya Poland latika klabu ya Piotrkow Trybunalski FC.
Kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo amesema mchezaji huyo leo alikua na programu ya mazoezi mepesi tu kutokana na uchovu wa safari na kesho anatarajiwa kuendelea na mazoezi na wenzake kulingana na ratiba iliyopo.
Endapo Emerson atafanikiwa kulishawishi benchi la Ufundi kumsajili basi moja kwa moja ataingia makubaliano na klabu ya
Young Africans kwa ajili ya kuitumikia kwenye michuano ya kimataifa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia bara.
SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI.
Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew Chenge (Mb)
Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6.
Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.
Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4
Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.
Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4
Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9
Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.
Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow
Zitto: Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006
Zitto: Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.
Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.
Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4.
Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4
Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.
Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4
Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9
Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.
Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow
Zitto: Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006
Zitto: Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.
Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Wednesday, November 26, 2014
Sakata ya Escrow leo jioni
Ripoti iliyokuwa ikisubiriwa na
wananchi kuhusu ukweli wa uchotaji wa mamilioni ya fedha kutoka akaunti
ya ESCROW ya Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha kashfa miongoni mwa
wanasiasa na maafisa wa serikali na majaji inatarajiwa kuwasilishwa leo
jioni katika bunge Kamati ya Hesabu za Serikali, PAC.
Ripoti ya PAC imefuatia kuwasilishwa kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini humo, TAKUKURU, zilizowasilishwa bungeni hapo.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya bunge, taarifa ya PAC itawasilishwa leo jioni kuanzia saa kumi na moja jioni na kujadiliwa kwa siku mbili ujadiliwa kwa siku mbili. Hata hivyo kabla ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo, kumeibuka madai ya kuwepo zuio la Mahakama Kuu kuhusu kujadiliwa kwa ripoti ya PAC.
Naye mwenyekiti wa bunge hilo Mussa Zungu Azan anawahakikishia wabunge kuwa ripoti hiyo itawasilishwa kama ilivyopangwa.
Makamu Rais Zimbabwe atimuliwa ZANU-PF
Vyombo vya habari vya Serikali nchini Zimbabwe vinaripoti kuwa Makamu wa Rais,Joyce Mujuru, ameondolewa kwenye kamati kuu ya chama cha ZANU-PF.
Mujuru anashutumiwa kupanga mauaji dhidi ya Rais wa nchi hiyo,Robert Mugabe.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Kampeni dhidi ya Mujuru iliyofanywa na Mke wa
Rais Mugabe, Grace ambaye kwa kiasi kikubwa anaamini anataka kumrithi
Mumewe atakapotoka madarakani.
Viongozi kadhaa wa ZANU-PF wameshindwa kutetea nafasi zao katika Chama hicho.
Bi Mujuru alitarajiwa kumrithi rais Mugabe mwenye umri wa miaka tisini.
Kamati
ya uchaguzi katika mkoa wa kaskazini wa Mashonaland ya kati imekataa
wasifu wa Makamu wa rais nchi hiyo Joice Mujuru kama baadhi ya
stakabadhi zake za kuomba kazi katika uchaguzi uliofanyika siku ya
Jumanne.
Vyombo vya habari vya Serikali nchini Zimbabwe vinaripoti kuwa Makamu wa Rais,Joyce Mujuru, ameondolewa kwenye halmashauri kuu ya chama cha ZANU-PF. Mujuru anashutumiwa kupanga mauaji dhidi ya Rais wa nchi hiyo,Robert Mugabe. hatua hiyo imekuja baada ya Kampeni dhidi ya Mujuru iliyofanywa na Mke wa Rais Mugabe, Grace ambaye kwa kiasi kikubwa anaamini anataka kumrithi Mumewe atakapotoka madarakani. Viongozi kadhaa wa ZANU-PF wameshindwa kutetea nafazi zao katika Chama hicho.
Tuesday, November 25, 2014
Zaidi ya watu 60 wauawa Syria
Zaidi ya watu 60 wameuwawa, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa na Jeshi la serikali ya Syria.
Raia wengi waliuwawa katika mashambulio tisa yaliyolenga ngome kuu za kundi la wapiganaji wa Islamic State.Wakereketwa wameiambia BBC kuwa Hospitali kuu ya Raqqa imesalia bila huduma kwani HAKUNA chakula na umeme.
Miili yatelekezwa Sierra Leone
Wafanyakazi ambao huzika miili ya
Watu waliokufa kwa Ebola, mjini Kenema nchini Sierra Leone wamegoma kwa
sababu hawajalipwa marupurupu yao.
Miili 15,kati ya hiyo mingi inahitajika kuzikwa,imetelekezwa katika hospitali kuu mjini humo.Mwili mmoja unadaiwa kutelekezwa kwenye Ofisi ya Meneja wa Hospitali hiyo, huku miili miwili ikiwa imetelekezwa kwenye mlango wa kuingilia Hospitali hapo.
Wafanyakazi hao wameiambia BBC kuwa hawajalipwa marupurupu ya waliyoyaita ya hatari kama walivyoahidiwa kwa ajili ya Mwezi Oktoba na Novemba.
Kenema ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Sierra Leone na Mkubwa katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo ambako ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza.
Takriban Watu 5000 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu katika nchi za Magharibi mwa Afrika, Guinea,Liberia na Sierra Leone.
P-Square wamepata pigo lingine,wamefiwa na baba yao mzazi.
Mapacha kutoka nchini Nigeria Peter Okoye&Paul Okoye P- Square
pamoja na kaka yao Jude Okoye,Jumatatu ya Nov 24 wamempoteza mzazi
aliyebakia ambaye ni baba yao mzazi hii ni miaka miwili tangu afariki
mama yao.
tovuyi ya www.Naij.com imesema kuwa Mr.Okoye alikua akisumbuliwa na maumivu ya Goti baada ya kufanyiwa upasuaji ingawa hali iliripotiwa kuendelea vizuri.
tovuyi ya www.Naij.com imesema kuwa Mr.Okoye alikua akisumbuliwa na maumivu ya Goti baada ya kufanyiwa upasuaji ingawa hali iliripotiwa kuendelea vizuri.
Monday, November 24, 2014
Muda wa mazungumzo na Iran waongezwa
Muda wa mwisho wa kufikia mwafaka
katika mazungumzo kati ya Iran na nchi sita tajiri zaidi duniani kuhusu
mpoango wake wa nuklia umeongezwa hadi Juni mwaka ujao.
Hii ni baada ya mazunguzo yanayoendelea mjini Vienna kukosa kufioka mwafaka uliotarajiwa.
Waziri
wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond kusema wamepiga hatua za
kuridhisha ingawa ni vigumu kufika mwafaka katika muda uliotarajiwa.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa China Wang Yi amasema kuwa anaamini mwishowe muafaka utapatikana.
Lakini taarifa kwenye mtandao wake ilisema kwa idadi kubwa ya masuala kadha ya kitaalamu yanatakiwa kuzungumziwa kwa undani.
Wapatanishi
wanasema kuwa kuna pengo kuhusu masuala ya kuiondolea vikwazo Iran ili
nayo iweze kuachana na mipango ya urutubishaji madini ya Uranium.
Kubwa
kwa yote hayo ni kwamba muda unayoyoma kwa viongozi wa dunia kufikia
mwafaka na Iran kuondoa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran
kuhusiana na mradi wake wa Nuklia.
Huku kukiwa na tofauti kati ya
mataifa, inaonekana mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna duru za
kidiplomasia zinasema kuwa yataakhirishwa hadi Disemba.
Iran
inashauriana na nchi nyingine sita zenye ushawishi zaidi dunaini ambazo
zilikuwa zimejipatia hadi mwishoni mwa leo kuwa na mwafaka.
Serikali ya Iran inasema kuwa inataka nishati ya nuklia kwa matumizi ya kawi ya atomiki wala sio kutengeza silaha za nuklia.
Marekani,
Urusi, China na Ufaransa, pamoja na Ujerumani, zinajaribu kufikia
mwafaka wa pamoja kuhusiana na mkataba uliofikiwa mjini Geneva mwaka
jana.
Mazungumzo ya ngazi ya juu yanaendelea kati ya waziri wa
mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, waziri wa mambo ya nje wa Marekani
John Kerry na mawaziri wa mataifa mengine matano.
Katika miezi
michache iliyopita, mazungumzo yamepunguza wasiwasi kuhusu vita vipya
mashariki ya kati na mawaziri watakuwa na wasiwasi kuondoka Vienna bila
ya kupata mwafaka.
Mfanyakazi mkatili matatani Uganda
Polisi wamebadilisha mashtaka ya
mfanyikazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea
unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kwa kosa la kutesa na sasa
anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji.
Video hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila babake mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi wenegine.
Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso.
Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba.
Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha mkuu wa mashitaka.
Tumuhirwe alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo kwa kurunzi, tuki olililonaswa kwa kamara ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi wa kiakili na kubaini kuwa ana akili timamu.
Afisaa mkuu wa polisi Fred Enaga, amewaonya waajiri kuchunguza mbinu zinazotumika kuwachagua wasichana wa kazi, kwa sababu matendo kama haya yanaweza kutokana na matatizo ya kisaikologia.
Waziri wa Jinsia, Kazi na maendeleo ya jamii Bi Mary Karooro Okurut alipongeza juhudi za wazazi wa mtoto huyo Arnella "kutokana na kitendo hicho kwa mtoto. Ingekuwa mtu mwingine angemuua mischana huyo wa kazi lakini alifuata sheria. Pia tunapeleka marekebisho katika katiba kuhusu maslai ya watoto bungeni kuimarisha sheria zinazowajali watoto," alisema waziri huyo.
Polisi wamesema kuwa nia ya shambulio hilo haijatambulika na pia msichana huyo amefanyia kazi familia hiyo kwa siku 26 pekee. Wazazi wamesema kuwa mtoto huyo ametolewa hosipitalini na hali yake ya afya inaimarika.
Kulingana na msemaji wa polisi Fred Enaga, kesi hiyo iliripotiwa na Baba ya mtoto Erick Kamanzi mnamo tarehe 13 Novemba katika kituo cha polisi cha Kiwatule baada ya kuona video hio.
Kesi hiyo ilipelekwa kwa kitengo cha polisi cha Kiira. Baada ya uchunguzi, msichana huyo wa kazi alihukumiwa na shataka la mateso katika mahakama ya Nakawa na kuzuuliwa katika gereza la Luzira.
Bwana Enaga alisema Bi Tumuhirwe alishtakiwa chini ya kifungo cha tatu kwenye katika kinacholinda maslahi ya watoto. Kifungo hicho kinajumuisha mashataka kama ya kutesa inayopeana uwezekano wa kumfunga mtu hadi miaka 15 gerezani.Hata hivyo, Bwana Enaga anashauriana na mkurugegenzi wa pande za mashtaka kurebisha hukumu hilo kuwa kifungu cha maisha.
Mama ashtakiwa kutupa mtoto Sydey
Mama mmoja nchini Australia
anashtakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji dhidi ya mtoto wake mchanga
ambaye alikutwa akilia katika eneo alilotelekezwa kwenye mfereji
unaopitisha maji machafu pembeni ya barabara mjini Sydney,ambapo Polisi
wanakisia kuwa mtoto huyo alikuwa katika eneo hilo kwa siku tano.
Waendesha baiskeli walisikia sauti ya mtoto ikitokea kwenye eneo hilo siku ya jumapili.Mwanamke huyo,Saifale Nai alitiwa nguvuni na Polisi baada ya msako uliodumu kwa saa kadhaa kwa kupata taarifa katika hospitali na operesheni ya nyumba kwa nyumba.
Polisi inasema mtoto huyo wa kiume alitupwa tangu siku ya jumanne .
Taarifa za mahakama zinasema mwanamke huyo alikubali kuwa alimtupa mtoto wake katika mfereji huo akiamini kuwa angekufa.
Mtoto huyo anaelezwa kuwa yuko hospitalini na hali yake inaendelea vizuri
Bunduki bandia yamletea maafa US
Wakili
anayewakilisha familia ya kijana mweusi mwenye umri wa miaka kumi na
mbili aliyepigwa risasi na polisi katika mji wa Cleveland nchini
Marekani, amesema familia yake itafanya uchunguzi wake sambamba na ule
unaofanywa na Polisi kubaini kilichotokea.
Kijana huyo kwa jina
Tamir Rice mwenye umri wa miaka 12 alikuwa amebeba kile kilichoonekana
kuwa bunduki bandia. Polisi wanadai kuwa kijana huyo alikataa kutii amri
alipoambaiwa asalimu amri.Kifaa walichokuwa nacho polisi ndicho kilibaini kuwa bunduki hiyo ilikuwa bandia.
Inaarifiwa kijana huyo alipigwa risasi mara mbili baada ya kuitoa bunduki yake kiunoni mwake lakini hakujaribu hata wakati mmoja kuielekeza kwa poliso wala kujribu kuifyatua.
