VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Wednesday, December 20, 2017

Wananchi Wampa Makavu Maulid Mtulia Baada ya Kutangaza Kugombea Ubunge Kupitia CCM Baada ya Kuikimbia CUF


SeeBait
Aliyekuwa Mbunge Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia ambaye amehamia CCM ametangaza nia ya kugombea tena ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho  tawala.

Desemba 2 Mtulia alijiuzulu nafasi ya ubunge,  huku akisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa mtu yeyote na amebaini Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani iliahidi kuyatekeleza.

Baada ya hatua hiyo, chama cha CUF upande wa Profesa  Ibrahim Lipumba  kilitangaza  kuwaomba radhi wapiga kura wa Kinondoni kwa Mtulia kujiuzulu uanachama kisha ubunge.

Lakini  jana Jumanne Desemba 19, 2017 kupitia andiko lake mtandaoni, Mtulia amesema atachukua fomu ya kuomba ridhaa  ya kuteuliwa ndani ya CCM ili agombee tena nafasi hiyo.

"Kwaza, nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni. Nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF. Nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu" aliandika Mtulia

Mtulia alitumia nafasi hiyo kutangaza nia yake kutaka kugombea;"Nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na Watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni" 

Kufuatia ujumbe huo ndipo hapo baadhi ya wananchi walianza kumpa maneno wakionyesha hisia zao juu ya jambo alilofanya na analotaka kulifanya. 
VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Friday, September 22, 2017

Mbowe Aipinga Serikali Sakata la Kumsafirisha Tundu Lissu


Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe, amesema Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hatosafirishwa kwenda popote mpaka pale madaktari watakaporuhusu.

Mhe. Mbowe ameeleza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari ikiwa imepita siku moja tokea serikali ya Tanzania itoe kauli yake kuwa ipo tayari kumtibia Lissu popote pale duniani kupitia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu.

"Tundu Lissu bado ni mgonjwa sana, hawezi kusafirishwa nje ama kutikiswa kwa njia yeyote katika kipindi hiki kwa hiyo mpango wowote wa kumuondoa hospitalini Nairobi kumpeleka nchi yeyote hautokuwepo kwa sasa mpaka hapo madaktari watakaporuhusu kulingana na hali yake", amesema Mbowe.

Pamoja na hayo, Mbowe ameendelea kwa kusema "Madaktari wametuhakikishia wana vifaa, dawa, utaalamu wa kukamilisha awamu ya pili ya matibabu ya Mhe. Lissu na yatafanyika hapo hapo katika hospitali ya Nairobi, Kama kutakuwa na ulazima katika hatua za baadae basi hizo zitafanyika kulingana na ushauri wa madaktari".

Aidha, Mbowe amesema wamelazimika kumuwekea ulinzi mkubwa Lissu katika hospitali aliyolazwa kutokana na kuhofia hali ya usalama iliyokuwa imetanda juu ya Mbunge huyo kutokana na shambulio alilofanyiwa na watu waliokosa utu.

"Nipende kusema tunawashukuru sana uongozi wa hospitali ya Nairobi, wenzetu walielewa hofu yetu na wametoa ulinzi wa ziada kwa ajili ya Mhe. Lissu masaa 24 ndani na nje. Kwa hiyo Lissu yupo chini ya uangalizi mkali sana na hili lilifanyika kutokana hofu iliyotanda na inayotanda kwa halali kabisa kwa sababu kuna watu walitaka kuondoa maisha ya Lissu lakini hawakuweza kufanikisha kazi yao, na hao watu hawana utu kabisa kwani tukiwapa nafasi hawatasita kukamilisha kazi yao", amesisitiza Mbowe.

Kwa upande mwingine, Mbowe amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kuhusu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwani madaktari wameshawahakikishia kuwa Lissu atapona na kurudi kuendelea katika harakati zake alizokuwa anazifanya kama awali.

VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Sunday, January 29, 2017

BREAKING: Picha 13 za uokoaji kwa waliofukiwa mgodini Geita





Taarifa zilizoripotiwa kutokea mgodini Geita kuhusu Wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi cha udongo kwa zaidi ya siku tatu zinasema kwamba wachimbaji hao wote 15 wameokolewa wakiwa hai na utaratibu mwingine wa huduma ya kwanza unaendelea, picha za tukio ndio hizi














VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......