VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Saturday, June 11, 2016

Mwanza: Kijana Awafungia ndugu zake Ndani na Kuchoma Moto Nyumba




Nyumba moja iliyopo mtaa wa Kiseke wilayani Ilemela mkoani Mwanza imeteketea kwa moto leo asubuhi na kuunguza vitu vingi huku wakazi wa nyumba hiyo wakinusurika. 

Taarifa zinaarifu kuwa,  nyumba hiyo imewaka moto baada ya mmoja wa watoto wa familia hiyo kuamka asubuhi na kumwaga mafuta ya taa katika moja ya chumba cha nyumba hiyo na kisha kuwasha moto.

Imeelezwa kuwa,  kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili amekuwa akiwatishia kwa muda mrefu kuwachoma moto lakini wamekuwa wakimpuuza kutokana na matatizo yake ya akili.

Baada ya kumwaga mafuta  na kuwasha moto,  kijana huyo alitoweka na kuwafungia ndugu wengine ndani ambapo majirani walifanikiwa kuwahi kuwaokoa.VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......

Friday, June 10, 2016

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi Ataka Mabasi ya Mwendokasi Kwa Ajili ya wanafunzi Udart

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ameishauri Kampuni inayoendesha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart) kuongeza mabasi ya wanafunzi na mengine ya wazi juu ya watalii wanaoitembelea nchini ili waweze kuangalia mandhari ya jijini Dar es Salaam. 
Rais Mwinyi alitoa ushauri huo jana alipotembelea mradi huo akiwa na mkewe, Sitti Mwinyi na kupokewa na Kaimu Mtendaji mkuu wake, Ronald Lwakatale, Mtendaji wa kampuni inayoendesha mradi huo, David Mgwassa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi. 
Mwinyi alikata tiketi katika Kituo cha Morocco na kupanda gari kwenda Kariakoo, Gerezani kisha Kivukoni. 
Alipofika katika kituo hicho alikutana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtendani na kuzungumza nao kwa kifupi kisha kuwaeleza ushauri huo alioutoa kwa Udart. 
“Nimekuja kupata maarifa na kuona mabasi yetu mapya yanavyofanya kazi kuhudumia wana Dar es Salaam. 
"Wakati nipo kwenye basi nimeteta na viongozi nikiwashauri kama kuna uwezekanao wa kuwa na basi moja au mawili ya wazi ambayo unaweza kupanda juu ili kuona mazingira ya jiji vizuri,” alisema Mwinyi, 
Alisema magari hayo ya wazi yatawasaidia watalii kulitazama jiji vizuri, lakini pia wanafunzi kujionea mandhari yake na kujifunza.
Mtendaji wa Udart, David Mgwassa alisema elimu imeanza kuwaingia wananchi kwani usumbufu na ajali hakuna na kwamba wiki ijayo matumizi ya kadi yataanza baada ya hatua za awali kukamilika na kubakia vitu vichache.
VITUS MTAFYA ..... ILEJE NI NYUMBANI ......