VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Monday, August 31, 2015

Wananchi Wafunga Barabara Baada ya Gari la Polisi Kugonga Wanafunzi wawili

 
Wananchi wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hii leo wamefunga barabara baada ya Wanafunzi wawili kugongwa na gari la Jeshi la Polisi na kupelekea kifo cha Mwanafunzi Mmoja

Akiongea na Mtandao huu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jaffary Mohammed amesema baada ya tukio hilo Wanachi walifunga barabara kutokana na hasira ya tukio lakini jeshi la Polisi limetuliza hali na linamshikilia Dereva wa gari hilo kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Jaffary ameongeza kuwa katika tukio hilo Mwanafunzi aliejeruhiwa amelazwa katika hospitali ya Tumbi na mwili wa marehemu upo mochwari katika hosptali hiyo.

Aidha Jaffari ameongeza kuwa kwa sasa hali ya kiusalama imetulia baada ya jeshi la polisi kutuliza hali iliyojitokeza huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi na badala yale wafuate sheria.
 
Katika hatua nyingine amewataka madereva wafate sheria za barabarani kwa kufuata alama zilizowekwa pamoja na kupunguza mwendo katika maeneo ya watu ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

ACT-Wazalendo wazindua kampeni, Mghwira aahidi serikali ya umoja Ambayo Waziri Mkuu Atakuwa Zitto Kabwe


CHAMA cha ACT Wazalendo kimezindua kampeni zake jijini Dar es Salaam kwa kuahidi kitakapopewa ridhaa ya kuongoza nchi, kitaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa. 
Aidha katika uzinduzi huo ambao viongozi mbalimbali wa chama hicho walihutubia, Mgombea Urais wa chama hicho Anna Mghwira alisema wananchi wakimpa ridhaa, waziri mkuu wake atakuwa Zitto Kabwe.

“Nitakapounda serikali, katika katiba, mtu wa kwanza kusaidiana na rais licha ya makamu, ni Zitto Kabwe, atakuwa Waziri Mkuu katika serikali ya kwanza,” alisema Anna Mghwira ambaye pia alisema atahusisha viongozi waadilifu kutoka CCM, Chadema na vyama vyote vya siasa na taasisi zote kiraia.

Akihutubia mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mbagala Zakhem, mgombea huyo, katika kuelekeza nia yake ya kuunda serikali hiyo ya umoja, alisema linapokuja suala la kitaifa, hakuna haja ya kuangalia masuala ya itikadi.
 
 “Mimi ni mama, hukusanya watoto wake.Hata mama wa vifaranga hukusanya vifaranga pamoja na kuviweka kwenye mbawa zake…mimi nina mbawa za moyo…nitaunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayotokana na sekta binafsi lakini kutoka watu wazalendo, wenye utu, waadilifu, taasisi za kijamii, mashirika ya kidini, makundi ya umma ili kuunda taswira ya nchi yetu.”

Mghwira alisema taifa linahitaji mabadiliko si ya tu kifikra na kisera, bali pia ya kijinsia kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa nchi. Alisema chama chake kinatilia mkazo utu, uzalendo na uadilifu.

Makao makuu Dodoma 
Aidha alisema, Serikali itakapoundwa itaapishwa Dodoma na watahakikisha wanarudisha kazi kubwa aliyoifanya Rais wa Kwanza, Julius Nyerere ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na serikali lakini siyo makao makuu ya chama.

Alisema kuweka mji huo makao makuu, maana yake ni kuleta watu wote kutoka pande zote za nchi.
 
Vipaumbele 
Alitaja vipaumbele vyake ni kuwa na mfumo imara na endelevu wa hifadhi ya jamii unaojengea uwezo wananchi kukabiliana na majanga. Alisema asilimia sita pekee ya Watanzania wanafaidika.

“Tutatumia hifadhi ya jamii kama nyenzo ya kukuza akiba nchini ili kuwe na vyanzo vya mitaji ya uwekezaji wa ndani…tutapanua hifadhi ya jamii kufikia makundi yote katika jamii ikiwamo wakulima, wafugaji, mama lishe na bodaboda,” alisema. 
 
