Wanafunzi
wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu
cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao
................................................................................ Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa
al-Shabaab wamevamia na kushambulia chuo kikuu cha Garissa kilichopo katika mji
wa Garissa. Zaidi ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 53
wamejeruhiwa.
Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema
kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi
walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye
swala ya asubuhi.
Polisi waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika
eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao
walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.
Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya
risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
Wanafunzi
waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna
majeruhi wengi sana.
Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa
idadi ya wavamizi hao ni angalau watano na bado kuna wanafunzi na
maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.
Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka
waliowashikilia.
Mateka mmoja (mwanafunzi) mwenye asili ya
Somalia aliyeachiwa huru na magaidi hao ameviambia vyombo vya habari vya
Kenya kuwa zaidi ya wanafunzi kadhaa wamekwishauawa na miili yao
imetapakaa ndani ya vyumba na madarasa huku zoezi la Uchinjaji wa mateka
wengine walio hai likianza.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia
za wale waliouawa katika shambulizi hilo.
Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo
maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao. |
No comments:
Post a Comment