Siku
moja baada ya mgomo wa madereva kumalizika madereva 15 wa daladala na
mabasi makubwa wamesimamishwa kazi na wamiliki wa mabasi hayo kwa madai
ya kujihusisha na mgomo huo.
Katibu
wa chama cha madereva BW RASHID SALEHE ametoa taarifa hiyo jijini dar
es salaam ambapo amesema madereva 18 wamefikishwa mahakamani huko mkoani
dodoma na kuongeza kuwa endapo wangekuwa na mikataba wanayopigania hivi
sasa wasingefukuzwa kazi kienyeji namna hiyo.
Akizungumzia
kamati iliyoundwa na serikali kushughulikia suala hilo baada ya mkuu wa
wilaya ya kinondoni kuwaahidi kuwa ile iliyoundwa na waziri mkuu
itafanyiwa maboresho wamesema hawana imani nayo baada ya idadi ya
wamiliki ambao ndiyo wanaowalalamikia kuwa kubwa zaidi yao.
Madereva
hao wana madai ya msingi matano ambayo ni pamoja na mikataba bora ya
kazi, faini za mara kwa mara hata kwa kosa linalohitaji onyo, ukaguzi
uliopitiliza, kwenda kusoma kila baada ya leseni kuisha muda wake na
mwendo wa kilomita 80 kwa saa madai yaliyosababisha mgomo uliotikisa
nchi.
No comments:
Post a Comment