VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Thursday, July 30, 2015

PICHA: Lowassa Achukua Fomu ya Urais CHADEMA


Edward Lowassa akionesha fomu ya kuwania urais aliyokabidhiwa leo Makao makuu ya Chadema,D ar.
CLJ5hSGWoAACCU3
Umati wa watu waliojitokeza kumpokea Lowassa wakati akichukua fomu ya urais kupitia Chadema.
CLJ8fhkW8AA6IKB
…Akisaini katika kitabu cha wageni.
CLJ9y4iWEAAZWy7
Mnadhimu Mkuu kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu akitoa yake machache.CLJ52JsWwAA--Yc
Lowassa akiwasiri kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Dar leo.
CLKRw2sWcAAzeL9
Baada ya kuchukua fomu.
mbowe na lowassa
Mwenyekiti wa Chadema (kushoto) Mhe. Freeman Mbowe Mhe. Edward Lowassa (katikati) wakati wa zoezi la kuchukua fomu lililofanyika leo Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar .
LOWASA (1)
LOWASA (2)
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika meza kuu ya Chadema.
 **
WAZIRI MKUU wa zamani, Mhe. Edward Lowassa hivi punde amechukua fomu ya kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Lowassa amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 
Lowassa alijiunga rasmi na Chadema juzi akitokea CCM baada ya kuondolewa kwenye mchakato wa kuwa mgombea urais wa chama hicho akidai kuwa jina lake liliondolewa kwa mizengwe.

Wednesday, July 29, 2015

CCM Wamjibu LOWASSA........Wasema Kuhama kwake Hakuna madhara na kwamba Watapata ushindi wa kishindo

 Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Dar, Juma Simba Gaddafi  jana  aliongoza  mkutano  wa  CCM  na  waandishi  wa  habari  uliofanyika  Peacock Hotel Dar, na  haya  ndo  mambo  aliyoyasema;
 
"CCM inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama chenye busara tumeona tuwashukuru

"Tume ya Uchaguzi tunawaomba wawe makini kuongeza Mashine na Watendaji ili watu wapate nafasi kujiandikisha na watumie fursa yao Kupiga Kura… CCM tuna uhakika tutashinda.

"Kingine tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura… 
 
"Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi nzuri… 

 "Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya mengi yanayokubalika."

Akiongelea  sakata  la  Lowassa  kuhamia  CHADEMA, Gaddaf  alisema;
 
"Yeye aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM, kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka.

"Mtu akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe… 
 
"Kama Lowassa angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara."

Akiongelea  kuhusu Uteuzi wa Mgombea wa Urais CCM Dodoma, Gaddaf  alisema;

"Mkutano Dodoma tuliumaliza, lakini tumekwenda kwenye NEC Wajumbe wako 360, walipiga kura majina matano na Wagombea wote wa Halmashauri Kuu akiwepo Rais, Waziri Mkuu na Lowassa walikuwepo… kama asingekuwepo hayo yangesemwa, lakini alishiriki na alipiga Kura"

Tuesday, July 28, 2015

Mbunge Mwingine wa CHADEMA Arudisha Kadi na kujiunga na CCM



MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere ameng'atuka rasmi jana katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam, Leticia alisema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.

Alisema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.
 
“Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa CHADEMA na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi nyumbani kutumikia” amesema Leticia.

Leticia alisema kwenda CHADEMA alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.

Alisema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi.

Monday, July 27, 2015

Lowassa Akaribishwa Rasmi UKAWA......Hapa kuna picha na kilichojiri Leo Katika mkutano wa UKAWA na Waandishi wa habari


“Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje”. Hii ni moja ya kauli  ambayo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliziongea Arusha May 30 2015 alipotangaza nia ya Kugombea Urais kupitia CCM.
 
CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40 ambao walitangaza nia na kuchukua fomu za Kugombea Urais 2015 lakini baadae Chama hicho kikampitisha Dk. John Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo, baada ya hapo kukawa na  taarifa nyingi sana kuhusu ishu ya Edward Lowassa na UKAWA.
 
