Mbunge wa Jimbo la
Mbeya Joseph mbilinyi akitema cheche
kwenye viwanja vya siasa Wilayani Kyela
Jana
Sehemu ya wananchi
wilayani Kyela Mbeya wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe
kwenye viwanja vya mchaga jana.
Mwenyekiti wa Chadema
Taifa Freeman Mbowe akikagua gwaride la Red Briged linalohusika na ulinzi
wilayani Kyela kabla ya kuanza kutema cheche wilayani Kyela.
Mbowe akitema cheche
kwenye uwanja wa siasa wilayani Kyela.Picha zote na Ibrahim Yassin.
IMEELEZWA
kuwa misingi mibovu ya kutozingatia utawala bora kwa wananchi unaofanywa na
Chama cha Mapinduzi (CCM)ndiyo sababu ya wananchi kushindwa kutumia lasilimali
za nchi na kupelekea kuishi maisha duni huku baadhi ya viongozi wa serikali
wakiendekeza uwizi bila kuchukuliwa hatua.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Freeman Mbowe wakati akizungumza na wananchi wa Kyela Mbeya kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Siasa uliohudhuriwa na maelfu
ya wananchi kutoka kata mbalimbali.
Alisema
chama cha Mapinduzi wakati wa utawara wa Ally Hassan Mwinyi waliua azimia la
Arusha lililoanzishwa na Hayati Mwl,Julius Nyerere na kuruhusu mambo yasiyo na
msingi,na kuwa katika utawara wa Benjamini Mkapa Chama hicho kiliuza viwanda
vyote vilivyokuwa na tija kwa wananchi.
Mbowe
alisema viwanda ambavyo walishindwa kuviuza walileta wawekezaji kutoka nje
kuwapa umiliki lasilimali za nchi na kuwanyima wazawa na kuwa kibaya zaidi
wameuziana nyumba za serikali kwa bei ya mchicha bila kujali athari zinazoweza
kujitokeza kama ilivyo hivi sasa ambapo chama hicho kimepoteza sifa.
Aliongeza
kuwa kutokana na ali hiyo ndiyo maana Chadema ikaasisiwa kwa lengo la
kuwakomboa wananchi ili waweze kupata nafuu ya maisha na kuzitumia lasilimali
zao na kuwa aliwataka waachane na Chama cha Mapinduzi kwa kuwa kinasera ya
ufisadi kimeshindwa kuwajali watu wake.
Mbowe
aliwataka watanzania kujifunza toka katika nchi za marekani,uingereza,Kenya,Malawi,Zambia
na zinginezo ambazo wakikiweka madarakani chama furani kama hakikufanya kazi
wanakipiga chini kwenye uchaguzi mungine na kuwa hata chadema ikiingia
madarakani waipige chini pindi itakavyofanya vibaya.
‘’Haiwezekani
lasilimali za nchi zinaendelea kuibwa kuku wakibeba wanyama poli zikiwemo twiga
kwenda nje ya nchi kuuzwa alafu muendelee kuwachekea,mwezi wa kumi ndiyo kiama
chao chagueni madiwani,wabunge na Rais kutoka Ukawa ili tufanye mabadiriko ya
kweli’’alisema Mbowe.
Mbunge
wa jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kwa upande wake aliwapongeza wananchi
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuwa ndiyo
ishara tosha ya anguko la CCM katika uchaguzi mkuu wa mwezi wa kumi katika
ngazi zote.
Alisema
Rais Jakaya Kikwete alimzawadia Mbunge wa Kyela Harrison Mwakyembe uwaziri wa
uchukuzi kwa lengo la kuiba kamailivyojulikana baada ya kununua mabehewa mabovu
pamoja na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari kwa chama chake bila kufuata
utaratibu huku jimbo la Kyela likizidi kuwa hoi kiuchumi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment