Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anaapishwa kwa muhula wa tatu uliozua utata.
Mwandishi
wa BBC Prime Ndikumagenge nchini Burundi anasema kuwa sherehe hiyo
imefanyika kwa mshangao mkubwa kwa kuwa rais Nkurunziza alitarajiwa
kuapishwa wiki ijayo.Hatahivyo hakuna kiongozi wa taifa lolote aliyehudhuria sherehe za kuapishwa kwake huku Afrika kusini ikishirikishwa na waziri mmoja kulingana na shirika AFP.
Mataifa kadhaa yakiwemo yale ya China na Urusi yalituma mabalozi wao.
Umoja wa Afrika haukutuma waangalizi.
Takriban watu 10 wameuawa tangu Nkurunziza atangaze mnamo mwezi Aprili kwamba atawania muhula wa tatu wa urais.
Serikali inaushtumu upinzani ambao unasema kuwa muhula huo ni kinyume na sheria kwa kuzua ghasia.
No comments:
Post a Comment