Viongozi wa Umoja wa UKAWA wamekutana Dar  leo  na mmoja wa Viongozi hao, James Mbatia amesema wamekubaliana kumkaribisha Mbunge Edward Lowassa ndani ya UKAWA na wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana nae.

Mbatia  ameongeza kuwa Lowassa ni mchapa kazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa kiutendaji katika majukumu anayokabidhiwa.
 
Alipoulizwa kuwa Lowassa atakuwa mgombea Urais Mbatia amesema kila chama kina utaratibu wake  hivyo mchakato ukishakamilika  atatangazwa mgombea urais wa UKAWA mmoja  mwanzoni mwa mwezi agosti.




Wednesday, July 22, 2015

Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo


Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema watu  zaidi  ya 10  wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo , huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.
 
Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma.Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu.

Monday, July 20, 2015

Majambazi Walioua Polisi na Raia Kituo cha Polisi Stakishari Wakamatwa



MAJAMBAZI waliovamia Kituo cha Stakishari jijini Dar es Salaam watatu wauwawa na wawili watiwa mbaroni wakati wakitupiana risasi katika eneo la Tuangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 
Tukio hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, na majambazi wa tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao  inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.
 
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika eneo la Tuangoma ndipo majambazi wakapita na pikipiki mbili walipowasimamisha askari majambazi hao walikaidi amri nakisha kuanza kurusha risasi na polisi wakajibu na majambazi watatu kuuwawa.
 
Majambazi waliouawa ni Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala,Yassin alitambulika kwa jina moja mkazi wa Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina moja mkazi wa Mandimkongo ,Mkuranga.
 
Kamanda Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15),Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, Omary Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.
 
Kova amesema baada ya kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki  15 walizopora katika kituo cha Stakishari ambazo walikuwa wamehifadhi chini ya ardhi na kuweka kinyesi juu.
 
Amesema katika Shimo walilohifadhi walikuta bunduki aina ya  Norinko ambayo wanatafuta ilipoibiwa pamoja na kukuta fedha taslimu Sh.Milioni 170 za kitanzania.
 
Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kwa kuwa halipi.
 
Amesema fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibwa wapi,na pikipiki mbili aina ya boxer nazo wanazishiklia na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanataarifa nao.
 
“Hatutafumbia macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au askari” amesema Kamishina Kova.
 
Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea  julai 12 majira ya saa nne.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari, Tazara,leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Stakishari ,Tazara,jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi katika kituo stakishari,Tazara leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na majambazi waliovyamia kituoa stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar es Salaam.
 Fedha za watuhumiwa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakiki zikiwa katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi habari na wananchi leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha picha za majambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi katika hafla ya kutuoa taarifa za kukamatwa kwa askari wa waliovamia kituo cha stakishari leo jijini Dar es salaam 
Pikipiki zilizokuwa zikitumiwa na majambazi waliovyamia Kituo cha Stakishari zikiwa mbele ya Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao leo jijini Dar es Salaam.

Lupumba Aiyumbisha UKAWA


Wakati bado haijafahamika lini mgombea urais kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) atatangazwa rasmi, imefahamika kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba, amekuwa ndiyo kikwazo cha kutopatikana kwa mgombea huyo.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu kwa siku nne sasa umebaini kuwa hatua ya Profesa Lipumba kukwepa vikao vya Ukawa, ni mkakati mahsusi unaolenga kukwamisha mchakato wa kupatikana mgombea urais wa umoja huo.

Ukawa unaundwa na Cuf, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi na NLD.

Taarifa kutoka ndani ya vikao vya Ukawa vimeeleza kuwa kikao cha kwanza cha umoja huo, Profesa Lipumba aliulizwa kwanini anataka kugombea urais na kujibu kuwa anaamini kuwa yeye ndiye bora kuliko wengine.

