Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bi. Theo Ntara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Kyela (watatu kutoka kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt.
Hamza Kabelwa (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na
washiriki wa warsha inayohusu uboreshaji wa huduma za hali ya hewa
katika maeneo ya Ziwa Nyasa kwa sekta ya wakulima na wafugaji, wavuvi na
wasafirishaji, tarehe 14 Mei 2015 katika hotel ya Kyela Resort-Mbeya
Mamlaka
ya Hali ya Hewa kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani
kupitia mpango wa utoaji wa huduma za hali ya hewa wa GFCS yaani “Global Framework for Climate Services” imezindua
rasmi huduma ya kutoa taarifa za hali ya hewa hususan tahadhari na
utabiri mahususi kwa watumiaji wa ziwa nyasa. Taarifa hizo zitasamabazwa
kupitia vyombo mali mbali vya habari ikiwemo redio za kijamii. Huduma
hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 11 Mei 2015 huko Kyela mkoani Mbeya na
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dkt. Thea Ntara aliyemuwakilisha Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya.
Katika kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu TMA wameandaa warsha ya“UBORESHAJI
NA UAINISHAJI WA MAHITAJI YA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA MAENEO YA
ZIWA NYASA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI, WAVUVI NA WASAFIRISHAJI’’ iliyofanyika katika
hotel ya Kyela Resort jijini Mbeya. Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya Bi. Thea Ntara alisema ‘Hivi karibuni tumeshuhudia matukio ya
mvua ya mawe, mafuriko na radi katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya,
hali hii imesababisha madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi.
Nimatumaini yangu kuwa taarifa zinazopatikana kutoka kwa wananchi na
wataalam mbalimbali kupitia semina hii zitaiwezesha Mamlaka ya Hali ya
Hewa kuboresha taarifa zake kwa umma na kuwawezesha watalaam kutoa
ushauri stahiki unaozingatia taarifa za hali ya hewa’. Alizungumza hayo
wakati akifungua rasmi warsha ya wadau wa hali ya hewa wanaotumia ziwa
nyasa iliyowajumuisha wasafirishaji, wakulima, wavuvi, wafugaji, Ofisi
ya Bandari, SUMATRA,usalama, Maafa, maliasili na vyombo vya habari.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi katika hotuba yake
iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Utabiri TMA Dkt. Hamza Kabelwa alisema
‘Katika kuhakikisha TMA inazidi kuziboresha huduma zake, wataalam wa TMA
wameweza kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyela ili kupata
uelewa zaidi wa majanga yanayoikumbuka wilaya hiyo na namna gani ya
kuweza kufanyia kazi’. ‘TMA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
vikiwemo vyombo vya habari imejikita katika kuhakikisha jamii inapata
taarifa za hali ya hewa kwa wakati hususan kunapokuwa na vipindi vya
matukio ya hali mbaya ya hewa kama vile mvua kubwa, ukame, upepo mkali,
mawimbi makubwa n.k kwa lengo la kuisaidia jamii kuchukua tahadhari
mapema ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na matukio
hayo hivyo kuchangia katika kuokoa maisha ya watu na mali zao’ alisema
Dkt. Kijazi.
No comments:
Post a Comment