Kipaumbele kingine alichoahidi ni uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora.

Alisema watu wengi hawana uhakika na maisha yao kimapato. Aidha alisema, watajikita kwenye uwekezaji wa kilimo na kusimamia uzalishaji wake.
 
 Aidha, aliahidi kuhakikisha ardhi na mashamba yote yaliyo chini ya mashirika ya umma, yanachukuliwa na kuwekwa chini ya uzalishaji mdogo.

Kwa upande wa viwanda, alisema atahakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinaongeza mapato ya fedha za kigeni. 
 
Chama hicho kupitia kwa mgombea, kimesema kitaweka msukumo kwenye bidhaa za nguo na vitakuwapo viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo.

Vipaumbele vingine ni kuhakikisha madini, mafuta na gesi, vinakuwa mali ya wananchi kikatiba. 
 
Kuhusu Katiba Mpya, alisema wataruhusu Tume ya Jaji Warioba imalize kazi ya katiba ilikoishia. Mgombea huyo aliendelea kutaja vipambele vyake kuhakikisha anaboresha huduma za afya ikiwamo kudhibiti vifo vya mama na mtoto.

Aliahidi kuondoa tatizo la watoto wa mitaani. Misamaha ya kodi kwa mujibu wake, haitazidi asilimia moja ya pato la taifa na wakati huo huo atadhibiti mianya ya ukwepaji kodi hususani kwa kampuni za kigeni.

Sifa za rais 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitila Mkumbo, alishauri wananchi kuangalia wagombea urais kama wanalinda haki za walio wengi au ni mateka wa matajiri. 
 
Mkumbo alisema, kiongozi mkuu wa nchi, kwa maana ya rais, ana kazi kuu nne ambazo ni fikra na kutoa dira ya nchi jambo ambalo anapaswa kuwa na uwezo wa kufikiri.

“Tatizo ni kufikiri na kutoa dira ya nchi…tunataka rais atakayetoa misingi ya nchi, atatuletea sera..,” alisema Kitila. 
 
Alisema kazi ya pili ya rais, ni kuwa mlinzi mkuu wa tunu za taifa huku akisisitiza katika tunu ya umoja, wananchi kuepuka mgombea mwenye tabia za kidini, kikabila na kikanda.

“Rais ndiye mlinzi wa usawa katika taifa…,” alisema na kushauri wananchi kuangalia wanaogombea kama wanaelekea kulinda haki za walio wengi au ni mateka wa matajiri. 
 
Alitaja tunu nyingine ni muungano kwa kusema anayeomba urais na kutaka kucheza na muungano lazima akataliwe.

Kuhusu uadilifu, alisema inapaswa aingie rais atakayekoleza vita ya ufisadi . “Kama kuna mtu anataka urais hata kutamka neno ufisadi anaogopa, huyu hatufai hata kidogo,” alisema Kitila.

Akizungumzia demokrasia, alisema nchi imepiga hatua katika demokrasia ambayo inahitaji rais atakayeipeleka mbele. Vile vile alisema katika kuchagua, ni lazima kuangalia mgombea ndani ya chama chake alipatikanaje.

“Kazi nyingine ya rais lazima awe mfano wa binadamu bora katika jamii. Hatumaanishi malaika, tunamaanisha kwamba popote atakapoenda, akisimama wajue huyu ni Mtanzania, awe sura ya utaifa,” alisema na kusisitiza sifa nyingine ya rais itokane na uadilifu wa chama chake.

Kitila alisisitiza, “Mtu asiye mlaghai lazima aliyotuambia jana, na leo yafanane. Akihubiri maji lakini yeye anakunywa wiski, yeye ni mlaghai. Akituambia ni nyeusi jana, leo nyekundu, kesho nyeupe, huyo ni mlaghai.” 
 
