Hali
ya taharuki imewapata wakazi wa kijiji cha Park Nyigoti kata ya ikoma
wilaya ya Serengeti baada ya mahakama kutoa ruhusa ya kufukuliwa kwa
mwili wa Bi. Celina Jumapili aliyefariki dunia na kuzikwa tarehe tatu
Machi kisha kuonekana utata katika kaburi lake.
Kufuatia
hali hiyo leo kaburi lake limefukuliwa na kukuta sehemu ya viungo vya
mwili wake vimekatwa vikiwemo kiganja cha mguu vidole vya mkono wa
kushoto na sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa hali iliyozua mashaka
makubwa kwa wakazi wa kijiji hicho.
Mwandishi
wa habari hzi alifika katika kijiji cha Park Nyigoti wilayani Serengeti
na kushuhudia zoezi la kufukua kaburi likiendelea ambapo inadaiwa kuwa
marehemu Celina alifariki dunia tarehe mbili ya Machi na kuzikwa tarehe
tatu lakini tarehe ishirini na mbili ndugu walikuta sehemu ndogo ya
kaburi likiwa limefukuliwa.
Hali
hiyo ndiyo ikawafanya wananchi wakataka kuhakiki kuwa mwili wa ndugu
yao upo au umechukuliwa na baada ya kupata kibali cha mahakama
wamefukua na kukuta viungo hivyo vikiwa vimekatwa na watu wasio
julikana.
Akielezea
namna tukio ilo lilivyo tokea mama wa marehemu Celina Bi Nyahende
Kwihamba amesema tukio hilo limewaweka katika mashaka makubwa kutokana
na kijiji hicho kushamiri kwa tabia ya ushirikina na kuiomba serikali
isaidie kumaliza tabia hiyo.
Kijiji
cha Park Nyigiti mara kwa mara kimekuwa na matukio ya kikatili kwani
tarehe mbili ya mwezi marchi watu watano waliuawa na wananchim kwa
kuwatuhumu kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina na tarehe saba ya
mwezi wa pili kijiji jirani cha lubanda waliuawa watu wawili na kuchoma
moto nyuma saba kwa kama tuhuma hizo hizo.
No comments:
Post a Comment