Wakili wa familia hiyo amesema kuwa ikiwa watapata kuwa haki za kijana huyo zilikiukwa, familia yake itachukua hatua za kisheria dhidi ya polisi.
Mwanasiasa mmoja anapendekeza sheria ambayo itahakikisha kuwa bunduki bandia zinakuwa na rangi unayong'aa zaidi ili ziweze kutambulika haraka.
Saturday, November 22, 2014
Friday, November 21, 2014
Mkanyagano hatari wawaua 11 Zimbabwe
Watu 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufnayika katika uwanja wa soka.
Polisi wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter Magaya.
Mhubiri huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza.
Baadhi ya walioshuhudia mkanyagano huo wanatuhumu polisi kwa kufunga baadhi ya milngo ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka kupitia mlango mmoja tu.
Hata hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.
Bwana Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya kutokea vifo hivyo alihuzunika sana.
Kero la wafanyakazi ghushi wa umma Kenya
Serikali
ya Kenya imeamuru uchunguzi kufanywa baada ya majina ya wafanyakazi
hewa 12,000 kupatikana kwenye orodha yake ya mishahara.
Majina
hayo, yaligunduliwa baada ya maafisa wakuu kuanza kuwasajili wafanyakazi
wa serikali kwa njia ya kielektroniki kuanzia mwezi Septemba.Tume ya kupambana na rushwa nchini humo pamoja na kitengo cha kupambana na wizi kwenye benki zimetakiwa kuanzisha uchunguzi.
Kenya inashikilia nafasi ya 136 kati ya nchi 177 kwenye orodha ya shirika la kimataifa ya Transparency International ya mataifa fisadi zaidi duniani.
Ripoti ya awali iligundua kuwa serikali hupoteza takriban dola milioni moja kila mwezi kwa malipo ya mishara ya wafanyakazi ghushi, pamoja na nyenzo nyinginezo fisadi
Serikali inashuku kuwa wafanyakazi wa zamani wanaendelea kupokea mishahara hata baada ya kustaafu.
Rais Kenyatta ameamuru uchunguzi kufanywa mara moja
Wachunguzi katika idara ya ujasusi imeamrishwa kufanya uchunguzi kuhusiana na madai hayo.
Zaidi ya majina 12,500 ya wafanyakazi wa umma, waliokosa kufika kwa usajili wa kielektroniki, waliondolewa kwenye orodha ya mishahara mwanzoni mwa Novemba,kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation ambalo limenukuu waziri wa mipango na ugatuzi Ann Waiguru.Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kupambana na rushwa katika sekta ya umma baada ya kuchukua mamlaka mwaka jana.
Thursday, November 20, 2014
Rais Obama awatangazia neema wahamiaji
Rais Barack Obama amelihotubia taifa
kueleza mageuzi makubwa katika mfumo wa uhamiaji wa Marekani. Amesema
atachukua hatua za kikatiba kutoa ruhusa ya muda kisheria kwa takriban
wahamiaji haramu milioni tano. Obama amesema nchi hiyo ilijengwa kwa
uhamiaji na ameshutumu wanachama wa Republican kwa kuzuia mageuzi hayo.
Wanachama hao wametishia kuchukua hatua.
Amesema
watakaohalalishwa watalazimika kulipa kodi na wasiwe na rekodi ya
uhalifu. Hata hivyo amesema urejeshwaji makwao kwa watu wenye makosa
utaharakishwa.Bwana Obama ametangaza mpango wake, ambao anaupitisha bila baraza la Congress, katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni.
Kwa upande wao wajumbe wa Republican wamesema hatua ya Rais Obama inavuka mipaka yake na uhusiano na rais utaingia dosariKuna wahamiaji wasio halali wapatao milioni 11 nchini Marekani na mwaka huu watoto wanaovuka mpaka wamesababisha tatizo.
Rais Obama ameliambia taifa kuwa kile anachopendekeza sio msamaha
"Ninachokieleza ni uwajibikaji - akili ya kawaida, mtazamo wa kawaida," amesema.
"Kama unatimiza vigezo, unaweza kujitokeza na kuishi maisha ya kawaida ukiendana na sheria."
"Iwapo ni mhalifu utarejeshwa ulikotoka.Kama unapanga kuingia Marekani kinyume cha sheria, nafasi ya kukamatwa na kurejeshwa ulikotoka ni kubwa." anasema Rais Obama.
Rais Obama amesema mfumo mpya wa uhamiaji utawawezesha watu wanaoishi nchini Marekani kinyume cha sheria, kujulikana na kuchangia katika uchumi wa taifa kwa kuwa watakuwa huru kufanyakazi.
Kuamuru kufanyika kwa mageuzi hayo kumesababisha malalamiko ya hasira kwa wanachama wa Republicans ambao wanasema hatua hiyo ni kutolishirikisha baraza la Congress na kuendesha mambo kwa mfumo wa Kifalme. Baadhi wanasema hawatatoa ushirikiano katika maeneo mengine ya kisera, na wengine wamemtaka Bwana Obama ashitakiwe.
Rais Obama anasema anachukua hatua hiyo kwa sababu baraza la Congress mara kadha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu limeshindwa kurekebisha mfumo wa uhamiaji ambao umeharibika.
Msichana kutoka Syria ashitakiwa
Msichana wa kiholanzi aliyerejea
kutoka Syria ambako alikwenda huko kujiunga na wapiganaji wa jihadi
lakini baadaye alirudishwa nyumbani na mamake anatarajiwa kufikishwa
mahakamani kwa kushukiwa kutishia usalama wa taifa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19, akijulikana kama Aicha, alikamatwa aliporejea nyumbani kwao katika mji wa Maastricht.Aicha, aliyebadili dini hivi karibuni kuwa Mwislam, anaaminika kusafiri kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State (IS) katika ngome ya Raqqa nchini Syria kuoana na mpiganaji mmoja.
Mama yake Monique alisaidia kumrejesha nyumbani Uholanzi na si mtuhumiwa.
Aicha ni mmoja wa idadi ndogo ya wasichana na wanawake kutoka Ulaya ambao wamekwenda Syria na Iraq katika miezi ya karibuni.
Baadhi wanaaminika kusafiri kwenda hukokupata mafunzo ya kiitikadi, wakati wengine wanasemekana kuoana na wapiganaji, wakiwemo wanaopigana bega kwa bega na wapiganaji wa IS.
Mahakama nchini Uholanzi Ijumaa itasikiliza kesi hiyo bila wasikilizaji na itaamliwa Aicha anaweza kushikiliwa kwa muda gani.
Upande wa mashitaka unatarajiwa kumwomba jaji kuongeza muda wa kumshikilia Aicha wakati wakichunguza ushahidi.
Wednesday, November 19, 2014
Ebola yapoteza ajira,Afrika Magharibi
Zaidi ya nusu ya raia wa Liberia
waliokuwa na ajira mara baada ya mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola
hawana ajira tena kwa sasa,umebainisha utafiti wa banki ya dunia.
Inadaiwa kuwa wafanyakazi waliowengi wameambiwa na waajiri wao kubakia nyumbani huku wengine wakiachishwa kazi kabisa kutokana mamsoko kulazimishwa kusitisha shughuli zao
Hivi karibuni ripoti ya wataalam wa uchumi wa benk ya dunia waliarifu kuwa ugonjwa wa Ebola ungetarajiwa kugharimu ukanda uliokumbwa na ugonjwa huo kiasi cha dola billion tatu hadi nne.
Ebola imeleta madhara kwa takribani watu elfu 14 Afrika Magharibi,huku watu Zaidi ya 5,000 wamekufa huku 2,800 wakiwa ni kutoka Liberia.
Ana Revenga, ni afisa mwandamizi wa benki ya dunia hata kwa wale wanaoishi katika maeneo ambayo hajaathiriwa na ugonjwa huo wa Ebola nchini Liberia bado wanakumbwa na madhara hayo.
Taairifa hiyo ya benki ya dunia inasema sekta ya kilimo Liberia imeathirika kwa asilimia 70 kutokana na utafiti uliofanyika
Binti ajinasua na ndoa ya mwanamgambo
Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi
amewasili nchini Uturuki baada ya safari iliyojaa hatari nchini Syria
kwa ajili ya kumchukua binti yake aliyekua mjini Raqqa, mji unaokaliwa
na waasi wa Islamic State.
Monique alikwenda Uturuki mara ya kwanza baada ya binti yake aitwae Aicha kusafiri kwenda Syria kuoana na mmoja wa wanamgambo wa kundi hilo mwenye asili ya Uholanzi na Uturuki.Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la IS.
Aicha ,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na IS.Raia wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria Mwezi Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa.