Alisisitiza kuwa ACT Wazalendo inazingatia misingi na sera huku akibeza vyama vingine kwamba vinauza mbwembwe na ulaghai.

Ukawa wasutwa 
Kwa upande wake, Meneja wa Kampeni, Habib Mchange, aliisuta Chadema na CUF kupitia viongozi wao akirejea mkutano wa Mwembe Yanga mwaka 2007, walipotaja orodha ya waliowatuhumu kuwa mafisadi papa. “Kipindi kile hawakuwa na Ukawa bali walikuwa na ushirikiano.

Walitaja watu wanaofilisi taifa hili ambao ni watu kumi na moja…kati ya watu hao waliotajwa kuwa ni mafisadi, namba tisa alikuwa ni Lowassa,” alisema Mchange. 
 
“Tulikubaliana 2007 kwamba tunapambana na CCM na wana mafisadi. Leo naomba mtafakari…ili tusiwe wajanja wajanja lazima tuseme ukweli.Unayosema jana ndo hayohayo uyaseme leo,” alisema.
 
 Akinyoshea CCM pia vidole, Mchange alilinganisha mgombea wa Ukawa sawa na chupa yenye sumu iliyobandikwa jina la maji. Alinadi chama chake akisisitiza wananchi wakiamini kwa kuwa kimekuja katikati ya sumu mbili za CCM na Ukawa.

Amshangaa Sumaye, Lowassa 
Mchange alisema anachoona ni kwamba, ufisadi uliokuwa CCM, umezaliana na kutanuka na hatimaye kuhamia Ukawa. “Jana (juzi) Sumaye ametulaghai… Anasema anashangaa kwa nini CCM inaendelea kuaminiwa,” alisema.

Alikumbusha kuhusu mjadala wa kununua ndege ya rais ambayo ilipigiwa kelele, kwamba wakati huo Sumaye ndiye alikuwa Waziri Mkuu. 
 
Pia kuhusu ahadi ya Lowassa ya kumwachia huru mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, Mchange alieleza kushangazwa naye kutokana na kile alichosema, wakati anafungwa, ndiye alikuwa Waziri Mkuu.

Mchange alikuwa mkali zaidi katika hotuba yake hasa alipokuwa anazungumzia ufisadi na wizi. “ Kumbe unaruhusiwa kuwaibia Watanzania ukiwa CCM ukirudi upinzani ni msafi. Mwizi ni mwizi tu.

Fisadi ni fisadi tu…Wanatudanganya kwamba kuna Ukawa…waongo. Ukawa wanatafuta rais tu. Ukawa huku chini kwa wapiga kura haupo,” alisema Mchange. 
 
Alihoji ni namna gani mgombea urais ataweza kunadi wagombea wa vyama vinavyounda Ukawa ambao wamegoma kuachiana majimbo hususani Jimbo la Tabora Mjini, Serengeti na Segerea.

“Sasa tuwaulize Ukawa Lowassa akipita Tabora mjini atamnadi nani?,” alisema akimaanisha mgombea wa CUF na Chadema wanaogombea jimbo hilo. 
 
Zitto Kabwe Alisema ACT Wazalendo wanarejesha miiko ya uongozi.

Alisisitiza kuhusu utaratibu wa chama chake wa kiongozi kutangaza mali na madeni yake. Zitto alisema kila chama kinachogombea, kinasema kitapambana na rushwa na ufisadi bila kueleza ni namna gani watapambana tofauti na ACT Wazalendo ambacho kimesema kitapambana kwa kurejesha miiko ya uongozi.

Alihoji ni namna gani mawaziri wakuu wastaafu wanatamba kuleta mabadiliko.
 
 Zitto alimsuta Sumaye akisema, wakati ATCL inauzwa aliyekuwa Waziri Mkuu ni Sumaye na wakati huo huo na mwaka 2007 ilipotaka kufufuliwa wakapewa Wachina ambao walisababisha hasara kwa taifa aliyekuwa Waziri Mkuu alikuwa Lowassa.

