VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Saturday, May 23, 2015

MATUKIO YA MKUTANO WA CHAMA CHA CHADEMA WILAYANI KYELA UKIONGOZWA NA FREMAN MBOWE



Mbunge wa Jimbo la Mbeya  Joseph mbilinyi akitema cheche kwenye viwanja vya siasa Wilayani  Kyela Jana
Sehemu ya wananchi wilayani Kyela Mbeya wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe kwenye viwanja vya mchaga jana.




Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe akikagua gwaride la Red Briged linalohusika na ulinzi wilayani Kyela kabla ya kuanza kutema cheche wilayani Kyela.
Mbowe akitema cheche kwenye uwanja wa siasa wilayani Kyela.Picha zote na Ibrahim Yassin.

IMEELEZWA kuwa misingi mibovu ya kutozingatia utawala bora kwa wananchi unaofanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM)ndiyo sababu ya wananchi kushindwa kutumia lasilimali za nchi na kupelekea kuishi maisha duni huku baadhi ya viongozi wa serikali wakiendekeza uwizi bila kuchukuliwa hatua.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe wakati akizungumza na wananchi wa Kyela Mbeya kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Siasa uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka kata mbalimbali.
Alisema chama cha Mapinduzi wakati wa utawara wa Ally Hassan Mwinyi waliua azimia la Arusha lililoanzishwa na Hayati Mwl,Julius Nyerere na kuruhusu mambo yasiyo na msingi,na kuwa katika utawara wa Benjamini Mkapa Chama hicho kiliuza viwanda vyote vilivyokuwa na tija kwa wananchi.
Mbowe alisema viwanda ambavyo walishindwa kuviuza walileta wawekezaji kutoka nje kuwapa umiliki lasilimali za nchi na kuwanyima wazawa na kuwa kibaya zaidi wameuziana nyumba za serikali kwa bei ya mchicha bila kujali athari zinazoweza kujitokeza kama ilivyo hivi sasa ambapo chama hicho kimepoteza sifa.
Aliongeza kuwa kutokana na ali hiyo ndiyo maana Chadema ikaasisiwa kwa lengo la kuwakomboa wananchi ili waweze kupata nafuu ya maisha na kuzitumia lasilimali zao na kuwa aliwataka waachane na Chama cha Mapinduzi kwa kuwa kinasera ya ufisadi kimeshindwa kuwajali watu wake.
Mbowe aliwataka watanzania kujifunza toka katika nchi za marekani,uingereza,Kenya,Malawi,Zambia na zinginezo ambazo wakikiweka madarakani chama furani kama hakikufanya kazi wanakipiga chini kwenye uchaguzi mungine na kuwa hata chadema ikiingia madarakani waipige chini pindi itakavyofanya vibaya.
‘’Haiwezekani lasilimali za nchi zinaendelea kuibwa kuku wakibeba wanyama poli zikiwemo twiga kwenda nje ya nchi kuuzwa alafu muendelee kuwachekea,mwezi wa kumi ndiyo kiama chao chagueni madiwani,wabunge na Rais kutoka Ukawa ili tufanye mabadiriko ya kweli’’alisema Mbowe.
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kwa upande wake aliwapongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuwa ndiyo ishara tosha ya anguko la CCM katika uchaguzi mkuu wa mwezi wa kumi katika ngazi zote.
Alisema Rais Jakaya Kikwete alimzawadia Mbunge wa Kyela Harrison Mwakyembe uwaziri wa uchukuzi kwa lengo la kuiba kamailivyojulikana baada ya kununua mabehewa mabovu pamoja na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari kwa chama chake bila kufuata utaratibu huku jimbo la Kyela likizidi kuwa hoi kiuchumi.
Mwisho.






No comments: