Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa KCMC, Paul Mhumba amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kutuma ujumbe wa simu ya mkononi (sms) kwa Rais Jakaya Kikwete.
Kuvuja
kwa ujumbe huo na nambari ya simu iliyotuma, kumeibua hisia tofauti
kuhusu usiri wa ofisi ya Rais katika kushughulikia malalamiko nyeti ya
wananchi na kuwaweka njiapanda watoa habari za siri.
Mhumba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Tawi la KCMC anadaiwa na Menejimenti ya KCMC kuwa ndiye aliyetuma ujumbe huo.
Katika barua yake ya Mei 5, ilidai uchunguzi umebaini kuwa Mhumba ndiye mtumaji wa ujumbe huo.
“Uongozi
umepokea taarifa iliyotumwa mwishoni mwa Aprili na mwanzoni mwa Mei
mwaka huu kwa njia ya ujumbe wa simu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk Jakaya Kikwete,” .
KCMC
imedai katika barua hiyo, taarifa hiyo ya sms ilibeba ujumbe
unaohusiana na matumizi mabaya ya fedha za hospitali hiyo unaofanywa na
baadhi ya viongozi na Shirika la Msamaria Mwema (GSF).
Mbali
na tuhuma hizo, lakini pia KCMC inadai taarifa hiyo ilimweleza Rais
kuwa KCMC na GSF linalomiliki hospitali hiyo, zinajitosheleza kwa
mapato, hivyo hakuna haja kwa Serikali kuendelea kuipatia ruzuku.
Pia,
menejimenti imedai taarifa hiyo ilidai wafanyakazi wa KCMC
wanatumikishwa kama watumwa, hivyo ni maombi yao (watumishi) Serikali
ilegeze masharti ili ajira zao zichukuliwe na Serikali.
No comments:
Post a Comment