VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Saturday, April 11, 2015

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ( CHADEMA) WILAYA YA ILEJE .




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUPIGWA KWA WANACHAMA WA CHADEMA NA KIKUNDI CHA ULINZI CHA CHAMA CHA MAPINDUZI MAARIFU KAMA GREEN GUARD KATA YA ITALE PAMOJA NA USHUSHAJI NA UCHOMAJI WA BENDERA ZA CHADEMA.

Ndugu Wanahabari, Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) wilaya ya Ileje kinawashukuru kujitokeza kusikiliza na kuchukua Habari hii ili kuufahamisha umma wa watanzania.


Ndugu Wanahabari, Mtakumbuka mwishoni mwa mwezi machi 2015 wanachama wa chama cha Mapinduzi( CCM) kwa ufadhili wa  JANET MBENE( mb) na ALIKO KIBONA( mb) walianzisha kambi ya kama vile Mafunzo ya Judo na kareti pamoja na Mafunzo mengine katika msitu mkubwa katika kata ya Itale wilayani Ileje na kulala katika shule ya msingi Itale.

Ndugu Wanahabari, Katika Mafunzo hayo ya vijana wa Green guard kuliambatana na maeneno na maagizo ya kuwashughulikia watu na wanachama wa vyama Vingine hasa CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI kwa kuwapiga,kuwateka pamoja na kuharibu vifaa vya uenezi vya vyama hivyo.

Ndugu Wanahabari, Kwa mujibu wa katiba ya nchi ya mwaka 1977 ibara ya 20(4) inatoa haki kwa kila mtu kujiunga na chama chochote cha siasa anachokitaka.Pia katiba ya nchi hiyohiyo ya mwaka 1977 ibara ya 18 inatoa haki kwa mtu yeyote kuwa na mawazo au maoni yake( UHURU WA MAONI NA FIKRA).Sasa CHADEMA tunajiuliza inakuaje kauli za CCM kwamba wapinzani washughulikiwe wakati vyama vyao vya siasa vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa Namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 8(1),(2),(3),(4) pamoja na kifungu cha 10(1) (a),(b),(c) na (d) ??.


Ndugu Wanahabari, Pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 147(1) inasema " Ni marufuku kwa mtu yeyote au shirika lolote au KIKUNDI chochote cha watu,isipokuwa serikali kuunda au kuweka jeshi la aina yoyote", Chama cha MAPINDUZI kupitia mtumishi wa umma WITO MLEMELWA( Mwalimu ) kama Green guard wa CCM Pamoja na maelekezo ya Mafunzo ya kijeshi ambaye ni askari wa jeshi la polisi wamevunja katiba ya nchi.

Ndugu Wanahabari ,Mafunzo hayo ya kupiga watu na wanachama wasioamini katika chama cha MAPINDUZI yanatolewa na viongozi wa umma amabao ni wito Mlemelwa( Mwalimu mkuu shule ya Msingi Rungwa wilaya ya Ileje),Lucas Mwashibanda( askari wa jeshi la polisi) kinyume na katiba ya nchi ya mwaka 1977 ibara ya 147(3) inayokataza mwanajeshi yeyote akiwepo askari wa jeshi la polisi kujiunga na chama cha siasa.CHADEMA tunaitaka serikali kumfukuza kazi haraka sana Lucas Mwashibanda anayetumia Mafunzo ya jeshi kuwafunza vijana wa Green guard kwa ajili  ya kudhuru wanachama wengine wasio wanaccm lakini kuvunja katiba ya nchi makusudi.


Ndugu Wanahabari, baada ya Mafunzo hayo,Mbunge wa Ileje ALIKO KIBONA na mkuu wa wilaya ya Ileje ROSEMARY SENYAMULE SITAKI walihitimisha Mafunzo hayo tarehe 03/04/2015 Itale.Mara baada ya kuhitimisha ,vijana wa Green guard waliaanza rasimi kupiga,kutesa na kuteka wanachama wa CHADEMA ambapo wanachama 6 walipigwa na Bendera 16 za CHADEMA zilishushwa na kuchomwa moto tarehe 04/04/2015.Hii haikubaliki.

Ndugu Wanahabari, Mpaka sasa,vijana hao wa CCM wameshusha Bendera moja katika soko la itumba na sasa wanampango wa kuteka vijana na wengine wanachama akiwepo COSMAS JIMMY MWAMPASHI,DANIEL EZEKIEL MSWELO,GWAMAKA KAGHOMBE MBUGHI, na wengineo ili watekwe na kupigwa vikali pamoja na kuadhibu vijana wengine wasipenda CCM.Huku ni kutapatapa kwa kifo cha CCM na siasa hizi za maji taka( GUTTER POLITICS) zinasadifu kwamba CCM inakufa kifo halisi( NATURAL DEATH) na sasa imekosa kabisa uvumilivu wa kisiasa( Lack of Political tolerance) na hivyo kukosa Demokrasia kabisa.

MATAMKO KUHUSU MATUKIO NA MIPANGO HIYO MICHAFU YA CCM.

1/CHADEMA ileje tunalaani vikali wanachama wetu kupigwa,kuteswa na kutishwa pamoja na kuwindwa.Tunalaani vikali unyama huu na rafu hizi chafu za CCM.

2/Tunaitaka serikali kumfukuza kazi askari wa Jeshi la polisi LUCAS MWASHIBANDA Kwa kukiuka maadili ya kazi yake na kuvunja katiba ya nchi ya mwaka 1977 ibara ya 147(3).


(3) Pia Chadema tunaitaka Serikali kumfukuza kazi mwalimu WITO MLEMELWA kwa kuacha kufanya kazi zake za ualimu na kujihusisha katika kutoa Mafunzo ya kwa vijana wa Green guard msituni.

(4) CHADEMA tunalitaka jeshi la polisi wilaya ya Ileje kuwasaka na kuwakamata vijana wa CCM wote waliohusika kupiga,kuteka wanachama wa CHADEMA pamoja na kuchoma Bendera 17 za CHADEMA Kata ya Itale na Itumba.


Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.


       Imetolewa na...

.................................................................
COSMAS JIMMY MWAMPASHI
MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA CHADEMA WILAYA YA ILEJE

NAKALA

1/WAANDISHI WA HABARI
2/OCD WILAYA YA ILEJE
3/RPC MKOA WA MBEYA
4/CHADEMA MKOA WA MBEYA
5/CHADEMA NYANDA ZA JUU KUSINI
6/CHADEMA
TAIFA(MAKAO MAKUU)
0718083536
jimmy.cosmas@yahoo.com

No comments: