https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=jgloS7DiOLo
MAAJABU!
Mtoto Irene Emmanuel Joseph (1) mkazi wa Kibamba-Mji Mpya jijini Dar,
ameendelea kuwa gumzo kufuatia kufariki dunia Agosti, mwaka jana akiwa
na miezi 9 na kudaiwa kufufuka katika mazingira ya ajabu hivi karibuni
akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi minne.
Tukio
la kupatikana kwa mtoto huyo akiwa hai lilitikisa Jiji la Dar, Jumamosi
iliyopita ambapo umati ulifika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo ili
kumshuhudia kwa macho.
MAZINGIRA YA KIFO CHAKE
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi nyumbani hapo, mama mzazi wa mtoto huyo,
Helena Raphael alisema kuwa, ilikuwa Agosti mwaka jana akiwa kwenye eneo
la biashara yake, Mbezi Mwisho, Dar, Irene aliugua ghafla. Alionesha
kulegea na kuwa kama mtoto mwenye degedege.
“Nilimwambia
mume wangu, tukampeleka kwenye zahanati moja iliyopo palepale Mbezi
ambapo daktari akabaini kuwa tatizo la mwanangu ni kubwa hivyo
akatushauri tumkimbize Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Pwani ambapo
iligundulika kwamba alikuwa na upungufu mkubwa wa damu.
“Pale
hospitali madaktari walianza kutafuta mishipa ili wamchome kwa lengo la
kumwongezea damu lakini cha ajabu mishipa ya mwanangu ikawa inavimba
tu. Ilipofika saa 6 usiku, alifariki dunia bila kuwekewa damu. Nililia
sana kama mzazi!”
Irene Emmanuel akiwa na baba'ke |
MAITI YAMDUWAZA MAMA MTU
“Baada
ya kifo, sikuwahi kuuona mwili wa mwanangu maana waliupeleka mochwari.
Siku ya kuaga mwili hapa nyumbani kwa ajili ya mazishi, nilishangaa sana
kumwona mwanangu ana alama ya duara kwenye shavu kama zile alama za
Wamasai.
“Niliwasimulia
baadhi ya waombolezaji wakasema kwa upande wao waliuona mwili wa
mwanangu ukitoka jasho jingi kama mtu aliyetoka kufanya kazi ngumu juani
na ulivimba sana,” alisimulia mama huyo na kuongeza:
“Pamoja na hayo, tulimzika mwanangu kwenye makaburi yaliyopo hapahapa Mji Mpya huku tukiwa na shaka juu ya kifo chake.”
MAMA AANZA KUZUNGUKA MAKANISANI
Helena
anasema baada ya mazishi, alianza kwenda kwenye makanisa mbalimbali
kumwomba Mungu amrejeshe mwanaye na mwishowe akajikuta amefika kwenye
kanisa la Nabii Flora lililopo Salasala, Dar ambako aliambiwa mtoto wake
alikuwa hai.
“Nilikuwa
naenda kusali kila siku ndipo siku moja Nabii Flora alinifuata na
kuniambia mwanangu hajafa alikuwa yupo sehemu lakini nguvu zake haziwezi
kumrudisha tena.
MGANGA ADAI AMEMPATA MTOTO
“Siku
ya kwanza kumpigia simu huyo mganga alituambia tushike shilingi mia
moja mkononi, tukafanya hivyo, akasema kweli mtoto wetu yupo hai na
atamrudisha. Siku chache mbele tulimtumia hela alizotuagiza na
akatuambia tusafiri kwenda Dodoma tukamchukue mtoto wetu kwani tayari
alishampata.”
WAZAZI WAONANA NA MTOTO
Helena
anasema kuwa, Februari mwaka huu yeye na mume wake walisafiri mpaka
Dodoma eneo la Pandambili na kuonana na mganga huyo akiwa na mtoto wao
ambaye alionekana kutokuwa na afya nzuri. Walitakiwa wamuache kwa muda
ili aendelee na matibabu mpaka arejee kwenye hali ya kawaida.
MGANGA ATINGA DAR NA MTOTO
“Baada ya miezi miwili
kupita mganga alitutaarifu kuwa anakuja Dar na mtoto. Kweli, alifika
hapa usiku wa Aprili 10 akiwa na mtoto wetu ambaye kwa sasa ni mzima
kabisa.
“Tuna furaha sana kuonana
na mwanetu tena haya kweli ni maajabu ndiyo maana watu wengi wamefika
hapa kushuhudia na wengine wamelala hapahapa tangu jana,” alisema mama
huyo.
MGANGA ANENA
Naye
mganga aliyedai kumfufua mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Bino
alikiri kupokea simu kutoka kwa wazazi hao na kusema:
“Niliongea
na mizimu ikaniambia mtoto yupo hai katika mazingira ya kawaida ila
alichezewa kimazingara. Nimewasaidia wengi tu na ninao watu wengi
niliowarudisha huko Dodoma,” alisema mganga huyo.
MJUMBE ATHIBITISHA KUZIKWA KWA MTOTO HUYO
Mjumbe
wa mtaa huo, Maimuna Abdallah alithibitisha kupokea taarifa ya kifo cha
mtoto Irene, Agosti mwaka jana na kuongeza kuwa yeye ndiye aliyetoa
barua ya utambulisho wa makazi kwa baba mzazi wa mtoto huyo ili aweze
kupatiwa mwili wa mwanaye kutoka Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya
mazishi.
“Na mimi nimeshangazwa
sana na tukio hili kwa sababu tangu nizaliwe sijawahi kusikia wala kuona
mambo haya, niwaambieni tu kuwa kweli yametokea mtaani kwangu,” alisema
mjumbe huyo.
MAJIRANI WAO
Baadhi ya majirani na
wazazi wa Irene walisema kwamba, japokuwa mtoto huyo alifariki dunia
mwaka jana na kuzikwa lakini walivyomwona wao ni yeye yule waliyemzika!
“Yaani hakuna shaka
kabisa kwamba huyo mtoto ni Irene mwenyewe, sijui nini kilifanyika
lakini kusema kweli ni mwenyewe na kweli kifo chake kiliacha maswali
hapa mtaani,” alisema jirani mmoja.
KABURINI
Ili
kuthibitisha kuzikwa kwa mtoto huyo, mwandishi alifika kwenye kaburi
alilozikwa mtoto Irene mwaka jana na kulikuta limeshaota majani huku
mchwa wakiwa wameanza kuutafuna msalaba sehemu ya chini.
Msalaba huo ulisomeka hivi; IRENE EMMANUEL, KUZALIWA 01/10/2013. Hata hivyo, sehemu yenye tarehe ya kifo ndiyo ililiwa na mchwa.
MPANGO WA KULIFUKUA KABURI
Baba mzazi wa Irene alipoulizwa kama wana mpango wa kulifukua kaburi alilozikwa binti yake, alisema hawajafikiria hilo.
KWA SASA IRENE
Kwa sasa, mtoto Irene
yuko kwa wazazi wake huku mganga huyo akisema ataendelea kumpatia dawa
mpaka atakapoimarika zaidi na kuendelea na makuzi.
CHANZO:GPL
https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=jgloS7DiOLo#t=22
No comments:
Post a Comment