Aicha aliondoka Uholanzi mwezi Februari, akaolewa na Omar Yilmaz, mwanamgambo mwenye asili ya Uturuki na Uholanzi ambaye alishawahi kuwa mwanajeshi nchini Uholanzi,alitumia mbinu alizopatiwa akiwa mwanajeshi na kuwafunza wapiganaji wenzake.
Monique amesema mwanae alibadilika ghafla kutoka binti aliyefahamika vyema na kuwa Msichana mwenye msimamo mkali.
Baada ya Polisi kumuonya Aicha kutosafiri kwenda Syria walikamata Pasi yake ya kusafiria, Aicha hakuvunjika moyo alitumia kitambulisho chake.
Aicha alikuwa akiwasiliana na Yilmaz kwa njia ya mtandao wa kijamii kisha wakapendana.
Monique alisafiri mpaka Uturuki mwezi Oktoba ili kumchukua mtoto wake lakini alishindwa kuvuka mpaka.
Lakini wiki iliyopita, baada ya Aicha kuomba msaada alirudi tena nchini Syria ingawa Polisi walimkataza kufanya hivyo.Monique alifika Raqqa nchini humo na kumchukua bintiye kisha kurejea Uturuki
Yilmaz, Mume wa Aicha anamtaja mkewe kuwa mtalaka wake kwenye anuani yake ya Tweeter.
Hivi sasa Mama na mwana wanashikiliwa mpakani mwa Uturuki, wakisubiri ruhusa ya kurudi Uholanzi.
Monday, November 17, 2014
Kanali ahukumiwa kunyongwa,Congo Dr
Mahakama ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji wa M23.
Afisa anayedaiwa kupangiwa
njama za kuuawa ni Mamadou Ndala mabaye kwa kiasi kikubwa aliamini
katika vita dhidi ya kundi hilo la wapiganaji na ambaye aliuawa mwezi
januari mwaka huu. Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa nane
ambapo kati ya hao mmoja ndiye Kanali Ndala aliyehukumiwa kifo. Mahakama imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa akitumiwa na waasi wa ADF kutoka Uganda kuandaa maujaji.Wito kwa wakazi kujihami dhidi ya Boko:H
Emir
wa Kaskazini mwa Nigeria, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kiisilmau
wenye ushawishi mkubwa, ametoa wito kwa watu nchini humo kuchukua silaha
na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa kiisilamu
wa Boko Haram.
Emir huyo wa Kano, Muhammad Sanusi, amewaambia wakazi wasisubiri wanajeshi kuwalinda kutokana na magaidi.Emir huyo ambaye alikuwa gavana wa benki kuu nchini humo kabla ya kuchukua wadhifa wake wa Emir, alitoa matamshi yake ya kutatanisha kwenye mkutano wa maombi.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kauli kama hii sio kawaida kutolewa kwani Emir huyo huyo hazungumzii sana maswala ya kisiasa.
Wapiganaji wa wa Boko Haram wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika sehemu kadhaa za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku wakiteka miji na mijiji ambko wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria kali ya kiisilamu.
Sanusi alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali alipokuwa anafanya kazi yake ya benki, alisema kuwa watu hawapaswi kuogopa wanamgambo hao na kwamba wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.
Mwandishi wa BBC anasema ingawa Emir huyo hakutaka kundi la Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee kwa kiongozi kama huyo kuwataka watu kujihami dhidi ya Boko Haram.
Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria
wapiganaji wa wa Boko Haram wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika sehemu kadhaa za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku wakiteka miji na mijiji ambko wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria kali ya kiisilamu.
Sanusi alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali alipokuwa anafanya kazi yake ya benki, alisema kuwa watu hawapaswi kuogopa wanamgambo hao na kwamba wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.
Mwandishi wa BBC anasema ingawa Emir huyo hakutaka kundi la Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee kwa kiongozi kama huyo kuwataka watu kujihami dhidi ya Boko Haram.
Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
HATARI!! Diamond aamua kuwapa ''makavu live'' team Wema baada ya wao kumdiss. HATARI!! Diamond aamua kuwapa ''makavu live'' team Wema baada ya wao kumdiss.
Baada ya mashabiki wa mwanadada Wema "kumjia juu mwanamuziki Diamond Platnumz" kuhusu
tuhuma za yeye kumtumia mwanadada huyu kimwili zaidi bila kumuendeleza,
hatimaye raisi huyu wa kundi la WCB ameamua nay eye kufunguka haya
mazito juu ya kauli hizo. Kupitia ukurasa wake wa mtandao ule maarufu wa
kijamii Diamond ameandika haya..