Hata hivyo, alipoulizwa kama amejiandaa vipi kirasilimali iwapo atateuliwa kuwania nafasi hiyo kupitia Ukawa, hakuwa na majibu ya kujitosheleza na badala yake ilibainika kuwa Cuf imejiandaa zaidi Zanzibar kuliko Tanzania Bara.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Profesa Lipumba amekuwa aking’ang’ania agombee urais na hata mkutano wa mwisho wa Ukawa ambao hakuhudhuria, inadaiwa kwamba ni mkakati wa kushinikiza ateuliwe yeye kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.

Katika vikao vya Ukawa, hoja kubwa imekuwa ni suala la mgombea urais, nafasi ambayo inawaniwa na Profesa Lipumba ambaye tayari ameshachukua fomu kupitia chama chake cha Cuf pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, anayeungwa mkono na vyama vyote vinne.

Profesa Lipumba ameshagombea urais mara nne bila  mafanikio, wakati Dk. Slaa aligombea mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili, akiwa ameitikisa CCM iliyopoteza asilimia takriban 20 ya kura za mwaka 2005.

Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia, akizungumza na waandishi wa habari Julai 14, mwaka huu, alisema umoja huo utamtangaza mgombea wao wa urais baada ya siku saba ambazo zinaisha wiki hii.

Alisema wamekubaliana kutangaza mgombea baada ya siku saba ili kutoa nafasi kwa viongozi walioshiriki majadaliano hayo kutoa taarifa kwa wanachama wa vyama vyao juu ya mambo waliokubaliana.
  
Aidha, Mbatia alikanusha uvumi kuwa kada wa CCM na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ana mpango wa kujiunga na umoja huo ili apewe nafasi ya kugombea urais baada ya kukosa nafasi hiyo kupitia chama chake.

Mbatia pia alikanusha uvumi ulioenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna mvutano mkubwa ndani ya Ukawa katika suala la mgombea urais ambao umesababisha Cuf kutaka kujitoa.

“Hakuna ukweli katika hilo na hata leo (jana), nimeongea na Profesa Lipumba kumtaarifu hatua tulioyofikia, hivyo hakuna mpasuko wowote,” alisema Mbatia.

Kabla ya taarifa hiyo ya Mbatia,Ijumaa iliyopita Ukawa walitoa taarifa ya kwamba wangemtangaza mgombea wake ndani ya saa 24, ahadi ambayo haikutimizwa.

Friday, July 17, 2015

KIMENUKA : Mh Tunsume Shingwa achukua fomu ya kutangaza nia kata ya Luswisi, wilayani Ileje Mbeya

Hatimaye baada ya kupatikana Kwa mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mh. John Pombe Magufuli 
kazi imehamia kwa Wabunge na Madiwani, Mnamo Jana 16/07/2015 Siku ya Alhamisi Saa saba  Mchana Mh: Tunsume Shingwa Wa Luswisi ileje Ameamua kujitokeza kuchukua Fomu ya kuwania Udiwani Kata ya Luswisi.

Tuesday, July 14, 2015

Tukio la Kituo cha Polisi Kutekwa: Viongozi Wa Dini Wacharuka.......Wamtaka Rais Kikwete Afanye Mabadiliko ya Jeshi la Polisi


VIONGOZI mbalimbali wa dini nchini wameandaa maandamano  kwa lengo la kumuona Rais jakaya kikwete ili kumuomba alifanyie mabadiliko makubwa Jeshi Polisi.

Mabadiliko hayo ni pamoja  na kubadili mawaziri  wote wa mambo ya ndani,  mkuu wa jeshi hilo (IGP)  na  MA-CP wawili ambao wametajwa  kuendesha jeshi hilo  kimtandao  kinyume  na taratibu za kijeshi.

Maandamano hayo yamefikiwa na Maaskofu na Mashekhe 160 wa mjini Dodoma jana chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya  Maadili, amani na haki za binadamu ya Madhehebu ya Dini Nchini Askofu William Mwamalanga.

Mwamalanga alisema  viongozi hao wamepokea taarifa ya kuuwa  kwa  askari polisi  wanne wa kituo cha stakishari cha jijini Dar es Salaam  kwa masitikito.

