VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Wednesday, February 24, 2016

Mtoto wa Miaka Mitatu Abakwa Na Kunyongwa Hadi Kufa




Mtoto mwenye umri wa miaka 3 na miezi 4 Mariam Deogratius mwanafunzi wa shule ya awali ya Makoko iliyopo katika Manispaa ya Mji wa Musoma mkoani Mara, amebakwa kisha kunyongwa hadi kufa na mtu asiyejulikana Usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara kamishna msaidizi Philllip Kalang amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linafanya Msako kuhakikisha Mhalifu anapatikana.
VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Tuesday, February 23, 2016

Magufuli Atinga GHAFLA Kivukoni na Magari yenye Namba za Kawaida



Rais John Magufuli ameendelea kufanya ziara za kushtukiza, baada ya kutembelea ofisi za Kivukoni Dar es Salaam kimyakimya juzi jioni kuangalia mwenendo wa utoaji huduma za vivuko.

Mashuhuda waliokuwepo eneo hilo Jumapili jioni wakati Rais anafanya ziara hiyo, walieleza mtindo alioingia nao Dk Magufuli ulikuwa ni wa kawaida na vigumu kwa mwananchi wa kawaida kung’amu uwapo wa Rais.

Mfanyabiashara wa eneo hilo, Sharif Mkamba alisema Rais Magufuli aliingia saa 11 jioni akiwa na msafara wa magari matatu ya kawaida yaliyokuwa na namba za kiraia.

“Hakukuwa na king’ora chochote kama tulivyozoea bali ulikuwa ni msafara wa kimya kimya. Aliingia moja kwa moja kwenye zile ofisi na alitumia kati ya dakika 10 hadi 15 kabla ya kutoka,” alisema Mkamba.

Said Likoko alisema kuwa baada ya kugundua kati ya magari matatu alikuwepo Rais, walisogea kufuatilia kwa kina kwa kuwa haijazoeleka na walitegemea huenda baadhi ya watumishi wangewajibishwa.

“Aliteremka na kumuuliza aliyemkusudia na taarifa tulizozipata jana zinadai hakumkuta huyo bosi, sijui ni meneja au ofisa sisi hatujui,” alisema Likoko ambaye hujishughulisha pia na biashara ndogondogo eneo la kivukoni.

Likoko alisema pamoja na kwamba aliingia kimya kimya, Rais Magufuli hakusita kuwasalimia wasafiri waliokuwa wakisubiri kivuko wakati alipofanya ziara hiyo.

Alieleza kuwa kama wananchi walifurahishwa na hatua hiyo ya Rais, kwa kuwa watendaji wengi hawafanyi kazi siku za wikiendi licha ya huduma zake kufanyika siku zote.

Tangu jana asubuhi kumekuwa na video inayosambaa ikimuonyesha Rais Magufuli akiwa Kivukoni akitembea kwa miguu ndani ya eneo hilo huku akishangiliwa na wasafiri waliokuwa wakingoja kivuko.

Hata hivyo, jitihada za kutafuta mamlaka husika kueleza kwa undani malengo ya ziara hiyo ziligonga mwamba baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kutopokea simu.

Ofisa habari wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Theresia Mwami, alitaka utafutwe uongozi wa juu kueleza yaliyojiri kwenye ziara hiyo kwa kuwa yeye yupo likizo.

VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Tuesday, February 9, 2016

Mbuzi Na Kondoo 200 Wakatwakatwa Mapanga Wakituhumiwa Kuvamia Shamba La Mkulima Huko Mvomero Morogoro



Zaidi ya Mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero Mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la Mwanu ' 
 
Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu ekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya kimasai
 
Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.
 
Waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio .
VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Sunday, February 7, 2016

Polisi Watatu Wafa Ajalini Msafara wa Rais Magufuli


Askari polisi watatu wamefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya gari lao lililokuwa kwenye msafara wa Rais John Magufuli kutoka Singida kwenda Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka.
Rais Magufuli alikuwa mjini Singida alikokuwa amekwenda kushiriki maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.

Hiyo ni mara ya pili kwa askari kufariki wakiwa kwenye msafara wa Dk Magufuli baada ya aliyekuwa akiongoza msafara wake wakati wa kampeni kugongana na dereva bodaboda katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Askari huyo alikuwa kwenye pikipiki maalumu iliyokuwa ikiongoza msafara wakati Dk Magufuli akitoka katika Hospitali ya Lugalo kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka alisema ajali hiyo ilitokea saa 9.40 alasiri, katika Kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi mkoani humo baada ya moja ya matairi ya gari hilo kupasuka na dereva kushindwa kulimudu.

Aliwataja waliofariki kuwa ni Mkaguzi Mwajelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerard.

Waliojeruhiwa ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Singida (RCO), Peter Majira (50
na PC Charles Simon (34) ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Gari hilo lililopata ajali ni lile lililokuwa limetangulia ili kufagia barabara kabla ya msafara wa Rais, likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha mkoa huo.

Sedoyeka alisema miili ya askari hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa huo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Kitundu Jacks alisema hali za majeruhi waliofikishwa kwenye hospitali hiyo zinaendelea vizuri.

“Mrope ndiye aliyeletwa akiwa kwenye hali mbaya, alikuwa amevunjika mbavu na mkono na akafa mara tu baada ya kufikishwa hospitalini hapa. Majeruhi wengine wamepata michubuko na wanaendelea vizuri,” alisema. 
VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Tuesday, February 2, 2016

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JKT



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama , Dk John Pombe Magufuli amemteua Brigedia Jenerali MW Isamuhyo kuwa mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamnyange amesema uteuzi wa Brigedia Jenerali Isamuhyo kuwa Mkuu wa JKT unafuatia kustaafu utumishi jeshini kwa Meja Jenerali Raphael Muhuga baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria.
Meja Jenerali Muhuga amestaafu utumishi Jeshini tarehe 31 Januari 2016 baada ya kutumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa muda wa miaka 43, ikiwemo miaka mitatu akiwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

IMETOLEWA NA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO,

MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA,

LEO TAREHE 30 JANUARI 2016


VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......