VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Tuesday, April 19, 2016

Video 8 za Mambo Yote Yaliyojiri Bungeni Dodoma Leo





1.Hatimaye mkutano wa kwanza kikao cha 3 wa bunge waanza kwa wabunge kuimba wimbo wa taifa na baadhi yao kula kiapo.
 https://www.youtube.com/watch?v=iV2ZYeyJyRU#action=share
 
2.Je ni nini hatma ya uchaguzi kwa majimbo ya Bulyankulu na kamindo ikiwa uchaguzi haujafanyika hadi leo? Dkt. Abdallah Possy atoa ufafanuzi. 
 
3.Mhe. Suleiman Jafo atoa ufafanuzi na utaratibu wa serikali juu ya hospitali zinazopandishwa hadhi kukidhi haja za wananchi.
 
4.Mbunge wa Njombe mjini aihoji serikali juu ya upigaji marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki unaosababisha uharibifu wa mazingira. 
 
5.Naibu waziri wa nishati na madini Dkt Medard kalemani atoa ufafanuzi wa kuanza kwa mradi wa kuzalisha umeme wa Malagarasi. 
 
6.Je serikali inaweka msukumo gani kwa Geita Gold Mining kuhakikisha inawalipa wananchi wa mtaa wa Mgusu fidia ili kupisha eneo hilo? 
 
7.Kauli ya Wizara ya mambo ya ndani kuhusu baadhi ya vituo vya polisi nchini kuwa na askari wachache na kutofanya kazi kwa masaa 24.
 
8.Je ni lini uwanja wa ndege wa Musoma utajengwa na kuwa kwenye hadhi ya stahiki ya kitaifa au kimataifa? Mhe. Joyce Sokombi ahoji.

VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Friday, April 15, 2016

Bibi Kizee Abakwa Mkoani Singida



Pichani ni Bibi kizee mwenye umri wa miaka 84 na mkazi wa Kijiji cha Chungu, tarafa ya Ihanja, wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida akiwa amebebwa na mmoja wa ndugu zake wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Singida kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 (jina lake halikupatikana) anayetuhumiwa kumbaka bibi kizee huyo kwa mara ya tatu sasa ndipo walipofanikiwa kumkamata. (Picha Na Jumbe Ismailly)
VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Monday, April 11, 2016

KITUMBUA Kimeingia Mchanga...Ikulu Yafuta Safari ya Wakuu wa Wilaya 10 Kwenda China China




Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi

Ikulu imefuta safari ya wakuu wa wilaya 10 na wakurugenzi idadi kama hiyo waliotakiwa kwenda China kwa mafunzo ya uchumi wa kimaeneo kuanzia jana, na kuna uwezekano mkubwa ikatangaza uteuzi mpya leo.

Wakuu hao wa wilaya na wakurugenzi wao  walikuwa waondoke jana kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China, lakini habari zinaarifu kuwa Ikulu iliamua kutotoa kibali, hali inayozidisha ubashiri kuwa uamuzi huo umetokana na kukamilika kwa uteuzi wa wakuu wapya.

Safari hiyo ilishakamilika kwa kiwango kikubwa baada ya kupata visa na wengi wao kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa safari hiyo, lakini wakalazimika kurejea kwenye vituo vyao baada ya kukosa kibali cha Ikulu ambacho hutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi.

Mara tu baada ya kuapishwa Novemba 5 mwaka jana, Rais John Magufuli alitangaza kudhibiti safari za nje za watumishi na viongozi wa umma kwa kuagiza kuwa Ikulu ndiyo itakayotoa kibali baada ya kujiridhisha na umuhimu wa safari hizo kwa Taifa.

Tangu atoe agizo hilo, ni mawaziri wawili tu ambao wameruhusiwa kwenda Vietnam kwenda kujifunza kilimo na viwanda. Mawaziri hao ni Mwigulu Nchemba (Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi) na Charles Mwijage (Viwanda na Biashara).

Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashatu Kijaji alikwenda nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa fedha, wakati kwa nyakati tofauti Makamu wa Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walikwenda Afrika Kusini na Botswana.

Mpaka sasa, Rais Magufuli amefanya safari moja tu ya nje alipokwenda Rwanda kwenye maadhimisho ya mauaji ya kimbari.

Lakini safari ya wakuu hao wa wilaya ilikuwa ifadhiliwe na China, kwa mujibu wa habari hizo na hivyo isingeisababishia Serikali kutumia vibaya fedha za walipa kodi.

Uamuzi huo unaonekana kuzingatia zaidi uteuzi wa wakuu wapya ambao taarifa zinasema unaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, wakati wa wakurugenzi wa wilaya unatazamiwa kutangazwa baadaye wiki hii au wiki ijayo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alikiri kuwapo kwa safari hiyo, lakini akasema hajui kama imeidhinishwa na Ikulu kwa kuwa si muhusika.

“Katika hatua za awali nilisaini safari hiyo kuwaruhusu waende China, lakini sijui kama wamenyimwa kibali kwa sababu hilo si suala la ofisi yangu,” alisema Waziri Simbachawene.

Kama ni kweli, alifafanua Simbachawene, inaweza kuwa ni kutokana na umuhimu wao wa kuwatumikia wananchi kwenye maeneo wanayotoka. “Hawawezi kuondoka na kuziacha wilaya zao ilhali wao ndiyo waangalizi,” alisema Simbachawene.

Akiwa Chato mkoani Geita, Rais aliwataka wakuu wa wilaya kuchapa kazi badala ya kuwa na woga wa kutoteuliwa akisema uchapaji kazi ndio utawafanya waendelee kuwapo kwenye nafasi zao.

Rais pia amekuwa akitoa maelezo kadhaa yanayoonyesha atafanya uteuzi kwa kutumia vigezo hivyo, hasa suala la elimu ambayo inakabiwa na tatizo kubwa la uhaba wa madawati na vyumba na majengo, kipindupindu, njaa, migogoro ya ardhi na watumishi hewa.






VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......