“Tumepokea taarifa ya vifo vya askari hawa kwa masikitiko, hali hii haikubaliki kila mara vituo vimekuwa vikivamiwa na hadi sasa takriban Askari 47 wameuwawa,” alisema Mwamalanga.

Huku akibubujikwa na machozi ya Uchungu Askofu Mwamalanga amehoji ukimya wa  Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe na IGP Erinest Mangu kwa vifo vyote ambavyo vimekuwa vikitokea tangu mwaka huu uanze.

“Uvamizi huu na mauaji ya askari wa chini unatisha   na hatuoni hatua yoyote ya maana  iweje wahalifu wawe na nguvu kuliko jeshi hasa kipindi hiki ambacho dunia inakabiliana  na makundi ya wahalifu hatari wakiwemo al shabab,” alihoji.

Kufuatia hali hiyo, ASkofu  Mwamalanga  amemuomba  Rais kikwete  kuwaongeza askari  wangazi ya  chini  mishahara   kwa kiwango cha Millioni moja ili  walingane na wenzao wa  nchi za afrika mashariki na kusini.

Alisema hatua hiyo itawawezesha askari hao kukabiliana na changamoto za maisha kama  ilivyofanya kwa wafanyakazi Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo ilisema hiyo itawaondolea tamaa za Rushwa.

“Kwa Polisi ni zaidi kwani kitendo cha kuuwawa kama tembo porini bila mshahara mzuri kunawakatisha tamaa na ari ya kufanya kazi,” alisema.

Askofu  Mwamalanga  ambaye ni Mwanaharakati  Mtafiti wa haki  za jamii  alisema idadi kubwa ya Maaskofu na Maashekhe nchini wamelaani Mauaji  hayo yanayoendelea dhidi ya polisi.

“Tayari zaidi ya askari 47 wameuwawa na wengine wamebaki vilema, silaha  lukuki zimechukuliwa vituoni na kutokomea kusikojulikana, hili lina dhihirisha kuwa Taifa letu lipo pabaya. Ndiyo maana tunaona ipo haja tena muhimu kwa rais kwachukilia hatua za haraka  wanaosababisha uzembe huo ikiwa ni pamoja na kulifanyia ukarabati jeshi hili,” alisema.

Aliwakumbusha watanzania kuliona jeshi hilo kuwa ni chombo chao cha kuwalinda  wao wawe salama dhidi magenge ya uhalifu  duniani hivyo wana wajibu kama  raia wema  kuhakikisha wanawalinda askari  hao kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa muhimu ili kuwakamata  wauaji wote pamoja  na silaha zote zilizoporwa.

Aidha  viongozi hao  walihoji kuondolewa kwa vizuizi [ berial] barabarani kulikuwa na maslahi gani kwa usalama wa nchi kwani hivi sasa  wahalifu  wametumia nafasi kutoroka kirahisi pale wanakuwa wamefanya uhalifu.

“Tunataka vizuizi hivyo virudishwe mara moja kwa barabara zote nchini,” alisema.

Kwa upande wake shekhe  Athumani Mukambaku   ambaye ni  Mwenyekiti mwenza wa Kamati  hiyo  na mjumbe wa BAKWATA halmashauri ya mkoa wa dar es Salaam alishauri serikali itunge sera mahususi ya  raia  wote kuwalinda  polisi  baadala  ya dhana iliyojengeka kuwa ni polisi pekee ndiyo wenye wajibu wa kulinda  raia, jambo linalojenga chuki pale ambapo  polisi wanaposhindwa  kusimamia haki za raia sawasawa.

“Katika kipindi hiki cha kulelekea uchaguzi mkuu jeshi linapaswa kuimarisha vituo vyake vyote ikiwa ni pamoja na kufunga kamera maalumu za cctv ili kuweka rekodi ya watu wote wanaotembelea vituo hivyo pamoja kuvunja kanda maalumu za kipolisi ambazo hazionesha juhudi ya kupambana na uhalifu na baadala yake zimeongeza gharama  kwa jeshi  hilo,” alisema Shekhe Mukambaku.