Zitto alikosoa pia kauli ya Magufuli juu ya ahadi yake ya kuanzisha mahakama ya kupambana na rushwa, akisema kwenye katiba mpya, kulikuwa na kipengele cha kuipa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mamlaka ya kukamata na kushitaki wala rushwa lakini CCM waliikataa.

Kuhusu ufisadi, Zitto alisema hakuna chama cha siasa chenye uwezo wa kupambana nao isipokuwa ACT Wazalendo. Akitumia kete ya jinsi kumnadi mgombea, Zitto alisema, ni wakati wa Watanzania kumpa mwanamke uongozi wa nchi ikizingatiwa miaka yote, imekuwa ikiongozwa na wanaume.

Sunday, August 30, 2015

HATIMAYE SHERIA YA MTANDAO KUANZA KUTUMIKA RASMI 01/09/2015.Zingatia haya mambo 10 muhimu ili sheria hii isikukamate.

Sheria ya mitandao inaanza kutumika rasmi tarehe 1 septemba 2015.
 
 1. Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao

2. Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao

3. Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k)

4. Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii

5. Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama ulivyopokea ) itakugharimu

6. Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu

7. Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu

8. Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu

9. Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini

10. Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia 'brand' ama jina la mtu itakugharimu

Hukumu
Ni kifungo cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha isiyopungua milioni 5 kulingana na kosa lililofanyika (au vyote!)

Saturday, August 29, 2015

Mwakyembe Amshambulia LOWASSA Kuhusu Sakata la Richmond...........Mwigulu Nchemba naye Adai Lowassa Ni Mpiga Dili Tangu Kijana


Aliyekuwa mwenyekiti wakamati teule ya bunge ya kuchunguza kashfa ya mkataba tata wa Richmond iliyomuondoa madarakani aliyekuwa waziri mkuu Mh Edward Lowassa, Mh Harrsion Mwakyembe amewahakikishia watanzania kuwa walijiridhisha pasipo shaka kuhusika kwa Edward Lowassa katika sakata la Richmond na kwamba hawakumsingizia kama anavyojitetea hivi sasa.
 
Mwakyembe aliyasema hayo mbele ya maelfu waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli katika viwanja vya Luandanzovwe jijini Mbeya, jana.

Akizungumzia madai ya kwa nini baadhi ya wahusika hawakupelekwa mahakamani kama kuna ushahidi, mhadhiri huyo wa sheria alisema kosa la jinai, halina ukomo na wakati wowote linaweza kufunguliwa mashitaka, huku akiapa kuwa anaweza kumfungulia mtu mashitaka hata kesho.

Alionya viongozi na makada wa Chadema na vyama vinavyowaunga mkono katika umoja wa Ukawa wanaozindua kampeni zao leo jijini Dar es Salaam, kwamba wasithubutu kujibu hoja zake.

Dk Mwakyembe alisema ikilazimika kusema ukweli, ataweka hadharani uchafu wote uliofanyika, ambao alisema bungeni kuwa asingeuanika na kuifanya Richmond hoja ya kila siku mpaka Watanzania waelewe kilichofanyika.

“Tunao ushahidi. Hawa walitakiwa kuwa jela badala ya kuimba nyimbo za ajabu,” alisema Dk Mwakyembe katika mkutano huo uliorushwa moja kwa moja nchi nzima na kuongeza kuwa Dk Magufuli akiingia madarakani, anakwenda kuanzisha Mahakama ya Ufisadi.

Alisema yeye na wenzake walipewa kazi ya Bunge kuchunguza ilikuwaje viongozi waandamizi wakaamua kuipa kampuni hewa zabuni ya mabilioni ya fedha, ambayo imesababisha mpaka leo kuna shida ya umeme nchini.

Dk Mwakyembe alikumbusha kuwa walikwenda mpaka Marekani kuchunguza uwepo wa kampuni hiyo iliyodaiwa kutoka katika nchi hiyo, na kukutana na kampuni ya kuchapisha kadi za harusi.

Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, baada ya kubaini ubadhirifu huo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alishinikizwa kujiuzulu na kumaliza suala hilo na hivyo hatua ya kiongozi huyo kutaka kwenda Ikulu, wazalendo hawawezi kuikubali.

“Hatutaruhusu watumie demokrasia kuingia Ikulu na hiyo ndiyo shida ya kuazima wagombea,” alisema Dk Mwakyembe akimaanisha kuwa chama cha Chadema, kimeazima mgombea bila kumfahamu.
 
 Dk Mwakyembe alisema suala hilo lilishafungwa bungeni, lakini anashangaa kusikia linarejeshwa kinyemela.

Mwigulu
Naye Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba, alisema mgombea wa Ukawa, Lowassa, tangu akiwa kijana alikuwa ‘mpiga-dili’.

Kwa mujibu wa Mwigulu, Rais Kikwete alipoingia madarakani, alidhani kuwa Lowassa alikuwa ameonewa, akamteua kuwa Waziri Mkuu, lakini kabla ya kumaliza miaka miwili, akaendeleza tabia yake ya ‘kupigadili’.

Mwigulu alionya kuwa, Watanzania wakimpeleka ‘mpiga-dili’ Ikulu, shida yake na wenzake si changamoto za watu wa Mbeya wapate maji, huduma bora za afya na nyingine bora za umma, bali kurejesha fedha walizotumia wakati wa kutafuta urais.

“Mkimpeleka mpiga dili Ikulu, ‘wapiga-dili’ wenzake hawatalipa kodi, mtalipa nyie wanyonge ili wale ‘wapigadili’ warejeshe fedha zao,” alisema na kufafanua sababu za vyama vya Chadema, CUF, NCCRMageuzi na NLD kuungana pamoja katika Ukawa. 
 
Kwa mujibu wa Mwigulu, kilichowaunganisha ni maslahi ya aina mbili; moja aliyetoa fedha kwa ajili ya kwenda Ikulu, ambaye anatafuta nafasi hiyo ili arejeshe madeni yake na wengine ni waliouza vyama ambao ‘wameshakunja’ chao.

“Nawaambia mwisho wa mbwembwe na maigizo, ni Oktoba 25 na baada ya hapo ni kazi tu,” alisema Mwigulu na kuhoji iweje Lowassa apande daladala leo, ambalo hakulipanda miaka 40 iliyopita?
 
 Mwigulu alisema Watanzania wana siku 60 za kujadili hatima ya taifa lao na katika hilo, hakuna namna zaidi ya kuelezana ukweli mtupu.

Friday, August 28, 2015

MAGUFULI NDANI YA WILAYA YA RUNGWE AWAHUTUBIA MAMIA YA WATU NA KUAHIDI MAMBO MENGI




 


Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kyela waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa John Mwakangale.
Umati wa wakazi wa Kyela wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM Mhe. Wiliam Lukuvi akisalimia wakazi wa Kyela.
 Mbunge wa Jimbo la Kyela Dk. Harison Mwakyembe akihutubia wakazi wa Kyela waliojitokeza kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli.
 Mbunge wa Jimbo la Kyela Dk. Harison Mwakyembe akihutubia wakazi wa Kyela waliojitokeza kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli.

 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tukuyu Sahul Amon akihutubia wakazi wa Rungwe waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa Kampeni ambao Dk. John Pombe Magufuli alihutubia.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Busokelo Kwere Fredy Mwakibete akiwaga sera zake kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambao Dk. John Pombe Magufuli alihutubia.




