Orodha ya wahitimu wa shahada na stashahada waliopangiwa katika halmashauri mbalimbali inafanyiwa marekebisho baada ya kubainika kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa (Sebastian Kolowa University College-SEKUCO) cha Lushoto uliwasilisha orodha ya wahitimu wapatao 491 wa mwaka 2013 ambao walishaajiriwa badala ya wahitimu wa mwaka 2014.
Kutokana
na sababu hiyo, orodha tajwa imesitishwa kwa muda ili kufanyiwa
marekebisho na kuwekwa orodha sahihi itakayojumuisha wahitimu wa SEKUCO
wa mwaka 2014.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na kasoro hiyo.
Imetolewa na;
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
No comments:
Post a Comment