“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu... kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe...
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng'ombe wake Kwenye Maji safi....ila yeye ng'ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!... leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeeeew!
“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu... kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe...
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng'ombe wake Kwenye Maji safi....ila yeye ng'ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!... leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeeeew!
Msako mkali dhidi ya misikiti Mombasa
Msako mkali dhidi ya misikiti Mombasa
Polisi nchini Kenya wamefanya msako
mkali dhidi ya misikiti inayotoa mafunzo ya itikadi kali za kidini mjini
Mombasa pwani ya Kenya.
Mtu mmoja ameuawa kwenye msako huo
ulioanzishwa Jumapili dhidi ya misikiti inayosemekana kutoa mafunzo ya
kuunga mkono harakati za kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab
nchini Somalia.
Misikiti ya kwanza kulengwa katika msako huo ni ile ya Masjid Musa na Sakina.
Mkuu
wa polisi mjini Mombasa alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema
kuwa walipata taarifa kwamba kundi hilo limekuwa likipanga kufanya
mashambulizi na hiyo ndiyo sababu ya msako huo kuanzishwa.
Sunday, November 16, 2014
Matokeo ya michuano ya dimba la Afrika
Mabingwa watetezi wa kombe la Afrika
Nigeria wameicharaza Congo Brazaville 2-0 siku ya jumamosi ili
kuimarisha matumaini yake ya kufuzu katika dimba la Afrika mwaka 2015
huku Afrika kusini na Cameroon zikifuzu katika kinya'nganyiro hicho.
Afrika
kusini iliichapa Sudan 2-1 katika mechi yao ya kwanza tangu kuuawa kwa
mlinda lango wake Senzo Meyiwa ili kuongoza kundi la Da.Zambia nayo iliinyamazisha Mozambique 1-0 mjini Moputo kufuzu na katika kundi Fa pamoja na viongozi wa kundi hilo Cape Verde.
Burkina Faso na Gabon pia zilifuzu katika kundi Cha baada ya Kuishinda Lesotho 1-0 mjini Maseru huku Angola ikipata sare ya bila kwa bila dhidi ya wenyeji wake mjini Luanda.
Saturday, November 15, 2014
Kura dhidi ya waziri mkuu yapigwa Somali
Wabunge nchini Somalia wanapiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed.
Shughuli za bunge zimekwama kutokana na tofauti zilizopo kati ya waziri kuu na rais wa Somalia Hassan Sheik Mohamud.Wadadisi wanasema kuwa hali imedhoofika kutokana na mizozo ya kisiasa.
Marekani inasema kuwa kura hiyo ya kutokuwa na imani haiwakilishi maslahi ya raia.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako
Wednesday, November 12, 2014
Wanasayansi wajawa na shauku ya kimondo
Wanasanyansi wa safari za anga za mbali wamejawa na shauku ya kutaka thibitisho kwamba Chombo kilichopelekwa na kutua kwenye kimondo au nyota mkia yaani Comet iliyo umbali wa zaidi ya kilometa nusu bilioni kutoka duniani.
Hapo jana Chombo hicho kiliwezesha kuwekwa kwa historia ya kuwa kifaa cha kwanza kuwahi kutengenezwa na binadamu kutua kwenye kimondo, kazi iliyochukua zaidi ya miaka 10.Hata hivyo huenda bado kifaa hicho hakijajibanza kwenye kimondo hicho chenye upana wa kilometa mbili , kama ilivyotarajiwa-Data mpya na hasa picha zinasubiriwa kwa hamu kubwa.
Tuesday, November 11, 2014
MSF: MBINU MPYA ZAHITAJIKA KUKABILI EBOLA
Mbinu mpya mbalimbali zinahitajika kwa ajili ya kupambana na virusi vya Ebola nchini Liberia, shirika la madaktari wasio na mipaka, MSF limeeleza.
Zaidi ya Watu 6,000 wameathiriwa na ugonjwa huo nchini Liberia lakini takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya maambulizi mapya imeendelea kupungua.
MSF imesema kuwa imekuwa na uwezo mkubwa wa kuwa na vituo vingi vya kupambana na maradhi hayo kuliko idadi ya wagonjwa.
Mfano kituo kimoja mjini Monrovia kilikua na vitanda 250 lakini kimekua kikitibu wagonjwa 50 pekee, hivyo shirika hilo limeomba kubadilishwa kwa mbinu za mapambano dhidi ya ebola
Liberia ni nchi iliyoathirika zaidi na ugonjwa wa
Ebola kwa karibu ya nusu ya idadi ya walioathiriwa wa ugonjwa huo Afrika magharibi.
Hivi sasa kiasi cha maambukizi kinaendelea kuwa juu nchini Guinea na Sierra Leone
BURIANI KWA RAIS MICHAEL SATA ZAMBIA
Mazishi ya kitaifa yanafanyika nchini Zambia kumuaga hayati Rais wa nchi hiyo Michael Sata aliyefariki hospitalini mjini London Uingereza mwezi jana.
Sata alikuwa na umri wa miaka 77.Katika wiki chache zilizopita, wanachi wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye mwili wake ulikuwa
umelazwa katika majengo ya bunge
Mazishi ya kitaifa yanafanyika nchini Zambia kumuaga hayati Rais wa nchi hiyo Michael Sata aliyefariki hospitalini mjini London Uingereza mwezi jana.
Sata alikuwa na umri wa miaka 77.Katika wiki chache zilizopita, wanachi wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye mwili wake ulikuwa umelazwa katika majengo ya bunge.
Monday, November 10, 2014
MAPIGANO MAPYA YAZUKA SUDAN KUSINI
Mapigano
mapya yamezuka katika majimbo matatu nchini Sudani kusini , siku chache
baada ya pande mbili hasimu kukubaliana kumaliza mzozo ambao umekuwepo
kwa miezi 11.
Wiki iliyopita, Raisi wa Salva Kiir na Kiongozi wa waasi Riek Machar walikubaliana kumaliza mapigano kufuatia mazungumzo ya siku mbili nchini Ethiopia.
Serikali na Waasi wamekuwa wakinyoosheana kidole kuwa wamekuwa wakitekeleza mashambulizi katika jimbo la Upper Nile,Unity na Jonglei.
Msemaji wa Waasi Brigedia Jenerali Lul Ruai Koang ameishutumu Serikali kwa kuanzisha mashambulizi dhidi yao hasa katika maeneo yenye mafuta katika jimbo la Unity.
Lakini msemaji wa Jeshi Philip Aguer amesema vikosi vya waasi ndivyo vilivyoanzisha mapigano, kisha wao haraka wakajibu mashambulizi.
Mazungumzo yanayoratibiwa na jumuia ya IGAD,ambayo imetoa muda wa siku 15 kwa pande zote mbili kufikia makubaliano kumaliza mzozo.IGAD imetishia kuweka vikwazo ikiwemo marufuku ya kusafiri na usafirishaji wa silaha,ikiwa makubaliano hayatafikiwa kwa kipindi kilichotolewa.
Maelfu ya Watu wameuawa kwenye mapigano ya Sudani kusini na wengine milioni 1.8 wamekimbia mapigano tangu yalipoanza nchini humo katikati ya mwezi Desemba mwaka jana.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako
Saturday, November 8, 2014
TODAY
Stori 5 Hot Magazeti ya leo Tanzania November8, 2014
MWANANCHI Wafanyakazi wapya katika hospitali ya taifa ya Muhimbili MNH
wamelalamikia kutolipwa mishahara kwa miezi minne sasa huku uongozi
ukishindwa kuwapa majibu ya ufumbuzi wa tatizo hilo. Wafanyakazi hao
zaidi ya5o waliajiriwa na Hospitali hiyo tangu mwezi wa nane mwaka...
Read More »
Kutana na Mapacha wanaoshirikiana kila kitu hadi Uhusiano wa kimapenzi
Huwa si kitu cha ajabu kuona mapacha wakifanana kila kitu ndani ya familia hadi kusababisha watu kuwachanganya pindi wanapokutana nao kama hawajawazoea kuwaona kila siku. Na mara nyingi mapacha wamekua wakishirikiana katika vitu mbalimbali lakini haijawahi kufikia hatua ya kushirikia... Read More »
Picha 15 za Usiku wa Damian Soul na watu wake ziko hapa….
Usiku wa Nov 7 Damian Soul amezindua video ya single yake ‘Ni Penzi’ aliomshirikisha rapper kutokea Arusha (87.9CloudsFM) Joh Makini.Uzinduzi huo umefanyika katika ufukwe wa bahari Escape One uliopo Mikocheni Dar es Salaam.Katika uzinduzi huo Damian Soul alitumbuiza live bendi....
Subscribe to:
Posts (Atom)