Alisema rais anapaswa ateue makamanda wabunifu wanaokwenda na wakati na kwamba  kila mkoa uwe maalumu kwa kuimarisha vitendea kazi vya askari ikiwa ni pamoja kuwapatia  motisha wale walio ngazi ya chini ambao hukesha  vituo kuimarisha ulinzi.

Tuesday, July 7, 2015

Watu 25 wauawa Zaria Nigeria


Wengi waliokuweko ni walimu na wafanyikazi wa umma.
Maafisa wa serikali Kaskazini mwa Nigeria wamesema kuwa watu 25 wameuawa katika shambulio la bomu la kujitolea mhanga katika mji wa Zaria.
Ripoti zinasema kuwa watu wengine 32 wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika jengo moja la serikali ambako wafanyakazi wa serikali walikuwa wamekusanyika kusajiliwa.
 
Watu 220 wameuawa katika mashambulizi kadha yanayolaumiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram
Wengi waliokuweko ni walimu na wafanyikazi wa umma.
Katika kipindi cha majuma 2 yaliopita takriban watu 220 wameuawa katika mashambulizi kadha yanayolaumiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Gavan wa jimbo la Kaduna amewaonya wenyeji kuwa waangalifu sana na kuepuka maeneo yaliyojaa watu kwani hayo ndio yanayolengwa na washambuliaji wa kujitolea mhanga.
 

Gavana Nasir El-Rufa'I amewasihi wenyeji waepuke misikiti makanisa masoko na vituo vya mabasi hadi pale hali itakapotulia.
Gavana Nasir El-Rufa'I amewasihi wenyeji waepuke misikiti makanisa masoko na vituo vya mabasi hadi pale hali itakapotulia.
Inspekta wa polisi wa Nigeria ameomba wanigeria kuwa makini na waangalifu akisema kuwa ''kwa sasa inaonekana mabomu yameundwa mengi na kwa hakika likishaundwa bomu ni vigumu sana kuzuia mashambulizi ya kujilipua kwenye umati wa watu ilikuzidisha maafa''.
Tayari hofu imetanda katika mji wa Abuja ambapo Polisi wamepiga marufuku uuzaji na uchuuzi katika barabara za katikati ya mji.

LIPUMBA: Tutaitisha Maandamano Mikoa Yote Yenye GESI


Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kitaitisha maandamano kwenye mikoa yenye gesi ili kulishinikiza Bunge kupinga muswada wa mafuta na gesi uliopitishwa juzi.
 
Akihutubia wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na viunga vyake, Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema haoni mantiki na hakuna sababu ya kufanya haraka kupitisha muswada huo.
 
“Suala hili linahitaji mjadala wa kina utaohusisha wadau mbali mbali, wataalamu na wananchi kwa ujumla wake,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza:
 
“CUF inaunga mkono jitihada za wabunge wa kambi ya upinzani kwa hatua zao kupinga muswada huo, ambao haukujali na wala haukuzingatia maslahi ya Taifa.”
 
Alisema CUF inatoa angalizo kwa Rais Jakaya Kikwete kwamba kwa hali inavyoenda huenda akaenda kufunga Bunge litalokuwa na Wabunge wa CCM pekee.
 
“Hiyo inatokana na ukweli kwamba Spika wa Bunge amepoteza muelekeo na ameshindwa kabisa kuliongoza Bunge kwa mujibu wa kanuni walizojiwekea katika kutimiza wajibu,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza:
 
“Kwa hiyo  basi, Rais Kikwete atakuwa amefuata nyayo za Rais wa Zanzibar.”
 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein Juni 26, mwaka huu alilivunja Baraza la Wawakilishi bila Wawakilishi wa CUF kuwapo barazani.
 
Wajumbe hao walisusia Baraza hilo kutokana na kutoridhishwa na uandikishaji wa wapigakura katima daftari la kudumu la wapigakura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki unaojulikana kama Biometric Voters Registrarion (BVR), wakisema kuwa uandikishaji huo ulitawaliwa na ubabe.
 
Profesa Lipumba alionya kuwa kama Bunge litaendelea na mpango wake huo, basi CUF  itaitisha maandamano ili kupinga muswada huo.
 
Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema kuwa Mkoa wa Kigoma unaweza kuendelea kiuchumi ikiwa utatumia vizuri rasilimali zilizoko akitolea mfano Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwamba ikitumika vizuri inaweza kuingiza mapato mengi.
 
Alisema kwamba jiografia ya Mkoa wa Kigoma inauruhusu kupata fursa nyingi za kuendelea kiuchumi kwa kuwa wananchi wake wanaweza kufanya biashara na nchi zinazouzunguka za Burundi Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Monday, July 6, 2015

ZITTO KABWE AWATAJA VIGOGO 99 WALIOFICHA MABILIONI USWISI

Zitto Kabwe akizungumza na wananchi kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam Julai 4, 2015.


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, (pichani) ametangaza majina 99 ya Watanzania wanaodaiwa kuficha mabilioni ya Shilingi katika benki moja nchini Uswis.
Majina hayo ameyatangaza katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam jana, ambapo amesema majina hayo ameyapata hivi karibuni katika taarifa ya benki moja inayofahamika kwa jina la HBC yenye makazi yake nchini humo.

Zitto ambaye hata hivyo, hakuyataja majina hayo kwa kile alichodai kuwa anabanwa kisheria, ameyakabidhi kwa vyombo vya habari ili kuhakikisha kila Mtanzania anafahamishwa.

Kwenye mkutano huo ambao ulihudhuriwa na maelfu ya watu, alipata nafasi ya kukitambulisha chama hicho kwa wakazi wa jiji hilo.

Alisema katika majina hayo, kuna wale waliohusika katika kashfa ya rada, hivyo ni dhahiri pesa nyingi zilizohifadhiwa zinatokana na vitendo vya ufisadi.

“Katika utaratibu wa kuweka fedha lazima watu hawa waombe kibali Benki kuu, lakini kutokana na serikali kuwa kimya licha ya kelele zetu, ni bora turudi kwenu,” alisema.

Alisema Mwembeyanga ni sehemu ya kihistoria kwani mwaka 2007 ndipo kulitajwa orodha ya mafisadi na jana ameamua kurudia historia hiyo.

Orodha hiyo yenye kurasa nne ilionyesha namba za akaunti ya watu hao, majina na tarehe ya kuzaliwa, ambapo mengi ni ya wafanyabiashara wakubwa wenye asili ya Asia na Watanzania.

Alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kuwa serikali imekuwa kimya licha ya majina kama hayo kupatiwa baada ya jaji mmoja wa Ufaransa kugundua kwamba kuna majina ya watu wenye akaunti zao kwenye benki ya Uswis.

Alisema hiyo ni benki moja, lakini kuna benki nyingi za nje ambazo Watanzania wameficha fedha.

“Tunachotaka serikali ichunguze kipi ni halali na haramu kwa kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara walipeleka fedha huko kihalali," alisema.

Zitto alisema tangu wapeleke vithibitisho hivyo, sasa ni miaka miwili na miezi sita imepita lakini serikali haijafanya chochote, kutoa majibu wala kupeleka bungeni suala hilo ili Watanzania waelewe.

Alitoa mfano katika vituo vya jeshi ambavyo Watanzania wameweka Paundi milioni 40,000 sawa na Sh. Trilioni 1.3 na Uswis ni dola milioni 305.
Alisema chama chake kimekuja kama chama mbadala kuleta mageuzi na misingi yake inafuata ile ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyoacha ya kuwa na maadili ya viongozi.

Alishangaa kitendo cha baadhi ya vyama kumuita msaliti, na kwamba katika shughuli za kisiasa hakuna usaliti kwa sababu wanasiasa wanapogombana baadaye huwa wamoja.

Alitoa mfano baadhi ya wabunge Dodoma waliitwa mashoga lakini sasa hivi ni wamoja.

Pia alitoa mfano wa James Mbatia, aliitwa mbunge wa viti maalum lakini sasa hivi wameungana na kuendeleza siasa. Alisisitiza kuwa katika chama chao wameweka sheria kila mtu anapojiunga lazima atangaze mali zake.

Thursday, July 2, 2015

WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA


Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Leo amehukumiwa tena kunyongwa mpaka kufa katika mauaji ya mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo hii imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).
Waliohukumiwa kunyongwa mpaka kufa ni Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga na Gerard Korosso Kalonge (wakazi wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje), na Leonard Msalage Mwakisole na Hakimu Mselem Mwakalinga (wakazi wa Kiwira wilayani Rungwe).
Mshtakiwa wa nne, Mawazo Philemon Figomole, ameachiliwa huru na mahakama hiyo baada ya ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasi na shaka kwamba alihusika katika mauaji hayo.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo ya mauaji yenye kumbukumbu Namb. KIW/IR/49/2008 na PI 5/2013, Jaji wa Mahakama Kuu Dk. Revila, amesema mahakama imejiridhisha pasi na shaka na ushahidi wa upande wa mashtaka kwamba washtakiwa hao wanne walitenda kosa hilo na hivyo wanastahili adhabu hiyo.
Hii ni kesi ya saba ya mauaji ya albino kutolewa hukumu ambapo mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 15 wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Ililezwa mahakamani hapo kwamba, mnamo Februari 5, 2008 majira ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni huko katika Kijiji cha Ilolo, Kata ya Kiwira, tarafa ya Ukukwe, wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, washtakiwa hao walimteka nyara kijana Henry Mwakajila, ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Ukukwe na kisha kumuua.
Wakati wa mwenendo wa kesi, ilielezwa na mashahidi wa upande wa mashtaka kwamba mshtakiwa wa kwanza Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga ambaye ni mganga wa jadi, mkazi wa Kijiji cha Mbembati, Wilaya ya Ileje, alikutwa na utumbo unaodhaniwa kuwa wa binadamu na ulipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ukathibitika kwamba ni utumbo wa marehemu Henry.(VICTOR)
Mshtakiwa wa pili, Gerard Korosso Kalonge wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje alikutwa na vidole vinne na mifupa kumi (10) vyote vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu na baada ya uchunguzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali ilibainika kwamba ni viungo vya marehemu Henry Mwakajila.
Ilielezwa pia kwamba, washtakiwa Leonard Msalage Mwakisole, Mawazo Philemon Figomole na Hakimu Mselem Mwakalinga ndio waliodaiwa kumteka nyara mtoto huyo na kumuua, kisha kupeleka viungo kwa mganga wa kienyeji Asangalwisye Kayuni.
Mshtakiwa wa tano, Hakimu Mselem Mwakalinga, tayari alikwishahukumiwa kunyongwa katika kesi nyingine ya mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake. Hukumu ya kesi hiyo namba 131/2012 ilitolewa Novemba 13, 2013 ambapo inaelezwa kwamba watuhumiwa walitenda kosa hilo Mei 19, 2011 katika kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Ingawa watuhumiwa walikuwa wanne, lakini Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya chini ya Jaji Samwel Karua iliwahukumu kunyongwa mpaka kufa mshtakiwa wa kwanza Hakimu Mwakalinga na mshtakiwa wa pili Daudi Mwasipasa kwa maelezo kwamba walihusika moja kwa moja na mauaji hayo ya kukusudia.
Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili yeye alitiwa hatiani kutokana na kosa la kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka kufanya mauaji wakati mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela alitiwa hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika katika mauaji hayo ingawa hakusika na kitendo hicho moja kwa moja, hivyo wote wawili walihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.
Hata hivyo, Myovela tayari alikwishahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria.
Inadaiwa kwamba, chanzo cha mauaji hayo ya John Mwankenja, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe, kilitokana na kiongozi huyo kufahamu kwamba hao ndio waliomuua mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila, hivyo aliuawa ili kupoteza ushahidi