MMOJA WA VIONGOZI WA CHADEMA TAWI MAARUFU LA KIWIRA TUKUYU WILAYANI RUNGWE AKIONGOZA UJUMBE ULIOHAMA CHAMA NA KUHAMIA CCM AMBAPO KATIKA UJUMBE WAO WAMESEMA WALIFANYWA SANA KUWA DARAJA LA KUVUKIA LAKIN SASA WAMEHAMIA CHA CHA MAPINDUZI






MAGUFULI AKIONDOKA KATIKA VIWANJA VYA TANDALE TUKUYU MJINI HUKU AKIZONGWA NA WATU WENGI AMBAO HAWAKUPATA NAFASI YA KUINGIA UWANJANI NA WENGINE KUCHELEWA KUMSIKILIZA KWA SABABU YA WATU WALITEGEMEA MKUTANO KUFANYIKA JIONI

Wednesday, August 26, 2015

CHAMA Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)wilayani Rungwe Mbeya kimezindua kampeni zake leo

 Mgombea Ubunge jimbo la Rungwe Kwa Tiketi ya CHADEMA akiwasalimia wananchi Wa RUNGWE




                                                     
CHAMA Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)wilayani Rungwe Mbeya kimezindua kampeni zake leo huku kikimnadi John Mwambigijakuwa mgombea Ubunge jimbo la rungwe magharibi kupitia UKAWA ambaye alitaja vipaumbele kadhaa pindi atakapochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
 
Mwenyekiti wa Chadema jimbo hilo,Juma Kibo alisema chadema haikukosea kumteua Mwambigija kugombea nafasi  hiyo kwa kuwa amekidhi vigezo na anakubarika ndani na nje ya Chama na kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa mbunge wanauhakika ataondoa kero zilizoshidwa kutolewa na ccm wilayani hapo.

‘’Ushindi wa Ukawa katika uchaguzi wa mwaka huu ni asubuhi kwa kuwa wananchi wanaimani na wagombea watokanao na Ukawa na kuwataka wananchi wachague madiwani,wabunge na Rais ili Chama cha Mapinduzi kiweze kupumzika kwa amani’’alisema  Juma Mwambelo amaye ndiye Mwenyekiti wa chama Wilaya.

Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (SUGU)alisema iwapo wananchi watamchagua Mwambigija kuwa mbunge wa jimbo hilo,atashirikiana nae  ilikuhakikisha wanaziondoa kero zote kwa kuwa ccm imeshindwa kuwatumikia wananchi.

Alisema Serikali ya Chama cha mapinduzi imeuza viwanda vyote na kuifanya nchi hii kuwa masikini wa kutupwa na kuwa Ukawa ndiyo tumaini la kweli hasa kuwapata wagombea makini akiwemo wa urais Edwald Lowassa kiongozi makini anayeweza kulikomboa Taifa hili.

kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo John Mwambigija mbali na kuwapongeza wana Rungwe kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo aliouita wa kihistoria alisema hata waangusha wanarungwe na kuwa atahakikisha anakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha maendeleo yanapatikana.

Alisema ni haibu kwa wilaya yenye kila kitu lakini imekosa maendeleo kutokana na viongozi watokanao na ccm kutokuwa na hofu ya mungu katika utawala wao na kwamba akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anaondoa kero za afya,maji,kilimo na masoko,miundombinu ya barabara na kusimamia masrahi ya wafanyakazi.

Nae mgombea Ubunge viti maalum kupitia chama hicho,Jeska Mkumbwa alisema atazunguka kila mahala kuhakikisha wanatoa elimu kwa akina mama ambao wanatajwa kuwa ni mtaji wa ushindi wa ccm ili wasiwe madaraja kwa chama kisichokuwa na misingi ya utawala bora na kuwataka wabadirike.

Wananchi kwa upande wao,walisema wanaimani na wagombea waliosimamishwa na Ukawa wakidai kuwa wamekidhi vigezo vya kuwa viongozi na kusema kuwa watawapa kura za ndiyo kwa kuwa chama cha Mapinduzi kimepoteza muelekeo hasa walipomteua Saul Amon mwenye sifa chafu kuwa mgombea kupia chama hicho.







 

MWISHO.

Monday, August 24, 2015

KAMPENI ZA MAGUFULI ZAITIKISA MPANDA



 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mpanda wakati akiwasili kwenye viwanja vya Azimio tayari kwa mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo alihutubia wananchi hao waliojazana kwa wingi.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mpanda mkoani Katavi na kuwaambia wananchi hao kuwa hatokuwa na msamaha kwa watu wasiotimiza majukumu yao.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo pinda akimtambulisha Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe magufuli kwa wakazi wa Katumba mkoani Katavi.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi Mishamo mkoani Katavi .

 Wakazi wa Mishamo Katavi wakionyesha mabango ya kumchagua Magufuli kwenye mkutano wa kampeni.



Wananchi wa Mishamo wakimsikiliza Dk.John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM mkoani Katavi.


 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akihutubia wakazi wa Katumba kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais Dk. John Pombe Magufuli.


 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Katumba mkoani Katavi.
 Umati wa wakazi wa Katumba kwenye jimbo la Nsimbo wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Saturday, August 22, 2015

Wanachama zaidi ya 500 wa CHADEMA wahamia ACT...Kadi Zachomwa Moto Laivu

Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.



Wanachama hao wamefikia maamuzi ya kukihama chama hicho huku wakiwalalamikia viongozi wao wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata mgombea wao wa ubunge jimbo la Ludewa waliyemuhitaji Bwana Okol Haule na kumuweka mgombea wanayemuhitaji wao bwana Bathoromeo Mkinga.
Mamia ya wanachama hawa kutoka wilaya ya Ludewa, wamefanya maandamano ya amani kutoka mtaa wa Kilimahewa hadi katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini Ludewa wakiwa na mabango ya aina mbalimbali yakilaani viongozi wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata Okol Haule aliyeshinda katika kura za maoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.


Hata mara baada ya wanachama hawa kuwasili katika ofisi za CHADEMA wilaya, viongozi waliingia mitini na kufunga ofisi, lakini dhamira ya wafuasi hawa wa CHADEMA wakiwemo viongozi wa juu kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Ludewa, haikuishia hapo na wote wakiwa hawana imani tena na CHADEMA wakaelekea ofisi za ACT Wazalendo mtaa wa Sokoni na kujiunga nacho.
Huku wakidhamiria kuisambaratisha kabisa CHADEMA wilayani humo, wanachama hao wakiungana na mgombea wao wanayemuhitaji bwana Okol Haule wakachoma moto nguo aina ya kombati alizokua akizitumia mgombea huyo, bendera na kadi za CHADEMA ambapo bwana Haule anasema ameshindwa kuvumilia ubakaji wa demokrasia uliofanywa na viongozi wa CHADEMA.

Thursday, August 20, 2015

Rais Nkurunziza aapishwa kwa muhula wa 3



Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anaapishwa kwa muhula wa tatu uliozua utata.
Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge nchini Burundi anasema kuwa sherehe hiyo imefanyika kwa mshangao mkubwa kwa kuwa rais Nkurunziza alitarajiwa kuapishwa wiki ijayo.
Hatahivyo hakuna kiongozi wa taifa lolote aliyehudhuria sherehe za kuapishwa kwake huku Afrika kusini ikishirikishwa na waziri mmoja kulingana na shirika AFP.
Mataifa kadhaa yakiwemo yale ya China na Urusi yalituma mabalozi wao.
 

 
Mabalozi wa Marekani na muungano wa Ulaya walisusia lakini wakashirikishwa na maafisa wa nyadhfa za chini.
Umoja wa Afrika haukutuma waangalizi.
Takriban watu 10 wameuawa tangu Nkurunziza atangaze mnamo mwezi Aprili kwamba atawania muhula wa tatu wa urais.
Serikali inaushtumu upinzani ambao unasema kuwa muhula huo ni kinyume na sheria kwa kuzua ghasia.
 

Umoja wa Afrika,muungano wa Ulaya na wizara ya maswala ya kigeni ya Marekani wote wameonyesha wasiwasi wao kwamba uchaguzi huo wa mwezi Julai haukuwa huru na wa haki.