VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Thursday, January 29, 2015

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO. BAVICHA WILAYA YA YA ILEJE. TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI KUFUATIA UHAMISHO WA MSNYANYASO NA KINYUME CHA SHERIA KWA WATUMISHI WA UMMA.





Taarifa hii ni maalumu kwa umma na vyombo vya habari kwa kukemea,kulaani na kupinga vikali vitendo vya uonevu na unyanyasaji kwa watumishi wa umma hususani walimu ILEJE wanao unga mkono harakati za mageuzi ya kisiasa kupitia CHADEMA na washirika wake ie UKAWA.Uonevu na unyanyasaji huu unafanywa na baadhi ya mamlaka za Kiserikali kwa ushirika na CCM kwa kukiuka waziwazi katiba,sheria na kanuni zote zinazo husu utumishi wa summa (shinikizo toka CCM kufuatia katibio la anguko lake)


Ndugu Wananchi,CHADEMA kupitia BAVICHA tunaomba ifahamike kuwa hakuna sheria yeyote katika vitabu vya sheria inayokataza watumishi wa umma hususani walimu ama watumishi wengineo isipokuwa baadhi ya makundi kujihusisha na siasa ama za upinzani au chama tawala katika kipindi husika.,Na hakuna sheria ama kanuni inayoelekeza ama kulazimisha watumishi wa umma kuwa wapambe,wakereketwa,mashabiki ama wanachama wa chama tawala tu yaani CCM isupokuwa upinzani.

Ibara ya 20(1) ya katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa "Kila mtu anao Uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani ,kuchanganyika,kushirikiana na watu wengine na kwaajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na kuanzisha na kujiunga vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kubifadhi au kuendeleza inami au maslahi yake au maslahi ya wengine"

Ibara ya 20(4) ya Katiba hiyo hiyo inaeleza kuwa "Itakuwa ni marufuku kw mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au shirika lolote au kwa chama chochote cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwasababu tu ya itikadi au falsafa ya chama hicho".Rejea pia Uhuru wa MTU kushirikiana na wengine sheria ya 1984 Name.15 in 6, she ria ya 2005 Na 1 ib 7.

Kwa kuzingatia vifungu hivyo vya katiba na sheria si shaka kuwa hakuna Mwalimu anayekayazwa kuwa CHADEMA kwani hata sheria nakanuni zinzotokana na katiba hazikatazi.Kwa mujibu wa kanuni za maadili ya utendaji wa utumishi wa umma toleo la 1998 kanuni namba 9(1) inaeleza kuwa KILA MTUMISHI ANAYO HAKI YA KUSHIRIKI MASUALA YA SIASA,na toleo la mwaka 2005 kanuni namba 5 (1&2) inaeleza kuwa WATUMUSHI WANAYO HAKI YA KIDEMOKRASIA KUSHIRIKI MASUALA YA SIASA NA KUWA NA VYAMA.

Hivyo kwa kuzingati katiba ,sheria na kanuni hizo za utumishi wa umma BAVICHA tunalaani vikali vitendo wanavyofanyiwa watumishi wa umma hususani walimu kwasababu tu ni wakereketwa,mashabiki na wanachama wa CHADEMA.

Tunalaani kitendo cha serikali kupitia Mkurugenzi wa wilaya ya ILEJE na Afisa utumishi wa wilaya kutishia kuwafukuza kazi na kuwahamisha vituo vya kazi bila kufuata sheria za utumishi wa umma mwalimu Emmanuel Mbuba aliyekuwa Ileje day,Lusekero Mwasasumbe wa Luswisi na Edgar Katembo aliyekuwa ILEJE day kwa Kile kinacho daiwa ni wafuasi wa CHADEMA. Na kama hiyo haitoshi wamewahamisha vituo vyao vya kazi pasipo kuzingatia kanuni za utumishi wa umma ambazo zinaelekeza kuwa uhamisho ufanyike Mara baada ya mtumishi kuhudumu kituo chake kwa muda wa miaka mitatu (3) lakini imekuwa kinyume kwa watumishi hawa kwani wamehamishwa kwa shinikizo la kisiasa toka CCM. Ifahamike kuwa hata kama ni wafuasi wa CHADEMA hawakupaswa kupewa kile kinacho itwa uhamisho wa kukomoa kwani hakuna sheria inayo kataza wao kuwa CHADEMA.

BAVICHA tunatambua kuwa pasipo chembe ya hofu wala shaka ,kuwa kitendo hiki ni shinikizo la CCM kwani historia inaonesha 1/8/2013 Mkurugenzi wa wilaya wakati huo alipewa shinikizo na Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Taifa Abdah Bulembo la kutoa uhamisho wa kukomoa kwa Mwalimu Bahati Nkota kwa Kile kilichoitwa yupo CHADEMA na si vinginevyo. Ikiwa ni mwendelezo ule ule tunatambua kuwa uhamisho wa na vitisho kwa mwalimu Emmanuel Mbuba,Edgar na wengineo unatokana na maazimio ya kikao cha CCM kilichofanyika Mbeya novemba 2014 ambapo kilihudhuliwa na Mkurugenzi ILEJE, Mkuu wa Mkoa, Aliko Kibona (MB) na makaada wengine waaminifu wa CCM ILEJE ambapo pamoja na mambo mengine kilijadili kuwashughurikia kwa namna yeyote ile watumishi wote hususani walimu wote wanao unga mkono upinzani kwa namna yeyote ile.

BAVICHA tunahoji, kama kweli sheria inakataza watumishi kushiriki siasa inakuaje kwa walimu Wito Mlemelwa, Said Ngondo wa Lubanda,Magelanga wa Mkumbukwa,Yoloda Kilonge wa Lubanda,Simbeye wa Nakalulu na Sanga wa Ilulu ambao ni makaada watiifu wa CCM mbona hawapewi kalipio? Au ni kwa CHADEMA tu?

BAVICHA tunamtaka Mkurugenzi akome Mara moja kutumika na CCM ili kukandamiza upinzani kwani kwa namna yeyote ile hayoweza kuzuia mabadiliko haya ya kisiasa wilayani ILEJE kwani ni kama mafuriko hivyo hatoweza kuzuia kwa mikono ama namna yeyote ile, YASIJE MZOA PIA.

Pia tunakishauri chama cha walimu ILEJE (CWT) kukemea kwa vitendo manyanyaso na uonevu wa aina yeyote unaofanywa kwa wanachama wake kwani wamekuwa wakichangia michango na gharama za uendeshaji wa CWT hivyo ni vema umoja huu ukatimiza wajibu wake pia kwa kuwalinda wanachama wake pindi wanapo kandamizwa.

MUHIMU: tunataka Mkurugenzi na makundi mengine watambue kuwa BAVICHA hatupingi kuhamishwa vituo vya kazi watumishi wa umma Bali tunataka uhamisho uwe wenye haki kwa kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma na si shinikizo toka CCM.

Imetolewa na Gwamaka Mbughi.
M/kiti BAVICHA ILEJE.
+255 764 107 610..

Nakala kwa Mkurugenzi
Nakala CWT ILEJE.

No comments: