TAASISI
ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya
mikopo kwa watumishi wa wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, mwishoni
mwa wiki ilizindua tawi lake jipya la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya,
huku Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Staki Senyamule, akiwataka wananchi
wake kukopa kwa sababu maalum.
Mkuu
wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Rosemary Senyamule kulia, akionyeshwa
nyaraka za ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services.
Wageni
mbalimbali wakiangalia shughuli za uzinduzi wa tawi jipya la taasisi ya
kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakisoma vipeperushi vya taasisi ya kifedha ya
Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Meneja
wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Bayport Financial Services, Alpha
Akim, akizungumza jambo katika uzinduzi wa tawi lao la 80 wilayani
Ileje, mkoani Mbeya.
“Kwanza nawapongeza mno
wenzetu wa Bayport Financial Services kwa kuamua kuja kufungua tawi hapa
katika wilaya yetu ya Ileje, ila ni muhimu wananchi kukopa kwa sababu
maalum ili waweze kuendeleza maisha yao kwa kutumia vyema fursa za
mikopo Tanzania.
“Tukifanya hivyo tunaweza kupata maisha bora kwa
sababu tutajimudu kiuchumi, hivyo ni wakati wetu kufurahia kuanzishwa
kwa huduma za taasisi hii hapa kwetu ileje, maana ndio kwanza wanafungua
tawi lao hapa,” alisema.
Naye Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini, Alpha Akim, alisema kufungua kwa tawi hilo pia ni sehemu ya
kutoa ajira kwa vijana sanjari na kuongeza kipato kwa watumishi wa umma
na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa kwa kupitia fursa nzuri ya
mikopo.
“Watu mbalimbali watapata mwangaza mzuri wa kiuchumi
wakiwamo wale watakaopata nafasi ya kufanya kazi nasi, hususan ile ya
uwakala, bila kusahau wale watakaokopeshwa bila amana wala dhamana.
“Naomba
wananchi na wakazi wa Ileje watumie vyema fursa ya uwapo wa taasisi hii
wilayani kwao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wote kwa pamoja
tunafanikisha kwa vitendo ndoto ya kukuza uchumi wetu na wa Tanzania kwa
ujumla,” alisema Akim, Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Bayport.
Bayport
Financial Services ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na utoaji
mikopo mbalimbali kama vile fedha taslimu, mikopo ya bidhaa, bima ya
elimu kwa uwapendao, ambapo mikopo hiyo inaweza kutolewa ofisini au kwa
njia rahisi ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.
No comments:
Post a Comment